Jezi feki haziepukiki

Jezi feki haziepukiki

kalipeni

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
1,571
Reaction score
1,328
Nimepitia web ya Chelsea bei ya jezi tshrt pekee usd105 sawa na zaidi ya laki mbili za Tanzania wabongo tutavaa jezi feki tu
 

Attachments

  • Screenshot_20200715-001751.png
    Screenshot_20200715-001751.png
    28.3 KB · Views: 2
Wenye jezi zao waliiona hii
 

Attachments

  • Screenshot_20200715-071136.png
    Screenshot_20200715-071136.png
    50.9 KB · Views: 2
Nafikiri bei za jezi za timu za Tanzania (kwa mfano Simba na Yanga) zinalenga kuwa nafuu kutokana na uhalisi wa kipato cha wananchi. Naomba niwasilishe mfano. Mimi ninaishi Marekani. Mchezo wa kikapu ni maarufu sana hapa. Ukitaka kununua jezi halisi (authentic) ya wachezaji maarufu kama Michael Jordan au Kobe Bryant, inabidi zikutoke kama $300 hivi. Hizi ni jezi (authentic) zinazotengenezwa maalum wakati wakicheza, zinakuwa zimeenda na miili yao ili mchezaji wa timu pinzani hawezi kuzivuta. Ni za kiwango cha hali ya juu sana. Nyingi zinakuwa zinatumia uzi (mshono) kwa namba za wachezaji na jina la timu.
Jezi nyingi ambazo unaona watu wengi wanavaa zinaitwa replica jerseys. Hizi ndizo watu wengi unaona wamenunua. Unaweza kuzipata kwa $50 mpaka $100, kutegemea na umaarufu wa mchezaji pamoja na timu anayochezea.
Hizi jezi zinatengenezwa kwa viwango vya juu sana. Ukiishika tu utaelewa. Kama timu za Tanzania zikitengeneza kwa viwango kama vya huku, sidhani kama kuna watu wengi watanunua kutokana na kuwa ghali sana.
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom