lewis mtunze
Member
- Aug 31, 2020
- 42
- 26
Jezi ya yanga iko poa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Weka na home kit kwa kwa upande wa yanga then ndio tupige kura, usiwe biased
Atlas copco
Acha kufananisha jezi za timu ya Mpira v/s Atlas za kujifunzia shuleni
Kwa kuwa ina AtlasJezi ya Yanga bado vizuri inafaa hata kuinunua 35000 ya Simba quality yake ni 15000
Hv jezi ya timu gan ya Taifa na hata Klabu ina Raman?Jezi ya Yanga ni nzuri.
"Usifananishe jezi na vitambaa vya mganga."
Kijana naona unajipa moyo kulinganisha JEZI BORA barani Afrika na yale MADEKIO YA MTUMBA kutoka kkooo[emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji12]
Hv jezi ya timu gan ya Taifa na hata Klabu ina Raman?
Sent from my SM-N910F using JamiiForums mobile app
Kiujumla zote ni jezi nzuri, lakini zina Kasoro nyingi za kimsingi ambazo wahusika wanapaswa kuzifanyia kazi.
Kwa mfano;
Simba jezi yake kitu kizuri cha upekee ni ufito/mkanda wa rangi tofauti kwenye kingo za mikono na shingo, tofauti na hapo jezi yote ni nyekundu/nyeupe hivyo inakosa ile Vibe ya kimishezo. Yaani kama ukitoa nembo zote kwenye jezi, kitakachoonekana hapo ni fulana yenye rangi moja! Hivyo kuifanya kuonekana kama fulana ya kawaida sana.
Kama ningekuwa mbunifu wa jezi ya Simba basi miraba ya rangi nyeupe/nyekundu ingepaswa kupita pia nyuma na mbele kuzunguka hiyo jezi.
Yanga jezi yake ina mpangilio mzuri wa miraba yenye rangi za kuvutia, kiasi ambacho inaleta upekee na kuleta Vibe ya kimichezo, tatizo ni kuwekwa hiyo ramani ya Afrika kubwa tena ubavuni, na wakati huo huo upande wa juu pembeni ya kifua kuna nembo ya GSM yenye ramani ndogo ya afrika tena! Badala ya kuvutia imegeuka na kuchefua, yaani imekuwa kituko tena.
Kama ningekuwa mbunifu wa Yanga, basi hiyo ramani kubwa ningeiondoa kabisa kwa kuwa haina maana na wala haiwezi kuongeza mvuto wowote.
Hitimisho langu la kiuchambuzi hapa JF ni kuwa Jezi ya Simba imerahisishwa sana kiasi cha kukosa mvuto wa kimichezo na Jezi ya Yanga imepambwa sana kiasi cha kuharibu mvuto wa kimichezo.
Simba Ni ya kifootball Zaidi, ila yanga ya kwendea kanisani na kujifunzia jiografia[emoji23][emoji23][emoji23]
Quality inapimwa na macho? Jezi za Simba zinatengenezwa na kampuni ya michezo ya uhlsport za yanga zinatengenezwa na kampuni gani?
Hiyo kampuni uhlsports inamilikiwa na nani na ina kiwanda wapi cha jezi? Hapo ndipo mtamjua mo dewji kwa nini akiulizwa bilioni 20 anakuwa mkali