Jesse John wa TBC Taifa tafadhali tafuta mtoto wa Kiume umuite Haruna Niyonzima

Kwani mbona hata yulemchambuzi alisema Niyo yuko kwenye ubora wake kwa Jana Mwl kashasha
 
Wewe si shabiki wa Simba? Andiko lako linatakiwa kutolitilia maanani au siyo Nifah
 
Umesahau kipindi kile charcoal hundred wakati ule anawapaisha mkia fc club a.k.a wamatopeni?? Nikutesa kwa zamu babu weeee! Ebooo
 
Tulia wewe mleta uzi.. Wanaume wako kazini wewe subiria Africa lyon akunyoe.. Haruna anajua.. Ni fundi
 
inawezekana una mimba katapike urudi mkuu
 
Huyu jamaa ni shida sana! Daily kutoa mapovu tu juu ya watangazaji

Tena hasa wenye ' vinasaba ' vya ' Kimahaba ' na Yanga FC. Wapo wengi sana ila wajitahidi wamuige ' Poti ' Chacha Maginga ambaye ni Yanga FC ' damu damu / kindakindaki ' lakini hutoweza kumsikia ' akitangaza ' kimahaba ya Yanga FC kama wenzie.

Yanga FC endeleeni ' kuneng'eneka ' ila sisi Simba SC tunajua kuwa ' breki ' zenu za Ubingwa zitasimamishwa na Mbeya City na Mbao FC na kama Yanga FC mkizifunga hizo Timu mbili nitapanda Mlima Kilimanjaro ' kifua wazi ' tena kule ' Kileleni ' kabisa.

Nakujua Wewe ni mwana Yanga FC tokea zamani ILA nakutuma kawaambie Yanga FC wenzako kuwa GENTAMYCINE kasema ' fitna ' na ' umafia ' ambao tunaenda kuwafanyieni katika hizo mechi mbili ya Mbeya City na Mbao FC ndipo ' mtatujua ' Simba SC kuwa katika nchi hii sisi ndiyo ' Mababa ' wa ' michezo ya hatari '. Mwambie Salum Mkemi kuwa hongera kwa Kazi kubwa ya ' Kifitna ' aliyoifanya jana Taifa katika Vyumba vya kubadilishia nguo vya Tanzania Prisons baada ya kuwapulizia ' dawa zenu zile ' za ' kuwanyong'onyeza ' Vijana wa Watu hadi waliporudi uwanjani Kipindi cha pili wote walikuwa ' wametota na kuchoka ' kabisa hadi mkawafunga zile Goli zenu za ' kubahatisha ' 2.

Hivi ni kwanini Yanga FC huu ' ujanja ' wao wa ' kuwapulizia dawa za kupunguza nguvu ' Timu pinzani huwa hawaufanyi wakiwa wanacheza na Sisi SImba SC? Huwa ' mnatuogopa ' nini? Ndiyo maana ' tuliwakomoa ' katika zile mechi zenu mbili za CAF ambapo zile Timu zote zilizokuja hapa Dar es Salaam ' tulizitahadharisha ' juu ya huu ' upuuzi ' wenu hivyo mkashindwa kuwafunga goli nyingi na mkaenda ' Kufa ' nyie Uarabuni na ' kufurumushwa ' mashindanoni.
 
Mikia fc,wamezabi fc,wakubebwa fc.
 
Halafu ni vitu vya kawaida sana kwa watangazaji lakini jamaa sijui anachukulia namna gani.!

Vingekuwa ni vitu vya kawaida nisingevipazia sauti humu JF. Jifunze kutumia ' brain ' yako vizuri sometimes sawa?
 
Umesahau kipindi kile charcoal hundred wakati ule anawapaisha mkia fc club a.k.a wamatopeni?? Nikutesa kwa zamu babu weeee! Ebooo

Ulishawahi kumsikia Charles Nkwanga Hillary au Swedi Hussein Mwinyi enzi zao wakiwa wanatangaza mpira wakionyesha ' mahaba ' yao ya wazi kwa Simba SC japo hakuna Mdau wa mpira asiyewajua kuwa Wao ni Mnyama Mnyamani ( Simba SC ) tena wa kindakindaki?
 
Ni ukiukwaji wa maadili ya Kazi hafai

Tena hawafai kweli Mkuu na nadhani huu ni wakati ' muafaka ' sasa Uongozi wa TBC ufikirie tu sasa kumpa ' jukumu ' la Utangazaji ' Poti ' Chacha Maginga peke yake na hawa wengine akina Jesse John na Yanga FC mwenzake Enock Bwigane wapewe tu ' majukumu ' mengine kwani kiukweli wamezidisha ' mahaba niue ' yao kwa litimu ' Libovu ' la Yanga FC.

Na leo kuna uwezekano Mtangazaji Enock Bwigane akautangaza mpira wa Simba SC na African Lyon sasa ole wake awe ' anaikandia ' Simba SC au asiache ' kuwasifia ' Wachezaji wetu akina James Kotei Mascherrano, Shiza Kichuya Robben, Laudit Mavugo Griezman na Jonas Mkude Pogba.

Na kama kawaida yangu leo nitausikiliza huo mpira kwa ' makusudi ' kabisa kupitia TBC Taifa japo najua Sibuka fm na Radio One Stereo nao watakuwepo ' mubashara ' kabisa wautangaza mchezo huo ambao mpaka hivi sasa nimetoka kuangalia ' nujum / utabiri ' kwa Babu Simba SC tunaweza kushinda Goli kati ya 5 mpaka 7 na kuna uwezekano leo Laudit Mavugo Griezman akaondoka na mpira wake kwa ' hat trick '.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…