cleokippo
JF-Expert Member
- Dec 21, 2014
- 2,149
- 1,852
MH WAZIRI WA MAMBO YA NDANI, SENGEREMA INALIA-JE, NANI ATASIKIA SAUTI YA WANANCHI?
Kwa kipindi cha hivi karibuni, wilaya ya Sengerema imekuwa ikikumbwa na matukio ya moto yanayo sababisha hasara kubwa kwa wananchi, kinachozid kuumiza ni kwamba karibu kila tukio linapoibuka, matumaini ya wananchi kwa jeshi la Zimamoto huishia kuwa majonzi ktokana na kuchelewa kwa huduma ama kushindwa kabisa kukabiliana na majanga hayo
miongon mwa majanga walioshindwa kukabiliana nayo ni
👉 kuungua kwa MBEYA KITIMOTO
👉 Kuungua kwa NYOTA 5 CAFE
👉 Kuungua kwa MADAM JUICE MGAHAWA
👉 Kuungua kwa ROCK CITY NIGHT CLUB
👉 Kuungua kwa MADUKA YA SIMU MJINI KATI nk
Kati ya matukio hayo yote hakuna tukio hata moja ambalo Zimamoto wamefanikiwa kuzima wala kufika kwa wakati
Mfano: tukio lililotokea jana june/17 katika maeneo ya nyatukala ni mfano halis wa hali hii
Moto ulianza kwenye showroom ya fenicha baada ya uchafu uliokuwa ukichomwa kushika kwenye sofa lililokuwa jirani katika hatua ya mwanzo kabisa
Niliwasilisha taarifa kwenye jeshi la Zimamoto Sengerema kwa lengo la kuzuia moto huo usisambae
baada ya gari la zimamoto kuondoka maramoja kwenda eneo la tukio, nilipewa taarifa dereva wa gari hilo hayupo na jitihada zilikuwa zikifanyika kumpigia simu dakika ziliendelea kuyoyoma uku moto ukiendelea kuunguza mali za wananchi
Shiwroom yote ya fenicha ikateketea
Moto ukasambaa hadi MADAM JUICE MGAHAWA pia ukateketeza mgahawa wote
wakati huo mimi niliyekwenda kutoa taarifa nazungushwa kwa maelezo kwamba dereva bado hapokei simu
swali ambalo wananchi wa sengerema wanajiuliza leo ni moja tu
kama jeshi la Zimamoto haliwezi kufika wakati wa moto, linafika kufanya nini baada ya mali kuteketea?
Huduma ya zimamoto ni huduma ya dharura haipaswi kusubiri mtu 1 , simu 1 au maamuzi yanayochelewesha uokoaji wa maisha na mali za wananchi
Tunaomba mh wazir wa mambo ya ndani kuingilia kati swala hili kwa haraka, tunahitaji uchunguzi wa kina juu ya utendaji wa jeshi la zimamoto wilaya ya sengerema na hatua madhubuti zichukuliwe dhid ya wote watakaobainika kushindwa kutekeleza wajibu wao
Wananchi wanalipa kodi kwa matumaini ya kupata huduma wanapopatwa na majanga
Hawalipi kodi ili washuhudie mali zao zikiteketea uku wakisubiri dereva apokee simu
👉 leo imekuwa showroom
👉kesho itakuwa nyumba ya familia
👉kesho kutwa inaweza kuwa shule
👉siku inayofuata inaweza kuwa hospital
Hatupaswi kusubiri majanga makubwa yatokee ndio tuchukue hatua
tunataka majibu, tunataka uwajibikaji tunataka huduma ya zimamoto inayookoa mali za wananchi kwa wakati si inayofika baada ya mali kuangamia
haya si malalamiko ya mtu 1 bali ni kilio cha wananchi wa sengerema wanaotaka kuona maisha na mali zao vikilindwa ipasavyo