Wakuu,
Matokeo haya ni kadiri yanavyoingia NEC; tatizo kubwa ambalo tumekumbana nalo na huenda hamjui ni kuwa:
- Vituo vilivyokuwa kwenye daftari la wapiga kura na vinavyokuja kwenye matokeo ya sasa vinatofautiana sana, inatupa wakati mgumu kuweza kung'amua nini chanzo.
- Vyama vilivyoonekana kuchuana kwa karibu ni CHADEMA na CUF (bara) na ndo maana tukawa na list ya vyama hivi ili kuonyesha mchuano ulivyo.
- Kuna watu wanadai hawaoni tofauti: Bluu ni upande wa urais na nyekundu ni upande wa ubunge.
- Tunapata majimbo kwa awamu, matokeo yaliyoingia NEC mpaka mida hii hayajaonyesha uhalisia wa matokeo kijimbo.
Wale mnaoangalia TVs, ni njia rahisi sana na mbadala ya kuweza kupata hali halisi kwani wao wanasoma yaliyo vituoni promptly.
TUNASIKITIKA kuwa kuna delay kubwa tofauti na matarajio yetu, matokeo yanaweza kuwasilishwa NEC masaa mawili au matatu yajayo kwa wingi hivyo tutarajie lolote.
Kwa mujibu wa observer wetu, race kubwa ni kati ya JK na Slaa