Jeshi laitaja Serikali ya Umoja wa kitaifa ya Myanmar kuwa kundi la kigaidi

Jeshi laitaja Serikali ya Umoja wa kitaifa ya Myanmar kuwa kundi la kigaidi

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Utawala wa kijeshi wa Myamar umelitangaza kundi pinzani la serikali ya Umoja wa kitaifa kuwa kundi la kigaidi na kulishutumu kuhusika na mashambulizi ya mabomu, uchomaji moto na mauaji. Kumekuwa na ripoti za mashambulizi ya kila siku ya mabomu huku makundi ya wanamgambo yakiundwa kukabiliana na jeshi.

Waandanamaji wanaopinga utawala wa kijeshi wameendelea na maandamano kote nchini humo na migomo ya kupinga mapinduzi imedhoofisha uchumi wa nchi.

Hapo jana Jumamosi maandamano yaliendelea katika maeneo kadhaa kupinga utawala wa kijeshi. Watu wapatao 774 wameuwawa na vikosi vya usalama na 3,778 wanashikiliwa kizuizini. Serikali ya Umoja wa kitaifa ambayo inaundwa na wabunge waliondolewa madarakani ilitangaza wiki hii kuanzisha jeshi la ulinzi wa wananchi.

Jeshi la Myanmar limekuwa likijaribu kurejesha utulivu tangu lipindue serikali ya kiraia mnamo Februari mosi na kumshikilia kiongozi wake Aung San Suu Kyi.

Chanzo: DW Swahili
 
Pale unapotumia ubabe pasipohitajika inakuwa mrama mrama mrama... jeahi mbona litakoma
 
Safi waanzishe jeshi la kulinda wananchi na jeshi rasmi wasilitambue hiyo itanoga dawa ya ubabe vurugu
 
Jeshi la myanmar hongera sana tandika hao magaidi ya kizungu mpaka akili iwakae sawa walifikiri hapo ni kwa waarabu wataleta mchezo, chinja kabisa hayo magaidi ya kizungu na vibaraka wao
 
Back
Top Bottom