JF Hard Talk "Zitto junior"

Utashi wetu pia unaitajika katika kuhoji kupata kuelewa na kufahamu zaidi mkuu,kwa mfano unaweza kunambia kipindi cha miaka 18 ambacho hakuna injili yeyote inayozungumzia alipokuepo yesu toka akiwa na miaka 12-30 as tunavoamini Mungu alimtuma mwanawe kwa mfano wa binadam je kipindi hicho chote alikuwa wapi makuzi ake as kijana rijali n.k biblia inatuonesha alipoanza mahubiri pale baada ya kubatizwa na yohana mbatizaji,ningependa unisaidie angle iyo!!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oooohhhh!!!!!
Yalio andikwa kwenye bible kuhusu Yesu alicho fundisha binadamu imekua ngumu sana kufata.

Sasa hayo ambayo hayajaandikwa kwenye biblia wew wayataka nn????

Ulitaka bible iwe kubwa kama....... Niseme kama sanduku????????????

Yesu kristo alikubalika na kundi kubwa la watu, kumbuka pia kuna kundi kubwa la wapinga kristo ambao wali mpinga na walimsurubisha.

Kuwa makini utadondokea kwenye vitabu vya wapinga kristo,
Mwl. Mwakasege alikua kishindwa kuelewa mahali fulani katika maandiko, Mungu pekee alimpa ufafanuzi kupitia hicho hicho kitabu kitakatifu kiitwacho Biblia.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naamini kwa kusema ulitaka biblia iandike kila kitu iwe kama sanduku...so unaniaminisha kuwa kuna baadhi waliyandika na mengine hayakuandikwa ili biblia isiwe sanduku...vixuri so unafikiri kwa nini baadhi wameviweka na vingine hawayaviweka na ni kwa matakwa ya nani yaliwekwa na kwa matakwa ya nani hayakuandikwa ili isiwe kama sanduku...?kuhoji kwangu uku si kupinga nataka nijiridhishe kwa uelewa wa kawaida tu mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiwe na shaka kabisa mkuu, kwani tunaeleza wote tu.

Kwanza Yesu sie aliyeshika kalamu akaanza kuandika, Kua nilifanya hichi nikafanya hichi na hichi na kufundisha haya na haya,

Labda uwenda hadi kuna mahali alikua akiulizwa vip wew unapenda kucheza mchezo gani???
Vip huitaji mke wa kuowa???
Vip Yesu mvinyo ni pombe je leo twende tukanywe pombe ya ndizi au bia kama zilikuwepo.
Pia tambua kuwa yawezekana alifundisha kitu furani huku na tena akaenda kukirudia kule..
So aliyofanya ni mengi,

Lakini Biblia iliandikwa na hao manabii wakiongozwa na Roho mtakatifu.
Chakula hicho cha kiroho kilichoandikwa katika biblia ndicho chakula ambacho Mungu kataka sisi tujifunze.

Nakumbuka wakati nasoma Kipaimara tulikua tukiandika vitabu vya biblia na manabii walio viandika, kuna manabii waliandika vitabu vitano wengine kimoja e.c.t
Ndio bible kukamilika.

Pia ukisoma sana Bible utajua kuna mambo ni magumu kweli kweli huwezi kuyaelewa hadi, ujifunze kwanza yale utakayo yaweza
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naliwapa maziwa kwakuwa chakula kigumu mlikua bado hamjakiweza.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mambo ya kidunia, naomba msiwe focused sana na vitabu hivo vya kidunia,

Mkavitumia kuipinga bible au kuikosoa bible,

Mkamsahau Mungu kwa kupunguza kusoma kitabu chake kitakatifu Bible.
Wewe ni moja ya watu hatare inapokuja kutafuta/kuchambua historical events!.. NAKUKUBALI SANA
Kuhusu technology na Novel well kuna app inaitwa WATTPAD humo ndani kuna story za kila aina. itumie if bado upo interest

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Asante kwa majibu mazuri tuendelee kujifunza zaidi huenda tukajapata majibu kamili
 
Naomba kujua chanzo cha mpasuko katika kanisa katoliki na kuzaliwa kwa madhehebu mbali mbali ya protestant.
 
Ni mambo ya kidunia, naomba msiwe focused sana na vitabu hivo vya kidunia,

Mkavitumia kuipinga bible au kuikosoa bible,

Mkamsahau Mungu kwa kupunguza kusoma kitabu chake kitakatifu Bible.


Sent using Jamii Forums mobile app
WATTPAD ni jumuiya ya waandishi wasioweza kupata nafasi kuchapisha vitabu vyao!.
BIBLIA ni jumuisho la maandishi ya kale ya waandishi waliyoonekana kuandika mambo muhimu yaliyowekwa pamoja. Yale yaliyoonekana sio muhimu hayakuwekwa.

Biblia nimeisoma yote, ninaijua yote kichwani only siwezi kukwambia kwa kutumia mistari na aya kama mnavyofanya!.
Im a moderate individual i seek knowledge kila sehemu, nitaikosoa nitakapoona contradictions!.
Moja ya contradiction ya biblia ni kuwa iliandikwa na wanasiasa wakitumia mwamvuli wa dini ili kuweza control wananchi wao na ndio maana yale yaliyoonekana sio muhimu ama hatarishi hayakuwekwa.
Mfano mdogo tu: Miaka ya mwanzoni kumiliki/kukutwa na biblia ilikuwa unachomwa moto wewe na familia au jamaa mtakaokutwa nayo!, aliyetakiwa kumiliki na kuisoma ni kasisi/padre tu!.
 
Kuongezeka kwa wimbi la wachambuzi na uhakiki wa biblia kati ya mstari kwa mstari kitu ambacho kinaibua mambo ambayo yalikuwa hayafahamiki au yalikuwa yanafahamika tofauti na vile tulivyokuwa tunafahamu. Je kunaimarisha imani za wakristo au kunavunja uaminifu wa biblia kwa waumini wake. Nini mtazamo wako katika hiki mkuu zitto junior

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu shukrani kwa ushauri wako wa kujenga ila tuwekane sawa vitu vichache

1. Kwanza sina imani haba juu ya Bible bali mimi ni mtu nayependa kuhoji sana ili nijifunze zaidi na ndio maana mwaka huu nimechukua initiative ya kuingia darasa la theolojia ili nikahoji vizuri na so far nimepata majibu ya maswali yangu mengi sana humu JF hivyo sipingi Biblia bali nahoji interpretation za baadhi ya mafundisho juu ya Biblia mfano

Mnara wa babeli kutaka kufika mawinguni kwa jinsi unavyoelezwa haupo realistic kuwa Mungu yupo mawinguni ilihali leo rocket zinapita na hatuoni Mungu akiziangamiza. Sasa nahoji vitu kama hivi ili kuelewa je interpretation ni sawa au si sawa ndio hapo inatakiwa usome sources zingine mfano historia za sumeria nakutana na Pyramid za Eridu na Akkad ambazo ni ndogo tu kama size ya ghorofa 10 ndipo najenga picha kwamba hili suala lilikuwa na meaning ya kiroho zaidi kuliko kimwili then nafungua nyuzi humu kupata maoni ya watu. Sasa hapo inakuwa napinga biblia au napinga interpretation ya vifungu vya biblia tunavyolishwa???

2. Kutoa maana nje ya Bible nafikiri ni sababu Bible haikuandika kila kitu hivyo kuacha gap ambazo ni lazima tuchambue kwingine ili tuongeze maarifa juu ya suala husika.

Mfano nyuzi ya Mfalme Ogu nilitoa reference ndani na nje ya Bible kwa kuquote mistari kadhaa kuwa alipona gharika ila watu wakasema natumia hadithi za nje.... Nikawauliza tu sasa wanefili waliponaje ndani ya Biblia?? Hawakujibu mpaka leo.... Sasa kama hawajui waliponaje kwanini mnakataza watu wasitumie reference za nje ambazo hata Biblia inazitambia i.e. book of jasher,book of enoch etc.

Nimeweka uzi humu JF biblia yenyewe ikitutuma tufanye reference kwa vitabu vya nje zaidi ya 20 na nilivitaja sasa why tukifanya hivo mnatuona watu wabaya?? Nadhani ni muhimu kufanya reference lwa ajili ya kuwekana sawa kimaarifa na kuongeza uelewa wa topic husika.

3. Mkuu suala la kuamini au kutoamini ni mapenzi binafsi maana hapa unasema Bible pekee ni takatifu na inajitosheleza ila naamini nikikuuliza je ni Bible ipi unayosema inatosha nahisi itakuwa shida kujibu maana bible za kikristo zipo kuanzia ya vitabu 39 mpaka 84 na wote hao wanasema Biblia yao iko sahihi!! Sasa basi kama wenye Biblia wenyewe wanatofautiana vitabu yaani unavyoviona ww haramu kwao ni vitakatifu je sisi watu baki kwanini tusivisome kuongeza maarifa??

Mfano ww utasema Book of Enoch kipo nje ya Bible ilihali Orthodox wanakitumia kwenye Bible yao takatifu kabisa.... Sasa ikitokea nakuhoji hapa je nani kakupa mamlaka ww kukikashifu hicho kitabu ilihali kinatumika miaka na miaka makanisani?? Je huoni orthodox ambao wanaokisoma makanisani wapo zaidi ya million 100 nao watakuona kama UMEPOTOKA??

Issue ya vitabu gani ni sahihi au lah yalikuwa mawazo ya binadamu tu na ndio maana mpaka leo wanakinzana kupata muafaka.... Hata leo wakiamua kuongeza au kupunguza bado utasupport tu ila ukiamua kuwa free thinker na kuhoji hutoona shida kusoma na hivo vingine hta kma ni kwa knowledge tu

Ni hayo tu
 
Alafu naomba uniambie,
Na hisi na mimi naweza nikawa niko tofauti hapo kidogo,

Kwamba kitabu cha mwanzo kimefundisha mambo gani???
Naomba unieleze kidogo naweza pata kitu kipya hapo ambacho sikua nikifahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kitabu cha mwanzo sura ya 1 kinatoa summary ya Biblia nzima yaani tokea uhusiano wa Mungu na mwanadamu ulipoanza kwa Adam hadi kurudi kwa pili kwa Yesu.... Ni topic ndefu kidogo itahitaji white board na marker pen na nikusomee mistari zaidi ya 100 ila all in all haiongelei kabisa kuumbwa kwa dunia ya kimwili wala mwanadamu bali ni uumbaji wa Kiroho sema imeandikwa kwa mafumbo na ndio maana Yesu alisema siri za ufalme wa mbinguni ZIMEFICHWA kwenye parables/mafumbo.... Hivyo mtu usipoelewa MAFUMBO ndio tunaishia kupotoka.
Hivyo nikufundishe kitu leo kabla hujasoma story yoyote ya Bible kuelewa tafuta maana ya neno by neno kwenye Bible mfano usiku na mchana,bahari,mwanga,moto,matunda u can even google alafu ukishaelewa zina maama gani ndio utaelewa hata genesis 1 inaongelea nini hivi hivi utamisinterpret.

Mfano Genesis 1 inaposema mti wa matunda hiyo figurative mti na figurative tunda vimeandikwa maana yake kwenye Bible kitabu cha Ezekiel sasa nani anaweza jua hilo?? Ndio maana watu tunalishwa matango pori kuwa Adam alikua mwanadamu wa kwanza sijui tunda lilikuwa APPLE!! na ukihoji unaonekana mpinga kristo..... Namshkuru sana Mungu kuanza darasa la theolojia nmegundua upotoshaji mkubwa sana makanisani.

Kama uko Dar unaweza arrange muda wako nikuletee notes zangu za hardcopy ujisomee mwenyewe naamini utaelewa nachosema maana kina maandiko ya kutosha kiasi kumaliza kiu ya maswali yako.....

Bible is 90% figurative
 
Kwa kiasi kinavunja imani ila hii ni sababu ya watu kusoma maandiko ya Biblia kama gazeti ila kwa wanaosoma bible kama CODES hawatetereka kiimani bali wataona kama ni compliment tu. Mfano Bible inaposema dunia huwa sometimes haimaanishi ni ulimwengu mzima bali inamaanisha watu wa Mungu tu (na mistari ipo) sasa unakuta Bible ikisema ''dunia nzima ikazama kwenye maji'' kuna watu wana interpret labda gharika lilimeza DUNIA hii nzima sasa watu kama hao ndio wakichambuliwa Biblia na kuletewa hoja kama ile niliyoleta kuhusu mfalme Ogu kupona gharika wanatetereka imani ila wale ambao wanajua lugha ya CODES za biblia hawakushtuka wala nini.

Hivyo kikubwa watu wajifunze lugha ya kimafumbo tu hawatotetereka kiimani
 
Nilitaka japo ueleza kamoja tu,
Mfano aliposema
"Naiwe nuru ikawa nuru..."

Au aliposema

"Na tunamfanye mtu kwa mfano wetu..."

nifafanulie maan ya tukio moja tu ambalo watu wengi wanashindwa kulielewa ka kulicopy vibaya.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Okay nitarudi mkuu na nondo kibao bado nafanya shughuli za kujenga taifa hapa.

Pamoja sana
 
Ngoja nikwambie kitu kimoja, wew unasoma bible kwa malengo yapi???

Do anything for reason.

Hizo history zingine mnazotafuta ukamilifu nje ya bible hata sion maana yake.

Mfano kuhusu mnala wa baberi
Unashangaa why Mungu aliwakatisha waliotaka kufanya hilo jambo,
lakini unasahau kuwa dhumuni la kujengwa kwa mnala huo ni walitaka wamfikie MUNGU
sasa loketi za sasa unafikili malengo yake ni kufika mbinguni?????
au wao wanadili na anga tu.

Alafu hata kama itokee watu wajarbu tena swala hilo, wew unampangia MUNGU la kufanya juu ya watu hao?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaaani mule mule umepita nimefany kufuta comment angu maana umemaliza kila kitu kwangu ilikua repetition tu....mi nachoona kila kitabu ni sahihi kwa matumizi ya imani husika,90%ya imani zetu xpecial tz ni urithi/adopted kutoka kwa wazazi/walezi fanya tafiti au mtu aseme asili ya imani ake leo hii kapata wapi utasikia toka mdogo baba/mama/mjomba n.k ndo nimefuata/amekuzwa nayo so usahihi wa kitu unachangiwa zaidi na imani ako uliokuzwa nayo....na sis wengine ambao kwa mfano mimi ni pure cristian kwa baba na mama Lutheran nimekuzwa uko kuanzia sunday school mpaka kipaimara na nilikua muumin hasa wa kuchimba mafundisho niliefunzwa,baadae advance nkasoma kiundani zaidi katika history ya ukoloni na mbinu mojawapo kueneza ilikua kupitia dini sana sana wa missionary ila b4 tulikua na maisha na maitaji yao ya kila siku walipata kwa imani yao ya mizimu....ndo apo nilipoanza kuzama zaidi kujua kipi dhamira kuu hasa,imani gani sahihi....so tunapohoji vile msivotaka kuvisema sio ni wapinga dini but tunaitaje kuelewa beyond the doubts....


Wengi wetu tujiulize leo hii wazazi/walezi wetu since childish wangekua dini tofauti na uliorithi leo ungekua wapi?na bado ulionaya saiv ungesema si sahihi...na wangapi kati yetu baada ya kuwa na ufahamu na uelewa wao wameacha imani walizokuzwa nao na kwenda imani nyingine kwa akili zao timamu??
Sent from my GT-I9082 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…