Jezi za Taifa stars kutolewa hovyo kama njugu bila uwoga wowote tuhesabie ni upigaji?

Jezi za Taifa stars kutolewa hovyo kama njugu bila uwoga wowote tuhesabie ni upigaji?

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
12,207
Reaction score
26,521
Moja kwa moja,

Barabarani na kwenye nimekutana na Jezi tofauti za Taifa stars Og zaidi ya ishirini na kitu ndani ya msimu mmoja za aina tofauti tofauti kinyume na zile rasmi zilizotambulishwa na Tff kwa matumizi ya wachezaji na mashabiki wa Taifa stars.

Jezi zenyewe ni hizo hapo chini zinatengenezwa na kampuni ya Uhlsports ambayo inatambulika kama mtenenezaki rasmi wa Jezi za Taifa stars.
IMG_20230117_173131.jpg


Katika hali isiyotarajiwa mtaani kuna Jezi nyingi tena imetengenezwa na material Og sio za kuchovyekwa ambazo zina nembo ya Taifa Stars .Hizo Jezi jina la kampuni limebadika sasa ina chapa ya 'Johsports' na zimepata mwamko mkubwa watu wengi wanunua hizo kuliko zile rasmi zilizotambulishwa.

Picha kwa uchache hizo Jezi zenyewe.
IMG_20230117_173342.jpg


IMG_20230117_173209.jpg


Hawa jamaa wanafyatua vitu tu..
IMG_20230117_173244.jpg


IMG_20230117_173149.jpg


MASWALI YA KUJIIULIZA.

1. Je Johsport wanamkataba ramsi wa kutengeneza Jezi za Taifa stars? kama ndio lini waliopewa hiyo kandarasi na kwa nini watoe Jezi hovyo kama njugu ndani ya msimu mmoja kitu ambacho ni kigeni sana kwenye soka?

2. Kama hawana Kandarasi hiyo kwa nini wapo huru sana na hakuna tamko lolote kuhusu wao na wahusika kuchukuliwa hatua

#UziTayari
 
Mi naona hapo hizo ni nguo zilizoandikwa jina la nchi kama uzalanendo tu

Kwasababu hazina logo ya TFF inayoweza kuashiria moja kwa moja kuwa ni jezi ya timu ya Taifa

Hapo ni sawa na utoe hilo neno Tanzania halafu uweke jina la nchi yeyote tu sidhani kama itaweza kuleta maana ya jezi ya timu ya taifa husika.
 
Sijaona nembo yoyote ya Taifa Stars hapo. Tena hata nembo ya TFF hawajaweka. Huu ni ubunifu mzuri.
 
TFF ya Wallace Karia haijitambui. Inavizia mapato kiduchu kupitia faini za makosa ya timu, wachezaji na makocha.
 
Huyo Johsport nitaenda kumuungisha ana vitu vikali sana
Sana zaidi ya sana ,anavitu vingi vya Tanzania vya ukali kuwazidi hata watengenezaji wakuu na amefanya watu waache kununua Jezi rasmi za Taifa stars kwa sasa .
 
Sijaona nembo yoyote ya Taifa Stars hapo. Tena hata nembo ya TFF hawajaweka. Huu ni ubunifu mzuri na nadhani ni ubunifu mzuri.
Kama hivyo basi kacheza kama Pele kwa kuepuka makosa ya kisheria .
 
Hayo ni mavazi tu ya kizalendo na anafanya vizuri hata vitu vyake ni vikali hatari kuliko vile vya watengenezaji rasmi vimekaa kishamba sana johsports amekaa kijanja zaidi, waruhusiwe maana ni mbinu moja wapo ya kulitangaza Taifa letu wasimbughudhi kabisa
 
Wasiishie tu kwenye jezi. Wengine tunasemaga serikali iachane na mambo ya kuunda kamati za kubuni mavazi ya taifa, watu na sekta binafsi ndiyo njia sahihi. Sasa hapo awepo huyu halafu waje washindani wake kama wawili utaona vitu vitakavyotoka hapo. Wakiwa wajanja design zingine ziwe simple sana na wasiweke hata jina Tanzania au bendera.
 
Hakuna shida hapo..ndio ajira zenyewe hizo na uzalendo
 
Mkuu adriz huyo johsport hatengenezi jezi za Taifa Stars, yeye anatengeneza jezi za kawaida tu ila anaziweka nakshi ya Tanzania. Kisheria amekwepa kosa japokuwa lengo lake ni dhahiri anazuhusianisha jezi zake na Taifa Stars.
 
Sijaona nembo yoyote ya Taifa Stars hapo. Tena hata nembo ya TFF hawajaweka. Huu ni ubunifu mzuri.
Ndiomaana kwenye uhlsport wao wameandika johnsport, nafikiri ni John ameamua kufanya biashara
 
Iko hivi, jezi za team ya taifa yeyote anaweza kutengeneza bila stickers maalum na logo halisi ya TFF, ukiachana na jezi za team za nje ndio jezi pekee mtu anaweza zama China au Turkey kuibuni na kuleta sokoni Tz.

Tanzania ni moya ya sehem rahisi kwa ukanda wa Africa kuuza brand za mavazi ambazo sio OG bila ya shida.
 
Hii ya Adidas haijawahi kuwa official jersey na ipo Sokoni tokea zamani mpk sasa na zipo aina tofauti tofauti mpaka za Nike nimewahi kuiona imeandikwa Taifa stars..
IMG_20230126_124811.jpg
 
Cheki unyama mpya huu, nashauri TFF waongee na hawa jamaa wawe wanatoa official za Taifa stars watauza sana.
IMG_20230415_081507.jpg


IMG_20230415_081452.jpg
 
Back
Top Bottom