Swali la kumi na tatu:
Swali hili linatoka kwa mkuu
FJM na Mkuu
SnowBall na linahusu kilimo. Niliona kwenye side comments kua umeligusia ila sio vibaya ukifafanua kwa undani:
2. Kilimo kinachangia 25.7% ya GDP. Tanzania's GDP ni USD 23bn. Hivyo 25.7% X 23 = USD 5.29. Sasa, leta figures za watu walio kwenye kilimo, 70-80% ya watanzania (aprox 30m people) wako vijijini na wanajishughulisha na kilimo. Kwa maana hiyo basi, 70-80 ya watazania kupitia shughuli kubwa wanayofanya -kilimo wanachangia only 25.7% ya GDP! Hapa tuna kilimo kwanza? and how much we've spent on this kilimo kwanza? return on investment iko wapi hapa?
Kitu unachoshindwa kuelewa ni kuwa pato la mazao ya kilimo ni mtambuka, hizo figures zako ongeza na zile za viwanda vinavyotumia mali ghafi za kilimo utapata kuelewa zaidi mchango wa Kilimo Kwanza kwenye uchumi wa Mtanzania. Usiwe confined kwenye kipato unachokiona kama "direct" figures za mazao yakiuzwa kama "raw materials" pekee, panuka kidogo.
Mfano mdogo tu; Viwanda vikubwa Tanzania pamoja na vya vyakula (Azzam), Beer, Sigara, na kwa viwanda vidogo kama vile vya kusaga na kukoboa vinachangia kwenye pato la taifa directly kutokana na mazao ya mkulima lakini mchango wake wa pato kitaifa utaukuta kwenye viwanda na biashara na si kwenye kilimo. Upo hapo ulipo?
Nadhani huelewi dhanna nzima ya kuongeza viwanda vya kusindika na kuzalisha bidhaa za kilimo kuwa ni moja katika mikakati ya Kilimo Kwanza, Na zaidi ya viwanda, kuna mapato mengine mengi yanayotokana na kilimo lakini mchango wake hauukuti kwenye kilimo, kama usafirishaji wa mazao (transport) na oboreshwaji wa barabara una direct impact katika kilimo kwanza. Hebu kijana panua mawazo kidogo usiwe confined katika kutafuta makosa tu, mara moja moja jaribu kutafuta na mema. Ukibaki katika kutafuta makosa tu hutaliona jema lolote na yapo mengi sana.
Dhanna nzima ya Kilimo Kwanza si kwenye shamba tu. Fikiri, ulime ukose barabara ya kusafirishia mazao utapata faida kweli? au utalima zaidi ukijuwa hata mazao kuyafikisha kwenye masoko yenye faida huwezi kuyafikia? Ulime ukose maghala? ulime ukose soko? ulime ukose walaji iwe wa viwanda au majumbani?
Halafu ROI ya mfumo mzima wa kilimo haitafutwi kama utakavyo wewe, be realistic. Unaongelea investment kama vile hapo paliwekezwa na serikali ndiyo inayolima? kuwa makini kidogo. Serikali inawekeza kwa mkulima kuweza kulima kwa ufanisi na haitegemei yenyewe iwe na direct profit, yaani iwekeze kwenye pembejeo halafu ioneshe faida? ndio utakavyo hivyo?. Faida inakuwa kwenye kipato cha mkulima, kipato cha transporter, kipato cha mfanya biashara, kipato cha mwenye kiwanda, kipato cha clearing agent, kipato cha dalali wa sokoni, na, na, na directly au indirectly.
Baada ya kupata hili darsa dogo la dhanna ya kilimo kwanza, pitia upya "calculations" zako uzirekebishe.
Funguka kidogo, duh, ikiwa Tanzania tuna watu wenye kutaka mambo na figures ziwe kama utakavyo wewe, tunaelekea kubaya.