Kiujumla zote ni jezi nzuri, lakini zina Kasoro nyingi za kimsingi ambazo wahusika wanapaswa kuzifanyia kazi.
Kwa mfano;
Simba jezi yake kitu kizuri cha upekee ni ufito/mkanda wa rangi tofauti kwenye kingo za mikono na shingo, tofauti na hapo jezi yote ni nyekundu/nyeupe hivyo inakosa ile Vibe ya kimishezo. Yaani kama ukitoa nembo zote kwenye jezi, kitakachoonekana hapo ni fulana yenye rangi moja! Hivyo kuifanya kuonekana kama fulana ya kawaida sana.
Kama ningekuwa mbunifu wa jezi ya Simba basi miraba ya rangi nyeupe/nyekundu ingepaswa kupita pia nyuma na mbele kuzunguka hiyo jezi.
Yanga jezi yake ina mpangilio mzuri wa miraba yenye rangi za kuvutia, kiasi ambacho inaleta upekee na kuleta Vibe ya kimichezo, tatizo ni kuwekwa hiyo ramani ya Afrika kubwa tena ubavuni, na wakati huo huo upande wa juu pembeni ya kifua kuna nembo ya GSM yenye ramani ndogo ya afrika tena! Badala ya kuvutia imegeuka na kuchefua, yaani imekuwa kituko tena.
Kama ningekuwa mbunifu wa Yanga, basi hiyo ramani kubwa ningeiondoa kabisa kwa kuwa haina maana na wala haiwezi kuongeza mvuto wowote.
Hitimisho langu la kiuchambuzi hapa JF ni kuwa Jezi ya Simba imerahisishwa sana kiasi cha kukosa mvuto wa kimichezo na Jezi ya Yanga imepambwa sana kiasi cha kuharibu mvuto wa kimichezo.