KERO Jeuri ya Makondakta kuongeza nauli daladala za Segerea-Kawe imefikia kiwango cha juu kisicho vumilika. LATRA mmelala?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Joined
May 4, 2024
Posts
37
Reaction score
190
Ni wazi, LATRA kama chombo cha udhibiti kimeshindwa kudhibiti tabia ya Makondakta na Madereva wa daladala za Segerea-Kawe kuongeza nauli kiholela.

Ikifika jioni, daladala hizi zimekuwa na utaratibu wa kuongeza nauli kinyume na sheri, zikidai wastani wa Tsh. 1000-2000 kwa baadhi ya siku.

Kwa leo, daladala yenye usajili wa T 302 DWG imetelekeza abiria waliopandia kawe kwa kuwa waligoma kulipia Tsh. 1500 ili iondoke stand. Kwa bahati mbaya sana, dereva na kondakta pia walikuwa na kauli mbaya kwa abiria, wakiwatisha kuwa hata wakishtaki LATRA hakuna kitakachofanyika.

Kwenu LATRA, ndiyo mmekuwa vibogoyo kiasi hiki? Abiria wa nchi hii, wenye kipato cha kawaida wanaotumia daladala kama chombo chao cha usafiri wakimbilie wapi?

Leo si mara ya kwanza kwa daladala za stendi hii kufanya ujinga wa aina hii. Mara kadhaa hali hii imekuwa inaleta sinfofahamu ambapo baadhi ya abiria wamekuwa wanagoma kukubali kiasi cha hata kupigana na makondakta. Mpaka afe mtu ndo muamke?

Kinyume na jinsi inavyopaswa kuwa, simu za LATRA zimekuwa pia hazipokelewi pindi abiria wanapotaka kutoa malalamiko yao. Wakimbilie wapi?

Nimechoka Sana

1000422845.jpg
 
Kila mtu ale Kwa urefu wa kudu yake ova.
 
View attachment 3449085
Wamechangia chama
 
Nauli inapanda hapo kawe Kwa gari za kawe- segerea kwa sababu kuu mbili

1. Abiria nyie wenyewe kuvunja utaratibu wa kusubiria kitosubiri gari ndani ya kituo na kusubiria kituo kimoja kabla ya kufika kawe, sijui panaitwa kanisani km sikosei na hivyo kutozwa nauli 2, japo lengo ilikuwa ni kupata siti, lkn ikumbukwe, kituo hadi kituo nauli lazima utoe, kwaiyo ukipanda pale kanisani na unaenda segerea atakutoza 500 ya kukufikisha kituoni japo ni karibu na 800 ya segerea!
2. Siku za ibada Kwa mwamposa, magari wanaringa sana na abiria nyie wenyewe mnajipandishia nauli Kwa kugombania hata mkiambiwa 5000🤣🤣🤣🤣
 
Dah "Thed weld dwellers, the 99% na hand to mouth mna safari ndefu sana.

Kwa kadhia hii IQ zenu zitazidi kuwa retarded na stagnant.
 
Nauli inapanda hapo kawe Kwa gari za kawe- segerea kwa sababu kuu mbili

1. Abiria nyie wenyewe kuvunja utaratibu wa kusubiria kitosubiri gari ndani ya kituo na kusubiria kituo kimoja kabla ya kufika kawe, sijui panaitwa kanisani km sikosei na hivyo kutozwa nauli 2, japo lengo ilikuwa ni kupata siti, lkn ikumbukwe, kituo hadi kituo nauli lazima utoe, kwaiyo ukipanda pale kanisani na unaenda segerea atakutoza 500 ya kukufikisha kituoni japo ni karibu na 800 ya segerea!
2. Siku za ibada Kwa mwamposa, magari wanaringa sana na abiria nyie wenyewe mnajipandishia nauli Kwa kugombania hata mkiambiwa 5000🤣🤣🤣🤣
Siyo kweli. Tafuta kitu kingine cha kusema.
 
Ni wazi, LATRA kama chombo cha udhibiti kimeshindwa kudhibiti tabia ya Makondakta na Madereva wa daladala za Segerea-Kawe kuongeza nauli kiholela.

Ikifika jioni, daladala hizi zimekuwa na utaratibu wa kuongeza nauli kinyume na sheri, zikidai wastani wa Tsh. 1000-2000 kwa baadhi ya siku.

Kwa leo, daladala yenye usajili wa T 302 DWG imetelekeza abiria waliopandia kawe kwa kuwa waligoma kulipia Tsh. 1500 ili iondoke stand. Kwa bahati mbaya sana, dereva na kondakta pia walikuwa na kauli mbaya kwa abiria, wakiwatisha kuwa hata wakishtaki LATRA hakuna kitakachofanyika.

Kwenu LATRA, ndiyo mmekuwa vibogoyo kiasi hiki? Abiria wa nchi hii, wenye kipato cha kawaida wanaotumia daladala kama chombo chao cha usafiri wakimbilie wapi?

Leo si mara ya kwanza kwa daladala za stendi hii kufanya ujinga wa aina hii. Mara kadhaa hali hii imekuwa inaleta sinfofahamu ambapo baadhi ya abiria wamekuwa wanagoma kukubali kiasi cha hata kupigana na makondakta. Mpaka afe mtu ndo muamke?

Kinyume na jinsi inavyopaswa kuwa, simu za LATRA zimekuwa pia hazipokelewi pindi abiria wanapotaka kutoa malalamiko yao. Wakimbilie wapi?

Nimechoka Sana

View attachment 3449085
Kifupi Latra WAMELALA. Hawatekelezi majukumu yao.
 
Mbongo akikumudu atakusakama sana. Akipanda boda atalipa ukwasi wa hele na hamna kulalamika, akipanda taski au bajaji vilevile kimyaaa, kumbuka hao boda au bajaji hawapakii wanafunzi kwa bei ya 200 kwao wao ni hela tu. Ila sasa wabongo wakipanda daladala kana kwamba wanajua kondacta kaishia la pili na dereva labda la saba. Hapa sheria zote wanazijua wao. Pamoja na hizo nauli za 1500 hao mnawaona bado wamepanga chumba kimoja.
 
Back
Top Bottom