Kwa kupitia blog mbali mbali wana JF tuliweza kulaani kitendo cha kishenzi cha kushikilia raia wasio na hatia. Shukurani kwa wadau wote, salute kwa Mike na Max, SD, MKJ, Rev, Mtanzania, FM na wengine wengi tulikuwa tukiwasiliana behind the scene.
Hii ilikuwa moja ya article niliyo ikututa kwenye blog moja wapo.
Habari na mwanablog
Jamboforums Chombo Cha Ugaidi Adai IGP Mwema
katika press conference jana IGP mwema alifafanua kisa cha kuwashikilia wana Jamboforum wawili. Akielezea kwa mbwembwe kabisa kwama jamboforum ni chombo cha kigaidi, mkuu huyo wa polisi alionyesha dhahiri kabisa kutofahamu kwakwe maana ya neno forums.
Hata hivyo mkuu huyo hakuzungumzia ni kwa nini hajamsweka lupongo Rostam Aziz, Jitu Patel au David Balali mpaka dakika hii. Hili limeonyesha ni jinsi gani kisiwa cha amani Tanzania kinavyotawaliwa na wababe wachache. Vilevile IGP huyo hakuelezea ni nini hitimisho la kampuni hewa za Kagoda, au Richmond.
Baadhi ya watanzania wengi waliojiwa na blog hiii walishangazwa kuona ya kwamba ni kwanini wezi wa shillingi million 152 kwa siku hawapo kizuizini mpaka leo. Na wanaokamatwa ni wale walio lia kwa miaka miwili mfululizo kuhusu wizi wa Richmond. Jee muheshimiwa IGP hii ndio haki sawa kwa wote? Jee aliyechafuliwa jina ni Rostam Azizi au Jitu Patel au? Na kama ni hao jee ni kwa nini usiwataje hadharani? Jee muheshimiwa IGP unamausiano gani na watu hao walio dai wamechafuliwa majina yao mpaka usiwataje?
Ni ufahamu wangu mdogo ya kwamba huitaji degree ya sheria ya Havard kufahamu ya kuwa muheshimiwa IGP na wenzie wametumia madaraka waliyonayo kusurpress democrasia. Wametumia jeshi na vifaa vyao vya moto kunyanyasa watanzania wachache. Jee kwa mwendo huu tutafika? Kama mtoa maoni anakwenda jela wakati Ditopile anatamba na STJ mtaani jee hiyo ni haki?
Ni wito wa wana Jamboforum kuzungumzia swala hili katika arena ya kimataifa, ni muda muwafaka kuwaumbua mandumilakuwili hawa, mandumilakuwili wajifanyao wao ni wapenda demokrasia kumbe ni madikteta. Ni muda muafaka wa kuwavua vilemba vyao vya ukoka vya kujidai wanaipenda Tanzania, kumbe wanapenda madaraka yao. Haki sawa kwa wote? Hii ni kauli ya muheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Jee haki ipo wapi? Jee ni haki hagi ambayo wengine wamekula zaidi ya million 500 na wapo mitaani, na wengine wameuwa raia kwa kusudia na wapo mtaani, na wengine wamechangia maoni yao kwenye mtandao na wako jela?
Kwa mwendo huu tunatofauti gani na iddi Amini Dada aliyewapa wahindi masaa kadhaa watimuke Uganda? Swala la kuifunga Jamboforum halina tofauti na swala la kumwagia waandishi tindikali. IGP tunaomba ufuatilie maswala yanayo ikwanza nchi kuendelea, na sio maswala yanayotia chachu maendeleo ya nchi.
Tunaomba Mh. Mwema ukamate wezi walioibia walipa kodi mabillioni ya shillingi na sio wachangiaji wa mtandao. Swala hili ni sawa na ukiukaji wa haki za msingi za binadamu, ni sawa na kuendesha gereza la siri la kutesa watu.