JF Hard Talk "Zitto junior"

1. Taifa tunanufaisha kupitia profession zetu maana hta ukiwa mfagia barabara pia una mchango kwenye pato la taifa lakini kwenye suala la maarifa kiduchu nayopata huwa napenda kushare na watu kupitia platform mbalimbali ili tuweze kujikwamua kifikra.

2. Awamu hii naona kidogo wamejitahidi kuwaweka wasomi frontline lakini nmegundua bado wanasiasa wanahodhi maamuzi ya wataalam. Na hii ipo maeneo mengi ukileta technicalities unaonekana kama unapoteza muda hivi wa watu kumbe unajaribu kutumia uweledi kwenye masuala muhimu.

Kwahiyo naweza kusema tunajitahidi kama nchi ila bado hatujafikia level ya kufungua potential walionayo wasomi wetu. Hata humu JF kuna wasomi kibao tu nawafahamu kwenye field mbalimbali ila hata vitabu tu hawajaandika sababu wanajua no one is interested or supporting so mtu anakufa na ujuzi kibao.

USHAURI: Kazi za kitaaluma zitolewe kwenye mfumo wa siasa ili kuepuka wasomi kuhodhiwa na wasaka madaraka. Mfano mawaziri wasiwe politicians bali experts wa masuala husika ili wajitenge na masuala ya vyama na vita za madaraka na hapo ndio tutaona wasomi wakitumika interest za taifa sio vyama.

Pia taasisi nyeti za umma zipewe independence fulani, kama ambavyo CAG haingiliwi basi taasisi nyeti watu wapewe uhuru kwenye kazi zao ili kuepuka kuburuzwa na interest za wanasiasa. Obvious hii itafuta uoga kwenye utendaji maana sahvi mtu anaona kitu hakijakaa sawa ila anaogopa akishauri tofauti atafukuzwa. Imagine Engineer ameweka lift kwenye hospitali lakini mwanasiasa anamwambia ni anasa!!! Kwa staili hii wasomi wetu watatumia ujuzi wao ipasavyo?

Sorry kwa andiko refu
 
Nashukuru sana mkuu kwa majibu murua kabisa. Niseme tu nina maswali mengi kutoka kwenye hili jibu lako, lakini kwasababu nilisema maswali yangu yatakuwa ya mwisho basi naomba niishie hapa.
 
Nashukuru sana mkuu kwa majibu murua kabisa. Niseme tu nina maswali mengi kutoka kwenye hili jibu lako, lakini kwasababu nilisema maswali yangu yatakuwa ya mwisho basi naomba niishie hapa.
Karibu sana mkuu, waweza uliza tu ukipata wasaa JF ndio sehemu ya kufunguka mawazo yetu
 
Mkuu,kwanza hongera,kwa kuwa kupitia kujibu maswali kuna mengi tunajifunza.

Mimi ni moja ya watu ambao huwa naelimika na mada zako kuhusu biblia na nimekuwa nikizifuatilia hasa kupitia Jamii intelligence

Na nikiri kutokana na mada zako na hasa rejea kutoka kwenye bibilia nililazimika kusoma bibilia yote ili niweze kupata uelewa wa kile kinachojadiliwa,na namshukuru Mungu nilifanikiwa kumaliza yote,ila baada ya kumaliza nikajikuta nina maswali mengi ambayo sina majibu yake na yote niliyaandika kwenye shajara.

Labda kuna siku nitaanzisha uzi niyaweke yote,labda kwa leo nikuulize machache ya bibilia na machache kuhusu wewe;

1.Hapo juu umemjibu mdau kwamba unaamini bibilia kwa sababu baadhi ya mambo ya bibilia 'yamejimanifest' kwenye maisha yako
Unaweza kututajia baadhi?

2.Je kwa uelewa wako wa Kibiblia unadhani ni sahihi kumtangaza Mwalimu Nyerere kuwa Mtakatifu?

3.Yesu alimaanisha nini kusema'Sikuja kuleta amani duniani Bali mafarakano?
(Luka 12:51)

NB; Kwakuwa umesema bibilia imeandikwa kwa lugha ya mafumbo unaweza ukanisadia material yatakayonisaidia kuelewa zaidi biblia na hasa ukizingatia nilikuwa muumini wa kusubiri Jumapili kusomewa 'somo la siku' mistari michache hivyo nahitaji kuelewa zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza nikupongeze kwa kusoma Biblia nzima sio jambo dogo na nmefurahi kuona kuna watu mnapokea mada zangu kwa mtazamo chanya.
1. Masuala yaliyo manifest ni mengi mnoo ila kwa machache ni manifestation ya Holy spirit, nguvu ya maombi, ahadi tulizopewa kwenye Biblia ukiishi kwenye imani n.k nimeyaona maishani mwangu so naweza sema Biblia ipo Hai.

2. SI SAHIHI kumpa binadamu utakatifu, especially binadamu wenzie. Anayejua nani ni msafi ni Mungu tu sio binadamu yeyote yule na hyo itajulikana wakati wa Hukumu pekee. Soma Mt 24,25 na Ufunuo 14,20-21.

3. Hiyo ni lugha ya fumbo kumaanisha Yesu alipofika duniani na kufundisha, watu watagawanyika na watakosana na wazazi na familia zao kisa kumfuata yeye rejea Yoh 15:18-25 .

Pia Huu ulikuwa ujumbe kuwa kwa kuleta injili ya kweli basi mataifa na familia zitagawanyika kuwa either ufalme wa giza au ufalme wa nuru na vita hii ipo kila siku na imeongelewa Eph 6:12.

4. Kuhusu material ninazo ila hard copy but sina soft copy kwa sasa. Ila all in all neno lolote la bible ukisoma fikiria na implication yake kiroho sio kimwili tu
 
Mkuu,nashukuru kwa majibu yako mazuri,
Nitaendelea kujifunza zaidi ili nielimike kimwili na nifaidike kiroho.

Lakini nakuomba utakapokuwa na softcopy ya hayo materials nisaidie, naamini yatakuwa msaada mkubwa kwangu (nitakukumbusha).

Tupo pamoja mkuu,tuendelee kuelimishana.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…