Tanzania hatujaweza kupata Waziri Mkuu mchapakazi kama huyu. Sokoine ndiye aliyeanzisha daladala yaani alipita pale Posta (Opps Posta ya Zamani si hii mpya) na msafara wake akaona watu wengi wanasubiri usafiri, akauliza pana nini hapa? Akaambiwa wananchi wanasubiri UDA kwa usafiri wa kwenda nyumbani.
Basi kesho yake akaagiza mabasi yote ya mashirika ya umma wakati ule yakimaliza kuwaleta/ kuwarudisha wafanyakazi yaendelee kuwachukua wananchi kuwaleta kazini na wenye mabasi binafsi waanze kufanya hivyo kama wanaweza. Ndipo ikazaliwa daladala. Alikuwa anajali Maisha ya wananchi wa Tanzania.
Hata kabla ya kifo chake, ndege iliyotakiwa kumrudisha Dar es Salaam kutoka Dodoma ilichelewa, basi akasema hakuna shida nitakwenda Dar kwa gari, hapo ndipo alipokutana na mauti kule Morogoro (Dumila).
Watu wengi walikuwa wanasema kwamba JK Nyerere alikuwa anamwandaa kuwa Rais akiondoka kwa sababu hiyo ilikuwa ni mara yake ya pili kuchukua cheo hicho baada ya kujiuzulu, ikumbukwe Mawaziri wengi wanyakuaji walikuwa wanamuhara.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake peponi salama.