Preta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 24,320
- 18,852
Jana niliongea na Mwita Maranya. Kimsingi tumeeelewana kuwa safari ya siku 1 ni fupi sana. Ingawaje inawezekana Mwita Maranya hatokuwepo, lakini ameshauri uwe na angalao siku 2. Tarangire au manyara. Then one of the day tukae tukiongea na kufahamiana. Mimi binafsi nakubaliana naye. Tunahitaji kufahamiana na kujuwana. Tofauti zetu za kisiasa na kimtizamo hazina nafasi kwa sasa. Kuna watu kama malaria Sugu humu ni mmoja wa jamii yetu! Tumtupe! Jibu ni HAPANA. ni wakati sasa tukakaa na kujuawana na kuelimishana. Sidhani kila jamii huwa na wazo moja. Kila familia huwa na watu wenye wazo tofauti na hapo jamii husika hulifanyia kazi wazo hilo. Ni wajibu wa kila mwanajamii forum mwenye nafasi siku husika kujumuika nasi pamoja. Idumu Jamii forum.
Kwa wale wlioko Moshi, naomba wani pm tujuane na ikiwezekana tujiandae kwa safari ya tarehe hiyo. Tupeane ushirikiani kwa hili.
Nawasilisha
hii inatia moyo sana.....kwa taarifa tu kidogo ni kwamba saa hii ndio tumeachana....tulikuwa na kikao kitamu mnoooooo......kwa kweli mimi binafsi sikutaka kiishe....lakini kutokana na majukumu imebidi.....ila big up sana kwa wote walioshiriki....na hata ambao hamkuwepo tuliwawakilisha........JF NI ZAIDI YA KEYBOARD.....luv you all