Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limetoa wito kwa wananchi kuwa waangalifu wakati wa matumizi ya gesi ya majumbani (LPG) ili kuzuia majanga ya moto na milipuko. Katika elimu iliyotolewa na afisa wa jeshi hilo kupitia kipaza sauti, alieleza kuwa matumizi ya mpira wa gesi au valve iliyoharibika kwa zaidi ya miezi mitatu bila kufanyiwa ukarabati ni chanzo kikuu cha uvujaji wa gesi.
Aidha, alionya vikali tabia ya kutumia zana kama plaisi (pliers) kulazimisha kufunga au kufungua sehemu ya valve pindi inapokatika au kugoma. Alisisitiza kuwa kitendo hicho kinaharibu mfumo wa mtungi na kuweka gesi katika hatua ya mwisho ya hatari, ambapo inasubiri cheche ndogo tu ili kulipuka na kusababisha madhara makubwa kwa maisha na mali.