jf Doctor hivyi kwa nini?

ng`wana ong`wa kulwa

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
2,420
Reaction score
1,752
Binafsi nimekuwa nikijiuliza ni kwa nini wachangiaji katika jukwaa hili ni wachache? lakini kwa uchunguzi wangu nimekuja kugundua kuwa watu wenye uwezo wa kuchangia jukwaa hili ni wengi sana.Kilicho nishitua zaidi ni ID.za watu niliowajua waliokuwa wakitoa michango yao mizuri wameipa kisogo site hii utaona wakichangia kwenye jukwaa la siasa nk.

kwa mawazo mengine mtu mwingine anaweza kusema ma Doctor ni wachache na wataalamu wengine wa afya ni wachache kitu ambacho si kweli maana kuna wengine wana uwezo wa ku google na kutoa mchango wao vizuri sana.

Nilichogundua mimi pamoja na wewe unakaribishwa kutoa maoni yako nini ila nilichoona ni kuwa watu wengi wanapo post shida zao jf Doctor wanaondoka,kama mjuavyo kuna mambo mengi kabla hujaanza kumshauri mtu nini cha kufanya, mfano unaweza taka kujua uzito,umri maana dawa nyingi zinatumika kulingana na kilo za mgonjwa,sasa wataalamu wakiuliza unakuta muulizaji hajibu chochote.mbona majukwaa ya mahusiano,siasa wengi wanaopost hutulia kuangalia michango na kujibu maswali huku si zaidi sana maana inahusiana na uhai.

Kutokana na hili wengi wameona ni kupoteza muda unataka kumsaidia mtu asiyekuwepo kukujibu hata maswali ya msingi,kumbuka muda anaokusaidia huenda kuna mgonjwa amemuomba asubiri kidogo huku akikujibu wewe uliyepost.

Kabla sijakukaribisha wewe kwa mchango wako niombe wataalamu turudi tusaidie wadau angalau wale wanaokuwepo kujibu maswali tusikimbie jukwaa hili.
 
Bado naisoma tena na tena lakini sijapata ujumbe uliodhamiriwa.

Inaweza kuwa vizuri iwapo utai-rephrase hoja uliyodhamiria...
 
hawakuongezewa mishahara
 
Bado naisoma tena na tena lakini sijapata ujumbe uliodhamiriwa.

Inaweza kuwa vizuri iwapo utai-rephrase hoja uliyodhamiria...

Ninachotaka kujua ni kwa nini wachagiaji ni wachache na wengine waliokuwepo wengine hawachangii tena naona umenielewa.
 
Mkuu mie naona kikubwa zaidi ni pale watu wanaposhindwa kutoa historia yao hili wapate msaada. Ndio maana mara nyingi ni bora kumshauri mtu aende hospitali baada kumtajia vitu basic kuhusu tatizo lake.

Kingine ni vizuri watu walete feedback baada kupata ushauri hili wengine wajifunze.
 

kweli mkuu umenena vema mtu anasaidiwa hakumbuki kabisa waliomsaidia inavunja moyo lakini ni vema kuendelea kuwa saidia wale wachache wanaokumbuka kutoa feedback.
 
Tatizo huwezi kupona siku hiyo hiyo hata ukijieleza ipasavyo kwa Dr wa JF ndio maana watu hukimbilia New Post ambazo hujaa recent topic.
Wengi wa wachangiaji sio lazima wawe MaWitch Doctor au MaDr wa kawaida lakini kutokana na uzoefu wao ndio maana watuelekeza tutmie Maji mengi au miti shamba
Bahati nzuri @ng`wana ong`wa kulwa
,
mara zote upomOn line ndio maana unasema hatujielezi na tunaondoka kabla ya kupata ushauri hiyo ni kweli lakini ukirudi baadaye hata mwaka, mwezi au siku lazima utaukuta huo ushauri maana Siasa au Habari za kimataifa ukiziacha huyakuti yakiwa Live ni sawa kusubiri kitu kilichocha
 

Hahaha umenifurahisha Ukwaju kwamba ni sawa na kusubiri kitu kilichochacha kuna kaukweli kidogo lakini ni bora basi mtu akaandika medical history kwa ufasaha ili hata asipokuwepo online watakakuja wakisoma tu wanatoa ushauri kuliko kutoa information nusunusu......

Sijakuelewa unaposema huwezi kupona siku hiyohiyo hata kujieleza kwa jf Doctor, kwa mfano mtu anasema mwanangu kapaliwa na kitu fulani nikimshauri amwinamishe ampigepige mgongoni kwani hawezi pona saa hiyohiyo?
 
inategemea na topic, mfano za udaku zinapata michango mingi.na watu kutokuwa serious na majibu yao.mfano kuna topic iliwekwa ya kijana aliingiliwa tigo,alipata comment nyingi.humu wengi hawako serious unless uweke vitu vinavyowafurahisha wao na wajibu majibu ambayo ya upondaji tu
 

Kisukari umenena kweli.
 
kikubwa ni kama ulivyosema watu wanaanzisha thread kuomba msaada pale anapoulizwa maswali na Dr hajibu anakuwa ameshatelekeza uzi wake,au anarudi baada ya siku kadhaa sasa ni ngumu kumpa msaada mtu usiyeelewa historia ya tatizo lake! Nadhani baadhi ya wataalamu wamekosa mvuto wa kuendelea kuwepo hapa,ila tunaomba warudi Cc: Riwa Mupirocin pia shukrani za pekee kwa Mzizi Mkavu
 
Last edited by a moderator:

Kweli Prishaz akina meningitis na wengine warudi jamani!
 
mimi nipo nawasaidia wengi tu ingawa walio wengi hawarudishi feedback, lakini najipa moyo kwamba mchango wangu unawasaidia. huwa natoa nafasi kama mtu anashida anaweza hata N Pm namsaidia. karibuni sana
 
Wakati mwingine hata baadhi ya washauriwa hawapo serious na shida zao, unakuta mtu anaomba ushauri kwa kujaribu tu ili awaone wachangiaji wanasemaje, hili kwa mtaalamu makini hawezi kuendelea kupoteza muda kwa jokes za baadhi ya watu wakati wapo wenye shida za kweli wanaohitaji msaada! tukiachana na mambo haya ya utani naamini wadau wote watarudi, nimeamua kuungana nanyi baada ya kuvutiwa sana na mawazo komavu ya baadhi ya wachangiaji. Let's be serious.
 
Kuna sababu kadhaa zinazifanya uchangiaji upungue,

1. Umakini wa mada.
2. Kutokujieleza vizuri kwa waleta mada.
3. Kutorudisha majibu/maendeleo ya msaada uliotolewa.
4. Kujirudia rudia kwa tatizo/mada ile ile.

1. Umakini wa mada.
- Hapa mada italetwa ikiwa ya mzaha, kukejeli n.k wakati kuna jukwaa husika (Utani, Udaku, n.k).Hii hufanya jukwaa kupoteza hadhi yake, mvuto kwa sababu, wachangiaji makini wa jukwaa hili hili utawakuta kule Jukwaa la siasa, Intelligence, Great thinkers forums!

2. Kutokujieleza vizuri kwa waleta mada.
Kuna vitu kadhaa ni lazima kuvieleza, inawezekana daktari haviulizi mkiwa pamoja kwani anakuona, lakini katika mazingira ya kutoa ushauri katika jukwaa vitu kama Jinsia, Uzito, Umri, n.k ni muhimu sana hivi husaidia katika dozi ya dawa/kupanua wigo wa ufikiri zaidi wa tatizo n.k.

3. Kutorudisha majibu/maendeleo kwa msaada unaotolewa.
Wakati mwingine, wanajukwaa hutoa msaada hasa pale msaada unapohitajika kwa kuonana mf. Namba za simu za madaktari, watoa huduma za afya, n.k lakini watu hawaleti maendeleo ya walipofikia, hii hufanya watu kukosa moya wa kufanya hivyo mara nyingine.

4. Kujirudia rudia kwa mada ile ile.
Ninatambua magonjwa ni yale yale lakini yaweza kujitokeza kwa namna mbalimbali, lakini wakati fulani mada inayoletwa ni ile ile, yaani mf, Tatizo la Fangasi (Fungi),mada hii italetwa leo, kesho, siku inayofuata n.k Sasa iwapo tungekuwa tunajaribu kusoma mada ya ugonjwa tunaotaka kuuleta jukwaani kabla ya kuandika, angalau hata kwa ku-search, ingesaidia.

Hivyo basi mkuu ng'wana ong'wa kulwa , tukijirekebisha kwa mambo hayo na mengine mengi, jukwaa litarudi katila hadhi yake.
 
Last edited by a moderator:
mimi nipo nawasaidia wengi tu ingawa walio wengi hawarudishi feedback, lakini najipa moyo kwamba mchango wangu unawasaidia. huwa natoa nafasi kama mtu anashida anaweza hata N Pm namsaidia. karibuni sana

Shukuani mkuu kwa msaada wako unaoendelea kutoa kusaidia jamii,uwepo wako ni muhimu sana hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…