zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
1. Taifa tunanufaisha kupitia profession zetu maana hta ukiwa mfagia barabara pia una mchango kwenye pato la taifa lakini kwenye suala la maarifa kiduchu nayopata huwa napenda kushare na watu kupitia platform mbalimbali ili tuweze kujikwamua kifikra.Daah, shukrani sana mkuu, nimeelewa vizuri. Uelewa wako wa hizi siasa ni mpanga, nakupa hongera.
Maswali ya mwisho kabisa. Unatumiaje huu ujuzi wako kulinufaisha taifa ? Pia unahisi Tanzania kama nchi unatumia vizuri wasomi wake wenye uwezo mkubwa kama wewe ?
2. Awamu hii naona kidogo wamejitahidi kuwaweka wasomi frontline lakini nmegundua bado wanasiasa wanahodhi maamuzi ya wataalam. Na hii ipo maeneo mengi ukileta technicalities unaonekana kama unapoteza muda hivi wa watu kumbe unajaribu kutumia uweledi kwenye masuala muhimu.
Kwahiyo naweza kusema tunajitahidi kama nchi ila bado hatujafikia level ya kufungua potential walionayo wasomi wetu. Hata humu JF kuna wasomi kibao tu nawafahamu kwenye field mbalimbali ila hata vitabu tu hawajaandika sababu wanajua no one is interested or supporting so mtu anakufa na ujuzi kibao.
USHAURI: Kazi za kitaaluma zitolewe kwenye mfumo wa siasa ili kuepuka wasomi kuhodhiwa na wasaka madaraka. Mfano mawaziri wasiwe politicians bali experts wa masuala husika ili wajitenge na masuala ya vyama na vita za madaraka na hapo ndio tutaona wasomi wakitumika interest za taifa sio vyama.
Pia taasisi nyeti za umma zipewe independence fulani, kama ambavyo CAG haingiliwi basi taasisi nyeti watu wapewe uhuru kwenye kazi zao ili kuepuka kuburuzwa na interest za wanasiasa. Obvious hii itafuta uoga kwenye utendaji maana sahvi mtu anaona kitu hakijakaa sawa ila anaogopa akishauri tofauti atafukuzwa. Imagine Engineer ameweka lift kwenye hospitali lakini mwanasiasa anamwambia ni anasa!!! Kwa staili hii wasomi wetu watatumia ujuzi wao ipasavyo?
Sorry kwa andiko refu