Kwa vile mkuu Zomba ameomba nafasi ya kwenda masjid tunaenda mapumzikoni, tutarejea wote saa moja na nusu East African time (19:30 EAT).
Tutakapo rudi tutaendelea na swali la saba. Asanteni wote.
Jamani wana JF kuna mambo ni personal zaidi, lakini hili lililonipata naona ni janga, mama yangu mzazi amefail step na alikuwa amefanyiwa oparesheni ya neuron surgeon sasa ametonenesha ile sehemu aliyofanyiwa oparesheni, nimeshinda MOI leo na sikuweza kufanya chochote, Nampenda Mama yangu siwezi kumteleza.
Natumia fursa hii kuwaomba radhi wana JF kwamba wanisamehe kwa kutokupatikana leo, nadhani kwa waelewa wanajuwa vyema uchungu wa Mama. Roulette mimi ndio nimerudi nyumbani sasa hivi wakati waliofunga wanajiandaa kupata daku. tusameheehane ndugu zangu, nina majonzi.
Nimekupata, ila naomba members watakao kua na swali kuhusiana na jibu lako waliwasilishe katika thread ya side comment. Tunaendelea na swali la saba.Nadhani dhanna nzima ya neno "fisadi" inakosa mshiko. Ikumbukwe kuwa ufisadi unaweza kuwa wa aina nyingi sana, ufisadi wa wizi, ufisadi wa ngono, ufisadi wa mali, ufisadi wa kuharibu tu, ufisadi wa kuchukuwa wake za watu.
Ukitazama kwa mantiki hiyo pana utaona mtu anarusha shutuma kuwa fulani ni "fisadi" lakini haainishi ufisadi wake ni nini. Huyo ni kama debe tupu haliishi kutika ni wa kumpuuza tu na hafai kujibiwa.
Ukitazama shutuma nyingine zilizojibiwa, kama ulivyozieleza hapo juu, utanielewa naongea nini, hizo zipo "specific". Lakini "general term" ya ufisadi ujibu ni nini? ufisadi upi?
Nadhani umenielewa.
Asante kwa jibu hilo. Tutasubiri data zaidi kwenye nyuzi ya side comment. Nilipata pia habari ya hotel bora duniani inayo toa safari experience ya kipekee kabisa. Nina swali la ufafanuzi:
Ukichunguza msafara wa Raisi Kikwete utakuta mara nyingi unawatu wengi, je hao watu wote wana umuhimu? Pia kufatana na jibu lako political diplomacy inaonesha matunda mazuri ila kuna umuhimu wa kujiuliza kama safari hizo anahitaji kufanya Raisi Kikwete mwenyewe au leadership nzuri ingependeza angewawezesha mawaziri wake na wahusika wengine, yeye akaishia kutoa vision na muongozo. Sijui unasemaje kuhusu hili wazo ambalo tumeliona likirudi sana katika critics za safari hizi.
Swali la nane:
Hivi karibuni mbunge wa Ubungo Mh. John Mnyika alitamka bungeni kuwa tumefika hapa tulipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete. Unadhani Rais Kikwete ni dhaifu na kwa nini?
Najua swali hili limejibiwa katika side comments, ila ingependeza ujibu tena na utoe ufafanuzi wako binafsi: je ikiwa kweli yeye ndie Rais bora wa Tanzania hadi sasa, unadhani ni kwanini watu wanamlalamikia sana Raisi Kikwete kuliko rais wengine wote kuhusu udhaifu wake na wa serikali zake?
Tuchukue dakika kumi na tano kujibu hili swali, halafu tuendelee na swali la tisa.
Asante kwa jibu lako. Nikikusoma vizuri (karibu kunikosoa) naona unacho kipinga ni neno "dhaifu". Nikitumia hoja za Mh Mnyika nabadili swali na kuuliza: Je unadhani "mapungufu" ya Raisi Kikwete pamoja na serikali yake yanaweza kua ni sababu ya Tanzania kufika hapa tulipo (Assumption yake ilikua hapa tulipo tuna hali isio kua nzuri sana)? Kama sio Raisi Kikwete na serikali zake (kuanzia 2005), nani alaumiwe?