JF Hard Talk "Zitto junior"

JF Hard Talk "Zitto junior"

Wakati natafuta ID gani ya kutumia humu JF kipindi hicho zitto alikuwa anatrend sana hasa kesi yake na CHADEMA hivyo likanijia wazo kwanini nsiite tu zitto junior.... Kiufupi nilikuwa namkubali sana zitto na kiukweli ndio mtu aliyenifanya kuanza kufuatilia siasa tokea 2006

nakumbuka hata laptop yangu ya kwanza kumiliki enzi hizo wallpaper nilimuweka zitto na nilikuwa na folder zima limejaa maandiko na video zake akiwa jukwaani,makongamano na bungeni lenye uzito wa takriban GB 20!! dah mahaba bhana!!

Anyway that was back then nikiwaga undergraduate...
Nikisema unamkubali sana sababu ni wa Kigoma mwenzako nitakua nimekosea???
Lol, (usijibu, i was kidding)

Be crazy, Be Weird, Be whatever coz life is too short to be anything but HAPPY.
 
Well, Kaka Zitto Junior ni masuala/mambo gani ya kufuata kama taifa kuwa na uchumi imara na endelevu?
Ni mengi kidogo mkuu ila kikubwa ni kuboost production function yetu kwa kuongeza uzalishaji kwenye kila sekta iwe service,manufacturing,tertiary etc ili tuweze kuuza bidhaa mbalimbali nje na kuongeza pato la taifa.

Pia kuwajengea uwezo wafanya biashara wadogo wadogo ili hata kukitokea uwekezaji mkubwa kma SGR,Bomba la mafuta n.k basi spillover effect iwanufaishe na wao sio uwekezaji wote unaishia kufaidisha makampuni ya nje kisa tu tunakosa internal capacity imagine hadi misumari kwa ajili ya SGR inatolewa nje!!

Pia vipaumbele viwekwe kwenye sekta ambazo zinaweza unganisha nguvu za watu wengi mfano kama kilimo tuna personnel wa kutosha tuwekeze huko hasa kilimo cha kisasa ili tuweze kuzalisha na kuuza zaidi nje.

Mfumo wa elimu pia wa muhimu sana uangaliwe ili uweze kutengeneza wasomi wenye kuweza kutatua changamoto za karne hii yaani wawe practical zaidi kuliko ''makaratasi'' tu inakuwa haina tija.

Pia sera mbalimbali kma za uwekezaji zifungamanishwe na sera zingine zote ili nguvu iwe kubwa mfano Rais amekuja na sera ya viwanda ila sioni wapi imefunganishwa kwenye sera zingine ili tuweze kuwa na shabaha moja.... Ilitakiwa kwa mfano tuone sera ya elimu inaweka mkazo kuhusu masomo ya ujasiriamali na ''shamba darasa'' ili tuone sera ya viwanda inakuwa haswa shabaa ya taifa sio iachwe kuelea elea tu.

Yapo mengi tu mkuu ila kwa uchache ni kama hivi
 
Mimi nikimkubali mtu kwa roho tu bila kumfahamu kiundani hiyo mtu anaouwezo mkubwa sana.

Nakili wewe ni mmoja kati ya hao wachache, asante kaka 🙇
 
Je nin mkombozi wa uchumi wa tz?

Sent using Jamii Forums mobile app
Watanzania kuchapa kazi na kujituma kila mtu kwa nafasi yake hakuna shortcut ndio tutafika.... Kwa upande wa serikali kuweka vipaumbele kwenye maeneo tunayoyaweza machache tu alafu nguvu iwekwe huko kama ni utalii,kilimo,uvuvi basi iwe ndio wimbo kuanzia mitaala kufundishwa kuhusiana na masuala hayo kwa undani zaidi ili kujengea uwezo wa nchi kuweza kujikita kwenye masuala muhimu yanayoweza kututoa hapa kuliko sasa ambapo tunataka tufanye mambo makubwa mengi kwa wakati mmoja bila kujua tunachotaka kulenga.
 
Njia ya kupata mtaji wa kufanya hilo jambo unayo tayar au unaijua?

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeah mtaji kuna source ipo tayari kufund ila sijautoa mfukoni mwangu.... Ila changamoto kwa vijana wenzangu wengi huwa ipo kwenye kupata mitaji bado access ya mikopo ni ngumu sana maana masharti mengi huku vijana hata mali za kuweka rehani hawana nadhani ifike mahala tatizo hili liangaliwe maana kuna kipindi serikali ya awamu iliopita ilitenga mabilion kusaidia wamama na vijana ila haikusimamiwa vzuri pesa hazikufikia lengo maana urasimu ulikuwa mkubwa na hivyo wengi hawakupata.

Suluhisho vijana wakimaliza chuo kuwe na option pia ya kujiunda vikundi wanakuja na proposals zao alafu wanapewa mikopo wakafanyie shughuli za kiuchumi then vyeti vyao vitumike kama BOND.... Kama serikali imewapa mkopo wa shule basi haiwezi shindwa wapa wa kufungua biashara.
 
Je unaihusudu teknolojia (😁) ?
Sana tu imenisaidia mengi nakumbuka hata kuna software tulipewa hatukufundishwa kikamilifu nilichofanya nilikesha usiku kucha naangalia tutorial youtube kuamka asbuhi nikawa master kabisa..... Tokea hapo huwa naihusudu sana teknolojia

Ubaya wake ikitumika vibaya inaweza leta madhara makubwa mfano kupoteza muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii,kutengeneza jamii ya watu wavivu kusoma vitabu maana akitaka jibu ana google tuu tofauti na zamani kwamba ni lazima upekue kitabu ndio upate nondo.

Zamani kabla ya teknolojia nikiwa mdogo nilikuwa nasoma sana novel ila nikiri tu baada ya teknolojia kuja ile spidi ilipungua sana nikawa mtu wa ma-game na kwenye kusoma nikaishia kudownload articles tu au summary ya vitabu ambavyo huko nyuma ilikuwa ni lazima nisome page zote!!
 
Pia Zito jr naomba ukipata muda unipe jibu la swali hili pia...

"Ni mambo gani wew hupenda kufanya in relation na ndugu, mpenz au rafiki kwa manufaa ya mtu huyo au na kwako pia??"

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni mengi tu ila kikubwa mimi ni mtu nayejali sana feelings za watu hivyo huwa nawapa sana priority wenzangu hadi muda mwingine najisahau..... Nakumbuka kuna kipindi nikiwa chuo niliwahi kuandikia assignment ya rafiki zangu wawili na kusubmit hata kabla yangu sijaanza..... Such sacrifices huwa ndio napenda kuoffer kwa rafiki na ndugu

Kwa wanawake ni special kidogo zamani nlikuwa najitoa sana ila wengi walitake advantage sana so siku hizi nimekuwa "mgumu" kwao ili kuepuka kuburuzwa.
 
Umeninspire saana na topic zako apa nasoma kitabu cha hanoko au enock pia umenifanya niwaze baadae kuanzisha church/iman ya free mind church ambalo litakua na mrengo wa kufanya critical reasoning ya mandiko na uelewa wa wasomaji kwa hoja mpaka sasa najaribu jinsi ya kuliintroduce kwa jamii tena kama wewe ndo iwe kiongozi wa iyo imani mpya coz I can see how deep any reasonable you are mkuu zitto jr uwa sichoki kisoma makala zako coz ipo indetails saana big up and may almighty jah bless u so much on ur mvt bro
Sana tu imenisaidia mengi nakumbuka hata kuna software tulipewa hatukufundishwa kikamilifu nilichofanya nilikesha usiku kucha naangalia tutorial youtube kuamka asbuhi nikawa master kabisa..... Tokea hapo huwa naihusudu sana teknolojia

Ubaya wake ikitumika vibaya inaweza leta madhara makubwa mfano kupoteza muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii,kutengeneza jamii ya watu wavivu kusoma vitabu maana akitaka jibu ana google tuu tofauti na zamani kwamba ni lazima upekue kitabu ndio upate nondo.

Zamani kabla ya teknolojia nikiwa mdogo nilikuwa nasoma sana novel ila nikiri tu baada ya teknolojia kuja ile spidi ilipungua sana nikawa mtu wa ma-game na kwenye kusoma nikaishia kudownload articles tu au summary ya vitabu ambavyo huko nyuma ilikuwa ni lazima nisome page zote!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sana tu imenisaidia mengi nakumbuka hata kuna software tulipewa hatukufundishwa kikamilifu nilichofanya nilikesha usiku kucha naangalia tutorial youtube kuamka asbuhi nikawa master kabisa..... Tokea hapo huwa naihusudu sana teknolojia

Ubaya wake ikitumika vibaya inaweza leta madhara makubwa mfano kupoteza muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii,kutengeneza jamii ya watu wavivu kusoma vitabu maana akitaka jibu ana google tuu tofauti na zamani kwamba ni lazima upekue kitabu ndio upate nondo.

Zamani kabla ya teknolojia nikiwa mdogo nilikuwa nasoma sana novel ila nikiri tu baada ya teknolojia kuja ile spidi ilipungua sana nikawa mtu wa ma-game na kwenye kusoma nikaishia kudownload articles tu au summary ya vitabu ambavyo huko nyuma ilikuwa ni lazima nisome page zote!!
Nikweli kaka, maswali yangu nakupelekea katika uwelekeo wa Uchumi na Biashara.

- Tanzania hii ya leo tunahitaji uwekezaji mkubwa katika technology haswa kwenye Economic, Business na Finance lakini viongozi wa serikali hawalioni hilo na hakuna support yoyote kwenye Startups, ni mbinu gani wewe unaweza kutumia kufanikisha hili?
 
Yaani bro ntafanya juu chini tufahamiane hope utaniogopa kama mtu nisiojulikana na wewe una wasiwasi wa kukumbana na kadhia iyo coz c mtu wa siasa siasa za kuogopana nowdays...hahaha...kuna vitu unavielezea as ni tabia zako naona zinafanana na mimi so ningependa uwe my tutor ili niwe positive n productive bro
Ni mengi tu ila kikubwa mimi ni mtu nayejali sana feelings za watu hivyo huwa nawapa sana priority wenzangu hadi muda mwingine najisahau..... Nakumbuka kuna kipindi nikiwa chuo niliwahi kuandikia assignment ya rafiki zangu wawili na kusubmit hata kabla yangu sijaanza..... Such sacrifices huwa ndio napenda kuoffer kwa rafiki na ndugu

Kwa wanawake ni special kidogo zamani nlikuwa najitoa sana ila wengi walitake advantage sana so siku hizi nimekuwa "mgumu" kwao ili kuepuka kuburuzwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Noma sana, very impressive.

Dan Brown kwenye Da Vinci Code anazungumzia issue ya Holy Grail, na kwamba Mary Magdalene alikuwa mke wa Yesu, na kwamba ndiye aliyeachiwa kanisa badala ya St Peter.

And then Bart D Ehrman kwenye Truth and Fiction in the Da Vinci Code anapangua points za Dan Brown kwa kusema kwamba Holy Grail ni fictitious issue na vitu vingine vingi anavikataa.

Kama mdau wa history juu ya hayo mambo, umewahi kukutana na hizo issues most likely, nini msimamo wako kuhusu kwamba Yesu na Mary Magdalene walikuwa mtu na mke wake?
Mkuu hii topic ni controversial sana nakumbuka hata Pastor credible kabisa Marehemu Myles Munroe aliwahi tamka hiki kitu kuwa Yesu alimuoa mary Magdalene na hata kuna apocrypha moja nmeisoma ya Gospel of mary Magdalene inajaribu pia kupotray ukaribu mkubwa uliokuwepo kati ya Mary na Yesu ingawa kitabu hiko hakikutambuliwa na bible.

Kwa mtazamo wangu lolote linawezekana maana licha ya kwamba Bible inamzungumzia Yesu ila inagusia kipande kidogo sana cha maisha yake mfano hatuambiwi umri wa balehe wa Yesu ulikuaje,hatuambiwi aliishi wapi akiwa umri wa miaka 20, Ngazi ya Elimu,Ndoa n.k hivyo naamini lolote linaweza kuwa sawa sababu mimi ni mmoja ya watu wanaoamini kuwa Biblia haikuandika kila kitu na ndio maana huwa nasoma apocrypha na pseudepigrapha ambazo huongelewa biblia characters mmoja mmoja kwa undani zaidi

Mfano ukisoma Gospel of Judas iskariot utagundua jinsi biblia inavyomtaja na jinsi yeye alivyokuwa hadi kufikia pale alipofika ni vitu viwili tofauti..... Sisemi Biblia imepotosha la hasha bali haikuongelea kila kitu na hapo ndipo umuhimu wa apocrypha unapokuja ili kujazilizia hizo nafasi.
 
Umeninspire saana na topic zako apa nasoma kitabu cha hanoko au enock pia umenifanya niwaze baadae kuanzisha church/iman ya free mind church ambalo litakua na mrengo wa kufanya critical reasoning ya mandiko na uelewa wa wasomaji kwa hoja mpaka sasa najaribu jinsi ya kuliintroduce kwa jamii tena kama wewe ndo iwe kiongozi wa iyo imani mpya coz I can see how deep any reasonable you are mkuu zitto jr uwa sichoki kisoma makala zako coz ipo indetails saana big up and may almighty jah bless u so much on ur mvt bro

Sent using Jamii Forums mobile app
Nafurahi kusikia kuna watu huwa mnasoma mada zangu na kuzielewa..... Ingawa changamoto kubwa watu wengi sana wama utumwa wa akili Yaani wamejifunga minyorork ya imani kiasi kwamba ukiwaleza concept mpya wanakuona kama shetani.

Kuna mtu nilimuuliza je Adam mtu wa kwanza akasema ndioa.... Nikamuuliza mbona kuna mafuvu yenye miaka zaidi ya elfu 10,000 yeye akadai wanasayansi wanapotosha

Nilipomuuliza mbona mapharaoh waliotajwa kwenye Biblia wakipigiwa hesabu na wanaachiolojia wanagundua wana miaka sawa sawa na kipindi ambacho walitajwa kwenye Bible!! Hivyo nikahoji iweje akipimwa pharaoh mnaona iko sawa ila akipimwa fuvu jingine ambalo lina miaka mingi zaidi muda aliozaliwa Adam mnakataa majibu yake!!??? Akaishia kuniita mpinga kristo!!

Kikubwa hapa nikutie moyo uendelee kujifunza na kuelemisha wengine ili waweze kujinasua kutoka makucha fulani ya kufungwa ufahamu na kuiona Biblia katika mwangaza tofauti kidogo...... Yaani kuichambua zaidi ili kupata maana halisi iliyokusudiwa sio misinterpretation za watu wachache ili kuficha baadhi ya facts zilizopo humo

Big up for that
 
Mkuu hii topic ni controversial sana nakumbuka hata Pastor credible kabisa Marehemu Myles Munroe aliwahi tamka hiki kitu kuwa Yesu alimuoa mary Magdalene na hata kuna apocrypha moja nmeisoma ya Gospel of mary Magdalene inajaribu pia kupotray ukaribu mkubwa uliokuwepo kati ya Mary na Yesu ingawa kitabu hiko hakikutambuliwa na bible.

Kwa mtazamo wangu lolote linawezekana maana licha ya kwamba Bible inamzungumzia Yesu ila inagusia kipande kidogo sana cha maisha yake mfano hatuambiwi umri wa balehe wa Yesu ulikuaje,hatuambiwi aliishi wapi akiwa umri wa miaka 20, Ngazi ya Elimu,Ndoa n.k hivyo naamini lolote linaweza kuwa sawa sababu mimi ni mmoja ya watu wanaoamini kuwa Biblia haikuandika kila kitu na ndio maana huwa nasoma apocrypha na pseudepigrapha ambazo huongelewa biblia characters mmoja mmoja kwa undani zaidi

Mfano ukisoma Gospel of Judas iskariot utagundua jinsi biblia inavyomtaja na jinsi yeye alivyokuwa hadi kufikia pale alipofika ni vitu viwili tofauti..... Sisemi Biblia imepotosha la hasha bali haikuongelea kila kitu na hapo ndipo umuhimu wa apocrypha unapokuja ili kujazilizia hizo nafasi.

Shukrani mkuu, kama nitapata swali lolote nitauliza mkuu. Ngoja niwe msomaji wa maswali na majibu.
 
Zamani kabla ya teknolojia nikiwa mdogo nilikuwa nasoma sana novel ila nikiri tu baada ya teknolojia kuja ile spidi ilipungua sana nikawa mtu wa ma-game na kwenye kusoma nikaishia kudownload articles tu au summary ya vitabu ambavyo huko nyuma ilikuwa ni lazima nisome page zote!!
Wewe ni moja ya watu hatare inapokuja kutafuta/kuchambua historical events!.. NAKUKUBALI SANA
Kuhusu technology na Novel well kuna app inaitwa WATTPAD humo ndani kuna story za kila aina. itumie if bado upo interest
 
Ngoja nifanye hima yakuelekea play store hiyo aap nadhani itakuwa ni rafiki na kwangu pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nini humkubaligi Paul Kagame?
Namkubaligi sana tu mbona kuna nyuzi mfano ile ya kigali vision 2040 nilimsifia sana kama kiongozi wa kuigwa kwa uchapakazi na hata nyuzi nyingine nlitambua Rwanda kama powerhouse kivita na kiintelijensia hasa kwa mafanikio yake katika Congo wars ya 1 na 2 hivyo namuelewa sana kagame.

Shida yangu na kagame ni hasa kuhusiana na issue ya genocide... Yaani wanapokuja na hoja kwamba sijui wahutu ndio walichinja watutsi peke yao sioni kama ni haki maana pia watutsi walikuwa na jeshi/vikundi vya mauaji so wote tu waliuana. Actually wahutu walikufa zaidi ila hii kitu kagame hajawahi kubali kabisa zaidi ya kusema Tutsi genocide ndio iliotokea na ukihoji unapotezwa.

Suala jingine ni wafuasi wa kagame kuamini hawezi tokea kiongozi mwingine kama yeye hadi kuamua kujiongezea muhula.... bila kujua ingekuwa vzuri kama angepisha mapema ili kuitengeneza Rwanda mpya huku akitoa ushauri na uzoefu kuliko sasa ambapo anaweza fariki bahati mbaya labda kwa uzee alafu nchi haijandaliwa kiongozi wa kumrithi ndio unatokea ugomvi zaidi wa kikabila maana sidhani wahutu watakubali nchi iende kwa mtutsi mwingine so itazuka vurugu na mengineyo!! Sasa nani atampenda kiongozi asiye na kiasi??
 
Back
Top Bottom