Jeshi la Warumi

Jeshi la Warumi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
150px-Roman_Military_banner.svg.png


Alama ya jeshi la Warumi

Jeshi hilo lilianza c.500 BC



Katika kipindi cha c.500BC mpaka c. 300BC jeshi la Warumi liliongozwa kwa vita vya vidogo vilivyoambatana na maandamano ya askari. Mfumo mzima wa jeshi ulikuwa nukuu ya jeshi la Ugiriki chini ya Alexander the Great, kuanzia muundo mpaka vifaa vya jeshi. Jeshi hili liliratibiwa kwa annua levy

Majukumu ya jeshi yakiwa

1. Kupanga na kukusanya kodi kwa mujibu wa sheria.
2. Kukusanya na kufundisha askari kwa mujibu wa sheria.
3. Kuanzisha mashambulizi na kuteka mali kwa mujibu wa sheria.

Askari waliotembea kwa miguu (infantry soldiers) walikuwa watu wa tabaka la chini, maofisa (calvalry) walikuwa watu wenye kutoka familia zenye uwezo, sababu kubwa ikiwa maofisa walihitaji kutembea kwa farasi na ni wenye uwezo tu ndiyo walikuwa na uwezo wa kumudu gharama. Kiongozi mkuu wa jeshi (Command in Chief) akiwa ni mfalme. Kuanzia mwaka c.508 Warumi hawakuwa na mfalme, hivyo iliamuliwa kuwa kila kiongozi wa sehemu ya utawala (Consuls) watakuwa command in chiefs wa majeshi yao. Consuls waliongoza jeshi lao lakini pia walitoa ushirikiano kwa majeshi mengine yaliyokuwa chini ya utawala wa Warumi yalipohitaji msaada.

Kila mwanaume mwenye umri wa miaka 16-45 kwa mujibu wa sheria alitakiwa kujiunga na jeshi. Jeshi la mwanzo la Warumi lilikuwa na askari 3,000 wa miguu (infantry) na maofisa (calvalry) 300
200px-Helmet_typ_Weissenau_01.jpg

Helmet hii ilivaliwa na askari wa miguu.


Jeshi la Warumi linajulikana kwa mchango wake katika kupanua dola ya Warumi kwa miengo mingi. Raia na wanajeshi waliamini na walikariri kuwa baba wa mwanzilishi na mwanzilishi wa jeshi la Roma ni mungu wa vita na ndiye aliyewaletea baraka na rehema na heshima zote zimuendee yeye.

Wanawake hawakuruhusiwa kujiunga na jeshi la Roma, ni wanaume tu. Kadiri makoloni yalivyoongezeka jeshi lilianza kuajiri aina mbili ya askari, Ligionaries (wazawa)na auxiliary.

Legionaries (wazawa), hawa walipata mafunzo ya hali ya juu na ilikuwa ni lazima uwe na umri wa miaka 17 na kuendelea pia uwe raia wa Roma, ili kujiunga na kikosi cha legionary. Kila aliejiunga na kikosi hiki ni lazima awe mwenye afya njema na mzuri wa kulenga shabaha. Ukikosa sifa hizo mbili uliachwa.

Mkataba wa legionaries ulikuwa ni kutumikia miaka 25 jeshini, kama utabahatika kuishi katika miaka hiyo 25 siku ya kustaafu unapewa kipande cha ardhi ili ulime na askari wasaafu walijengewa miji yo iliyoitwa 'colonia'.

Askari wa nchi koloni walichukuliwa kama auxiliary, hawa hawakupata ujira sawa na askari wa Roma, walipata 1/3 ya pesa waliyopata legionaries na katika vita walipelekwa kwenye mashambulizi hatari, wengi walifia vitani.

Majukumu ya kiutawala katika jeshi la Roma.
Jeshi la Roma liliweza kuwa na askari laki tano kwa wakati mmoja. Ili kuwezesha utawala jeshi hilo liligawanywa katika makundi ya askari 4,000 mpaka 6,000. Makundi haya yaliitwa legions.

Legions ziligawanywa zaidi katika makundi ya askari 80 hawa waliitwa 'centuries' na wasimamizi wa century waliitwa 'centurion'. Centurion alibeba kipande cha fimbo ya chuma kuonyesha umuhimu wake katika jamii pia kilitumika kupigia askari wasio na nidhamu na walioshindwa kutii amri.

Askari walifundishwa mbinu nyingi za kivita kama vile kurusha mawe kwa adui, kurusha mishale kutumia upinde na pia kuogelea na kumshangaza adui.

Askari wa jeshi la Roma walipata mafunzo mbali mbali na waliweza kupigana kwa kutumia machine, walikuwa na uwezo wa kutembea maili 20 kwa siku wakiwa wamebeba vifaa vyao mgongoni, waliweza kuogelea, kuendesha boat na mashua pia kujenga madaraja ili mradi wamfikie adui.

Askari hawa walifundiwa kutii amri, asiyetii amri alipata adhabu kali, ukikutwa umelala kazini adhabu yake ilikuwa hukumu ya kifo.

Askari hawakuwa vitani wakati wote lakini walikuwa mafunzoni wakati wote. walipata mafunzo ya man-to man fighting. Legionaries walizungukia maeneo waliyoteka na kujenga barabara, na madaraja.
 
Dola ya Kirumi hawa ndiyo waliomsurubu & na kutoa hukumu ya utata hadi kupelekea kifo cha Jesus ?
 
Sometimes Brigedi ya jeshi la kirumi au Legion ilikua na askari 6,666.
 
Hivi jamani watu wenye asili ya kurumi wanapatikana wapi maana washawahi kuitawa isreali lakini chakushangaza wao hawapo lakini isreali bado ipo
 
The core ya Warumi ni waitaliano wa zamani
Yes na wanafanana zaidi na walevantines kama Wasyria,lebanon na Iraq. Kimuonekano wanafanana hata na wagiriki pia.
 
Back
Top Bottom