Jesse Lingard: Mfalme mpya kwenye anga za akina Ronaldo, Messi na Neymar.

Mlianza na rashford sahivi mmehamia kwa lingard sijui mnamsifia kwa lipi jipya
 
MANCHESTER, ENGLAND.

JESSE Lingard???
Ndiyo, Jesse Lingard huyuhuyu unayemjua wewe. Ndiye, mchezaji ambaye yupo kwenye kiwango bora kabisa kuliko mastaa wote unaowafahamu wewe huko Ulaya.
Ni Lingard huyuhuyu ambaye mashabiki wa Manchester United hawamkubali sana. Lakini, ukitafuta ukweli na kama unapewa chaguo la kusajili mchezaji kwa sasa kwa kuzingatia ubora uliopo, ukiwekewa Lionel Messi na Lingard, hakuna atakayekushangaa ukimbeba Lingard. Hahahaha. Hii inahusu kiwango cha sasa cha mastaa hao wawili.
Kwenye mabao 14 ya mwisho yaliyofungwa na Manchester United, Lingard amehusika kwenye nusu ya mabao hayo, kiwango bora kabisa ambacho kinamfunika Messi hadi kuingia anga za mpinzani wake wa miaka yote kwenye soka, Cristiano Ronaldo.
Kwa kukusanya rekodi za mechi tisa zilizopita, Lingard amewaburuza mastaa wote wanaonekana kuwa bora huko Ulaya. Katika mechi hizo timu za mwisho, Lingard amefunga mabao saba na asisti mbili. Rekodi bora kabisa, ambayo hata Messi hazifikii, lakini zikimweka kwenye daraja moja na wakali kama Ronaldo, Neymar na mwenzake Kylian Mbappe. Cheki rekodi za mastaa wengine.

LIONEL MESSI – Magoli 3, asisti 3
Mfalme wa Barcelona na ni mshindi mara tano wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Dunia, lakini kwa kuzingatia rekodi za mechi tisa za mwisho, Messi hatii mguu mbele ya Lingard. Staa huyo wa Kiargentina katika mechi hizo tisa amefunga mabao matatu na kupiga asisti tatu.

ANTOINE GRIEZMANN – Magoli 4, asisti 3
Atletico Madrid itamuuza staa huyo wa Kifaransa kwa pesa nyingi sana kama utahitaji huduma yake kwa sasa. Kwa bei anayouzwa unaweza kuwanunua kina Lingard hata wanne. Lakini, kwa kuzingatia ubora wa kwenye mechi tisa zilizopita, Antoine Griezmann hamfikii Lingard. Mfaransa huyo amefunga mabao manne na asisti tatu katika mechi tisa za mwisho alizocheza.

JESSE LINGARD– Magoli 7, asisti 2
Hii inaitwa usiyempenda kaja.Kama unabisha waulize mashabiki wa Arsenal watakwambia. Lingard si mchezaji anayeshabikiwa sana huko Man United, lakini ukweli utabaki palepale, ndiye mwokozi wa kikosi hicho cha Old Trafford kwa siku za karibuni. Lingard amekuwa kwenye kiwango bora kabisa, ambapo katika mechi tisa za mwisho alizocheza, amefunga mabao saba na kuasisti mengine mawili.

KYLIAN MBAPPE – Magoli 6, asisti 4
Paris Saint-Germain kwa sasa inaitumia huduma yake kwa mkopo, lakini ikifika mwishoni mwa msimu watalazimika kulipa kiasi cha Pauni 165 milioni huko AS Monaco ili kumbeba jumla. Hapa anazungumziwa kinda wa Ufaransa, Kylian Mbappe, ambaye amekuwa moto huko Paris ambapo mchango wake umekuwa kitu muhimu kwelikweli kwa timu. Katika mechi tisa za mwisho, Mbappe amefunga mabao sita na kuasisti manne na hivyo kwenda sawa tu na staa wa Man United, Lingard.

CRISTIANO RONALDO– Magoli 8, asisti 2
Supastaa wa Real Madrid huyu, ambaye kwa siku za karibuni amekuwa akihusishwa sana na mpango wa kuachana na timu hiyo yenye maskani yake huko Bernabeu. Ronaldo amebeba tuzo ya Mwanasoka wa Dunia mara tano na ni mmoja kati ya mastaa makini kabisa katika soka la dunia.
Katika mechi tisa za mwisho alizocheza staa huyo, amefunga mabao manane na kuasisti mawili.

NEYMAR – Magoli 7, asisti 5
Kwa ubora wa kuzingatia mechi tisa za mwisho, supastaa wa Kibrazili, Neymar amewafunika mastaa wote wa Ulaya. Mwanasoka huyo ghali duniani baada ya saini yake kuigharimu PSG Pauni 198 milioni walipomsajili kutoka Barcelona kwenye dirisha lililopita, amehusika katika mabao 12 katika mechi tisa za mwisho, akifunga saba na kuasisti mabao matano.
Lingard yuko level moja na kina nani?????...mkuu naona hauko serious kabisa......sijaelewa huo ujasiri unautolea wapj!!!!!...sijamuona harry kane wala mo salah..hadi sasa najiuliza kwa nn sijawaona hapo...
Kisa kufunga magoli mangapi sijui ndo mmeshamfikisha huko..khaa!!!! Mtu ndo anastruggle kuingia first eleven ila kuna watu washampa ufalme.... Wabongo ni hatare!!!!
 
Kama mimi ndiye mod ningeshaiwasha kiberiti hii mada Messi kawafunika wakina Pele na Maradona alafu unatuletea ka lingard!!! Hata sterling kamfunika mbali tu.....hizi ni dharau kabisa,, mtake radhi mfalme'' please!!!
 
kama ni hivyo bas kuna mkongo mmoja anacheza ligi dalaja la tatu Gabon ndio anaongoza mechi tisa ana magoli 13 na ameassit mara 8 au unaongelea kwa ulaya pekee, anaitwa Enyina Mbolo
 
Mmebadili mawazo sio Marcus Rashford tena?

Sio Anthony Martial mliesema eti ndie mrithi wa Thiery Henry?

Hebu pambaneni na Lukaluka kwanza!
 
Huyo dogo ana safari ndefu sana ya kuwafikia hao uliomfananisha nao.
 
MANCHESTER, ENGLAND.

JESSE Lingard???
Ndiyo, Jesse Lingard huyuhuyu unayemjua wewe. Ndiye, mchezaji ambaye yupo kwenye kiwango bora kabisa kuliko mastaa wote unaowafahamu wewe huko Ulaya.
Ni Lingard huyuhuyu ambaye mashabiki wa Manchester United hawamkubali sana. Lakini, ukitafuta ukweli na kama unapewa chaguo la kusajili mchezaji kwa sasa kwa kuzingatia ubora uliopo, ukiwekewa Lionel Messi na Lingard, hakuna atakayekushangaa ukimbeba Lingard. Hahahaha. Hii inahusu kiwango cha sasa cha mastaa hao wawili.
Kwenye mabao 14 ya mwisho yaliyofungwa na Manchester United, Lingard amehusika kwenye nusu ya mabao hayo, kiwango bora kabisa ambacho kinamfunika Messi hadi kuingia anga za mpinzani wake wa miaka yote kwenye soka, Cristiano Ronaldo.
Kwa kukusanya rekodi za mechi tisa zilizopita, Lingard amewaburuza mastaa wote wanaonekana kuwa bora huko Ulaya. Katika mechi hizo timu za mwisho, Lingard amefunga mabao saba na asisti mbili. Rekodi bora kabisa, ambayo hata Messi hazifikii, lakini zikimweka kwenye daraja moja na wakali kama Ronaldo, Neymar na mwenzake Kylian Mbappe. Cheki rekodi za mastaa wengine.

LIONEL MESSI – Magoli 3, asisti 3
Mfalme wa Barcelona na ni mshindi mara tano wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Dunia, lakini kwa kuzingatia rekodi za mechi tisa za mwisho, Messi hatii mguu mbele ya Lingard. Staa huyo wa Kiargentina katika mechi hizo tisa amefunga mabao matatu na kupiga asisti tatu.

ANTOINE GRIEZMANN – Magoli 4, asisti 3
Atletico Madrid itamuuza staa huyo wa Kifaransa kwa pesa nyingi sana kama utahitaji huduma yake kwa sasa. Kwa bei anayouzwa unaweza kuwanunua kina Lingard hata wanne. Lakini, kwa kuzingatia ubora wa kwenye mechi tisa zilizopita, Antoine Griezmann hamfikii Lingard. Mfaransa huyo amefunga mabao manne na asisti tatu katika mechi tisa za mwisho alizocheza.

JESSE LINGARD– Magoli 7, asisti 2
Hii inaitwa usiyempenda kaja.Kama unabisha waulize mashabiki wa Arsenal watakwambia. Lingard si mchezaji anayeshabikiwa sana huko Man United, lakini ukweli utabaki palepale, ndiye mwokozi wa kikosi hicho cha Old Trafford kwa siku za karibuni. Lingard amekuwa kwenye kiwango bora kabisa, ambapo katika mechi tisa za mwisho alizocheza, amefunga mabao saba na kuasisti mengine mawili.

KYLIAN MBAPPE – Magoli 6, asisti 4
Paris Saint-Germain kwa sasa inaitumia huduma yake kwa mkopo, lakini ikifika mwishoni mwa msimu watalazimika kulipa kiasi cha Pauni 165 milioni huko AS Monaco ili kumbeba jumla. Hapa anazungumziwa kinda wa Ufaransa, Kylian Mbappe, ambaye amekuwa moto huko Paris ambapo mchango wake umekuwa kitu muhimu kwelikweli kwa timu. Katika mechi tisa za mwisho, Mbappe amefunga mabao sita na kuasisti manne na hivyo kwenda sawa tu na staa wa Man United, Lingard.

CRISTIANO RONALDO– Magoli 8, asisti 2
Supastaa wa Real Madrid huyu, ambaye kwa siku za karibuni amekuwa akihusishwa sana na mpango wa kuachana na timu hiyo yenye maskani yake huko Bernabeu. Ronaldo amebeba tuzo ya Mwanasoka wa Dunia mara tano na ni mmoja kati ya mastaa makini kabisa katika soka la dunia.
Katika mechi tisa za mwisho alizocheza staa huyo, amefunga mabao manane na kuasisti mawili.

NEYMAR – Magoli 7, asisti 5
Kwa ubora wa kuzingatia mechi tisa za mwisho, supastaa wa Kibrazili, Neymar amewafunika mastaa wote wa Ulaya. Mwanasoka huyo ghali duniani baada ya saini yake kuigharimu PSG Pauni 198 milioni walipomsajili kutoka Barcelona kwenye dirisha lililopita, amehusika katika mabao 12 katika mechi tisa za mwisho, akifunga saba na kuasisti mabao matano.
Mashabiki wa Man U mna kelele sana. Kelele nyingi utasikia Januzaj anafanana na Zidane, Pogba anafanana na Neymar Jr, Rashford zaidi ya Cr 7, Martial ndie mrith wa Cr 7 mara hakuna straiker kama Lukaku. Sio bureeeee.........! Mechi 9 ndio bora kuliko Messi na Cr 7.
 
Delle Ali ni bora kuliko huyu Lingard
 
Back
Top Bottom