kvelia
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 246
- 44
Ndugu zanguni wataalam, nina tatizo la muda mrefu. Nikiwa kijijini kama mwaka na nusu uliopita nilikuwa namwelekeza ng'ombe kwenye zizi lake ghafla akanivuta na mkono ukauma sana. Nilienda hospitali nikapigwa X-RAY doctor akasema hakuna mfupa ulioteguka wala kuvujika, nilipewa dawa za kutumia kama mwezi hivi. Nilipata nafuu lakini baadae kama miezi sita hivi kipindi cha baridi mkono ukauma tena na haufai kabisa kufanya kazi yeyote. Nauliza kuna uwezekano nikapona na niende wapi, NISAIDIENI JAMANI, TATIZO NI NINI. Natanguliza shukrani