Mkuu unafuatilia mpira kweli au ndy wale wanaojua kulaumu tu? bila ya kufanya uchunguzi kwanza. Umeambiwa CAF inazitaka team ziwe na jezi aina tatu tofauti, sasa simba tayari ina 2, kwahy kuna ubaya gani wakiongeza rangi nyingine? Kadri siku zinavyokwenda na mambo yanabadilika.
Kanuni na taratibu za mpira wa miguu zinabadilika ili kukidhi matakwa na mahitaji ya kipindi husika, kwahy hili suala la kuongeza rangi nyingine haliepukiki na me binafsi nimelielewa sana. Alafu rangi ikiwa ni zilezile zinachosha sana, sema sisi huu ujinga wa usimba na Yanga unatuharibu na kuzidi kudumaza akili zetu.
Duniani kote team kubwa kubwa kama unafatilia vzr, wana jezi aina tatu, na mara nyingi huwa zinabadilika badilika ktk rangi, hasa hizi za away, sasa simba ni nani wasifanye hvy, ikiwa ndy team pekee Tanzania inayoonesha ishara kuwa inataka kujipambanua kama ni team ya kisasa kwasababu ya aina ya utofauti ya mmb inayoyafanya hasa kipindi hiki cha miaka mitatu tangu mabadiliko ya uendeshaji wa club yafanyike.