Tunaendelea na swali la tisa ambalo litajibiwa pia ndani ya dakika kumi na tano:
- Chagua jibu lililo sahihi. Ninategemea jibu litazingatia ukweli halisi wa maisha ya sasa ya Watanzania bila kujali kama Rais metimiza ahadi ya kuwaletea maisha aliyowaahidi au la! Watanzania wanaishi
Tafadhali, jibu na kutoa maelezo mafupi.
- (a) Maisha bora
- (b) Maisha bomu
- (c) Bora maisha.
Asante kwa jibu lako, na data kamili kuhusu idadi ya watu walio guswa na miradi hiyo. Swali la ufafanuzi:
Imekadiriwa kua leo Tanzania ina wananchi 43,188,000 (source: http://www.nbs.go.tz/pdf/Tanzania_in_Figures2010.pdf). Ikiwahivo tunaweza kua na shaka katika uwezo wa miradi hiyo kuwagusa watanzania wote, hasa tukizingatia muda uliotumika na idadi ya watu walioguswa na miradi hiyo hadi sasa. Ni asilimia ndogo sana ya watanzania walio ona mabadiliko kupitia miradi hiyo.
Unachukuliaje pendekezo za kubadili institutions na system nzima kuliko kuvizia individuals kwa kupitia msaada kwa familia moja mmoja?
Tunajaribu kuokoa muda, nataka kuleta swali la kumi ambalo ndilo swali langu la mwisho kabisa kwa Mkuu zomba. baada ya hapa tunaweza kupumzika kwa leo, na kurejea kesho kwa maswali tano toka kwa member. Hii ni kama mkuu Zomba atapendezwa.
Swali la kumi:
Tunajua kua katiba hairuhusu Rais kugombea uawala mara ya tatu. Ila tuzungumze kidogo kwa lugha ya "je ikitokea", Unafikiri kama Rais kikwete akipewa nafasi ya kugombea tena Urais mwaka 2015 atashinda? Katika kujibu hapa jaribu kukumbuka ahadi zake za 2005 na utekelezaji wa ahadi hizo, kumbuka pia ahadi za 2010 na utekelezaji, zingatia mahitaji ya taifa, halafu jaribu kumlinganisha Rais Kikwete na potential candidates wengine tunao waona hivi sasa, toka chama tawala au upinzani.
Karibu mkuu.
Mwali kutekelezwa na kushughulikiwa ni kitu kinachofanana na kwa muono wangu ni kimoja.Nimesoma na kuelewa jibu lako ila naomba ufafanuzi: Ahadi kutekelezwa ni tofauti na ahadi kushughulikiwa. Nikirejea jibu lako kuhusiana na ahadi 69, zingine bado zipo kwenye feasibility stage. Ndugu FJM (him again) aliuliza budget zilizo tumika katika kutekeleza ahadi hizo.
Nadhani ni wazi kua ahadi nyingi BADO ZINAFANYIWA UTAFITI AU BADO ZINASHUGHULIKIWA. Kwa mwananchi wa kawaida fesibility stage haimaanishi lolote, wanataka ahadi zitekelezwe kabla ya uchaguzi ujao. Kwa wananchi wanaofatilia zaidi wanaweza kuona Mgombea Rais anaweza kuahidi kitu kabla ya kufanya uchunguzi wa feasibility ya mradi sababu ikitokea feasibility ioneshe kua mradi sio "feasible" kuna hatari ya kuonekana muongo.
Kufatana na machache hayo, unaweza kusema kua kweli wananchi wameridhika na Rais Kikwete na kwamba anabaki kua chaguo la kwanza la watanzania?
Sasa tunaanza na maswali toka kwa members.
Swali la kumi na moja (toka kwa Mr Rocky na Ngongo):
Kuhusu sheria na utawala, kwa mara ya kwanza Tanzania tumeona ingezeko la mahakimu, majaji, na kupunguwa kwa kesi kwa kiasi kikubwa sana mahakamani.
Je ongezeko hilo linareflect hali halisi ya mahamaka zetu na mlundikano wa kesi? je hao mahakimu na majaji walioongezeka kuna vitendea kazi kuwawezesha kuhimili hali ya nchi yetu? Maana kuna wilaya ambhazo hazina mahakama za mwanzo au hata majengo kuendeshea kesi mbalimbali. Au inabidi hakimu aendeshee kesi zake kwenye ghala (refer Magu)?
Je budget ya kuendesha shughuli za mahakama inatolewa kwa wakati kukidhi uhalisia na mahitaji ya hizo mahakama? Au ni kuongeza tuu majaji na mahakimu bila kujali kama kuna majengo au vitendea kazi kuendesha hizo kesi?
Huenda ukawa umesha jibu hili swali kwenye side comments. Kama ni hivo basi nitakuomba tu unukuu jibu lako na tuendelee na swali la kumi na mbili. Karibu mkuu zomba
Asante kwa jibu hilo.
Swali letu la kumi na moja linatoka kwa Ngongo na Kibanga Ampiga Mkoloni na linahusu muswada wa NSSF:
Qn;
Ujenzi wa UDOM umekomba fedha za NSSF na kusabisha shirika hilo matatizo makubwa ya cash flow na hatimaye sisi wanachama wa NSSF tunalazimika kulipwa fedha zetu tutakapofikisha miaka 60 haijalishi umefukuzwa kazi ukiwa na miaka 20 au 30 !.
[1] Inafahamika wazi ajira za sekta binafsi hazina usalama mtu unafanyakazi miaka yako sita au kumi unatambaa au unakimbizwa.
[2] Umri wa kuishi mTanzania ni chini ya miaka 50
[3] Maamuzi ya ujenzi wa Udom na Daraja la kigamboni wanachama wa NSSF na PPF hawakushirikishwa.
zomba huoni Kikwete na serekali yake wanastahili kushtakiwa kwa kutuweka sisi wanacha wa hiyo mifuko ya hifadhi ya jamii katika hali ya ngumu kwa nia ya kujipatia ujiko wa kisiasa ?.Katiba mpya kipengele cha kumshitaki Rais anayechezea uhai wa wananchi wake kiwekwe.
Asante kwa jibu hili. Kuna baadhi ya members na hata watanzania mtaani waliohusisha miradi hiyo na muswada. Wanasema hivo kutokana na Serikali ya Tanzania kushindwa kulipa pesa ya wanachama wa NSSF. Mbaya zaidi, inasemekana kua feasibility ya miradi ya serikali ilionesha dalili zote kua haziwezi kulipa ila serikali ilitumia nguvu zake (official and unofficial) kulazimisha miradi hiyo ipate pesa toka NSSF. Kutokana na serikali kushindwa kuilipa NSSF ndio uamuzi huu wa kusogeza miaka ya kupokea hadi 55 imetokea.Dhanna nzima ya mfuko wa NSSF ni kumwekea mtu akiba ya baadae kwa kuchangia yeye asilimia fulani na muajiri wake asilimia fulani.
Si vyema kuanza kusema mfumo ni mbaya bila kuziona kanuni zake. Tunatoa tathmini "premature". Ikumbukwe kuwa kabla ya kubadili hii sheria kuna tathmini imefanyika na kuona ni vipi iboreshwe ili hiyo akiba inufaishe zaidi muhusika. Ngoja tuone kanuni kamili inasemaje, tusikurupuke.
Tusihusishe miradi ya maendeleo na hii kanuni. NSSF kukusanya fedha zote hizo bila kuwa na miradi ya maendeleo na kuziwekeza kwa manufaa ta Watanzania itakuwa ni upuuzi wa hali ya juu, na wala hiyo miradi siyo iliyoamuwa hii sheria irekebishwe.
Nasisitiza tungoje tuione sheria na kanuni za NSSF zinasemaje kabla hatuja kurupuka. Nna uhakika kuna mema mengi ndani yake kuliko mabaya.
Kuna tetesi kuwa katika kanuni mpya zitazoambatana na sheria hii, NSSF itaweza kukudhamini kupata mikopo ya riba nafuu sana na manufaa ya mara kumi zaidi ya akiba yako ili kuendeleza wigo wa kumwezesha mwananchi wa kipato cha chini kwa "collateral" ya akiba yake.
Asante kwa jibu hili. Kuna baadhi ya members na hata watanzania mtaani waliohusisha miradi hiyo na muswada. Wanasema hivo kutokana na Serikali ya Tanzania kushindwa kulipa pesa ya wanachama wa NSSF. Mbaya zaidi, inasemekana kua feasibility ya miradi ya serikali ilionesha dalili zote kua haziwezi kulipa ila serikali ilitumia nguvu zake (official and unofficial) kulazimisha miradi hiyo ipate pesa toka NSSF. Kutokana na serikali kushindwa kuilipa NSSF ndio uamuzi huu wa kusogeza miaka ya kupokea hadi 55 imetokea.
Ila sasa watu wengi wamekua na shaka na uwezo wa wakuu wa NSSF kuchagua miradi gani ikopeshwe na miradi gani ikataliwe. Kwa vile pesa zinazo tumika ni pesa za wanachama, baadhi ya wanachama hao wanapendekeza NSFF iunde utaratibu wa kuwa-consult kabla ya kutumia pesa zao. Unasemaje kuhusu wazo hili la members kuchukuliwa kama shareholders?
Swali la kumi na tatu:
Swali hili linatoka kwa mkuu FJM na Mkuu SnowBall na linahusu kilimo. Niliona kwenye side comments kua umeligusia ila sio vibaya ukifafanua kwa undani:
Ukisoma kwa haraka haraka unaweza kupiga vigelegele. But let's look at the numbers, shall we?
1. Pamoja na cosmetic efforts za kupata number 'nzuri' kilimo kinakuwa kwa 5.1% (FY 2010/11). From 2005 -2010 growth rate kwenye agriculture ilikuwa around 4.4% kwa hiyo kuna increament of just 1.1%! Yote tisa, kumi, ukiangalia figures za MKUKUTA, by 2010 mipango inaonesha kuwa kilimo kilitakiwa kikuwe na kufikia 10%. 2011 tuko 5.1%., kwa hiyo tuko off MKUKUTA target.
.
Swali la kumi na tatu:
Swali hili linatoka kwa mkuu FJM na Mkuu SnowBall na linahusu kilimo. Niliona kwenye side comments kua umeligusia ila sio vibaya ukifafanua kwa undani:
2. Kilimo kinachangia 25.7% ya GDP. Tanzania's GDP ni USD 23bn. Hivyo 25.7% X 23 = USD 5.29. Sasa, leta figures za watu walio kwenye kilimo, 70-80% ya watanzania (aprox 30m people) wako vijijini na wanajishughulisha na kilimo. Kwa maana hiyo basi, 70-80 ya watazania kupitia shughuli kubwa wanayofanya -kilimo wanachangia only 25.7% ya GDP! Hapa tuna kilimo kwanza? and how much we've spent on this kilimo kwanza? return on investment iko wapi hapa?