JF Hard Talk "Zitto junior"

1. Zitto junior ana taaluma ya uchumi na biashara kuhusu level ana degree moja na kwa sasa ndio anamalizia masters masuala ya international trade.

Pia nimeanza kozi ya theologia ili kuongeza maarifa juu ya maandiko na hasa kupata majibu kwa baadhi ya maswali yangu

2. Kitabu cha Henoko ukikigrade na Biblia unaweza ukakiona kama kina makosa ila ukikisoma kwa akili neutral utakiona kina nondo nyingi sana tu na ndio maana hata Mtume Yuda kwenye Biblia pamoja na muandishi wa Timotheo wa 2 wamecite mistari kadhaa kutoka humo ila akina sie tukikisoma tunaonekana wapinga kristo!! Mind you kanisa la Ethiopia orthodox wamekitunza mpaka leo toka enzi na enzi na kinatambulika kama kitabu kitakatifu.... So hapa nafkiri ni suala la maamuzi tu kukubali Canon ya waafrika wenzetu au ya wazungu!! Cha kushangaza watu wengi wanaona ya wazungu pekee ndio ipo sahihi bila kujua ukristo ulikuwepo Misri libya na Ethiopia hata kabla haujafika ulaya!!

Kuhusu David Icke nilimuelewa sana kwenye kile kitabu chake cha the biggest Secrets nilikisoma 2013, alipokuja na nadharia kuwa civilization ililetwa na martians kutoka nje ya dunia... Akaleta na ushahidi wa michoro ya UFOs,ndege,solar system n.k kwenye mapango iliokuwepo kwa miaka maelfu na maelfu kabla hta space discovery kufanyika!!

Anyway kuna nadharia zake ambazo bado zimepingwa kwa sana tu ila hata yeye aliweka angalizo kwamba hujalazimishwa kuamini na akasema kama zitateteresha imani yako unaweza acha kusoma kitabu chake hicho cha Biggest secrets. So namkubali sio kwa sababu ya nadharia zake bali kuamua kuwa free thinker na kuhoji masuala magumu

That's all....
 
Mkuu kuhoji kuhusu mnara wa babeli sio kuhoji adhabu ya Mungu bali nahoji misinterpretation ya huo mnara kuwa ulitaka kumfikia Mungu KIMWILI..... Na ndio maana nikasema ili uelewe unatakiwa usome sources za nje ya Biblia upate picha halisi mfano wanaume kuhesabiwa peke yao kwenye Bible suala hilo limepata jibu NJE YA BIBLE kwamba ilikuwa mila ya wayahudi. Hivyo ukisoma outside source utagundua minara ilijengwa kibao tu huko Sumeria ila ilikuwa size ya ghorofa 3 au 4 ila ilikuwa inatumika kufanyia matambiko!!! Sasa haya maelezo ndio unaconnect dots na mnara uliojengwa na ndio maana tafuta kokote hutowahi pata hata msingi wa mnara mkubwa uliozidi ghorofa hata 10 tu ndio sembuse huo uliotaka kufika mawinguni!! Mbona pyramids zipo hadi leo??

Ndio maana nasema Bible imejaa lugha ya mafumbo jikumbushe suala la hekalu hapa

Yohana 2
19 Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha.
20 Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu?

.

Unaona hapa Yesu alikuwa kwenye hekalu na akasema wakivunja hekalu atalijenga..... Wayahudi wakapigwa butwaa hapa ndio akajibu

21 Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake

Hii ndio BIBLIA mkuu hata kuna sehemu miti inamaanisha wanadamu na mwanamke inamaanisha mchungaji!! Sasa ukisoma kichwa kichwa utapigwa butwaa kama hao wayahudi waliodhani hekalu ni jengo la kimwili
 
Hapana mkuu hapa pia utapotoka meza ya Bwana huwa sio PHYSICAL kwamba ukila divai na mkate ndio unakuwa umefanya meza ya Bwana come on brother!! Tunahitaji darasa la moja kwa moja

Kama unaamini Yesu alimaanisha mkate na divai ndio utamuokoa mtu basi nisaidie hapa inawezekanaje maana alikuwa hai bado
Yohana 6
53 Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.
54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho


Karibu
 
Mkuu yani ulipo jarbu kuelezeaa hilo somo la yohana; mimi sikatai kilicho andikwa,
Pia kama tafsri ya neno hilo tena limetolewa kwenye bible ni sawa.

Ndio maana nikakwambia toka mwanzo, maana ya maandiko hupatikana humo humo ndani ya bible na sio nje ya bible. Note hapo.

Pia swala la minala mingine iliyojengwa na maelezo ya kirefu kuhusu minala hiyo ww unaamin vi story za nje ya bible kirahis rahis hivyo?


NARUDIA TENA KUSEMA BIBLE HAIJAOUNGUKIWA KIASI CHA SISI KWENDA KUTAFUTA MAANDIKO MENGINE NJE YA BIBLE.

KWANI NJE YA BIBLE WAMEJAA WAPINGA KRISTO.

WATAKURUBUNI TU.


sasa kifungu cha biblia kinachosema alikua akizungumzia hekalu la mwili wake, kifungu hcho kwenye bible kipo wapi??????????????
Au umekwenda kutafuta maana nje ya bible???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante kwa mengi ya kweli na mengine mengi tu ambayo nadhani unapaswa kujifunza zaidi hasa Neno LA Mungu kupitia Biblia maana bado mchanga sana.. Je! Hili Neno figurative umelitumia sana kusema Biblia zaidi ni figurative je! Kiswahili chake fasaha ni nini??
 
Hivi ukijua Adam na Hawa walikula tunda gani
Apple au embe au komamanga au pera inakusaidia nn? maishan mwako?

Sent using Jamii Forums mobile app
Yesu alisema hivi

Mathayo 13
11 Akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuijua siri ya ufalme wa Mungu, bali kwa wale walio nje yote hufanywa kwa mifano,
12 ili wakitazama watazame, wasione;Na wakisikia wasikie, wasielewe;Wasije wakaongoka, na kusamehewa.
13 Akawaambia, Hamjui mfano huu? Basi mifano yote mtaitambuaje?

Kwahiyo usipojua hayo mafumbo/parables basi Yesu anasema utakuwa unatazama maandiko ila huoni kilichoongelewa!! Ndio hapo unaweza ona tunda halina maana kujua ilihali kupitia Biblia tunaamini ndio limesababisha kadhia yote hii!! Huoni usipojua maana yake utarudia makosa.
 
Mbona nimekiweka

YOHANA 2:21
21 Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake
 
Hahahaaaaaaa.
Hahahaaaaaaaa

Zitto JR
Ni kweli muda huo Yesu alikua hai, na ndio maana aliwaambia wanafunzi wake kuwa
wanye divai na kuhula mkate, kwani huo ndio mwili wake na damu yake itakayo mwagika pale msaraban FANYENI HIVI KWA UKUMBUSHO WANGU.

Huo ni ukumbusho.
Sasa wew ulitaka ajikate ka nyama na ajitoboe atoke damu awape wanye????

NAOMBA MKUU UNIPE NA MAANA YA MANENO HAYO KAMA KWELI SISI HATUSTAHILI KULA NA KUNYWA MKATE NA DIVAI.
TUPE maana ya maneno hayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Suriya kuhusu minara kuwa "habari za vijiweni" basi nimekuomba angalau uniwekee hapa ugunduzi wowote wa mnara/pyramid lililozidi hata ghorofa 10 tu huko babel (Iraq ya sasa) ukilipata ndio nitaamini kuwa mnara wa babeli ulikuwa unaelekea mawinguni.

Sasa mimi ushahidi wa uwepo wa minara huko babeli ninao mfano El ziggurats.... Unaweza google tu uone hio minara alafu sasa ndio tuje tuhojiane je nani kapotosha maandiko!!
 
Mbona nimekiweka

YOHANA 2:21
21 Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake
Yaaah naona maana ya kile alichokisema imeelezwa hapo hapo wazi wazi,

Ndio maana nikwambia, maana ya mafumbo ya vifungu vya bible hupatikana humo humo kwenye bible na kama hakuna, basi ujue maana yake ni hiyo hiyo kwa jinsi ulivo soma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu inaonekana husomi maandiko hayo maneno hakusema akiwa na wanafunzi wake alisema akiwa kwenye mkutano wa injili .... Hayo ya meza ya bwana kaongelea alipokaribia kufa

Ndio maana nimekuhoji wangewezaje kula nyama yake kama alivyowataka wale wayahudi?? Hapa hakusema ukumbusho popote alisema WAILE NYAMA YAKE

Embu nieleweshe alimaanisha nini
 
Yani unamaanamisha unataka mm nikutafutie uthibitisho wa kile kilichoandikwa kwenye bible???????
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe unakubali hilo sasa kwanini ukiambiwa tunda halikuwa APPLE mnakataa ilihali maaja imewekwa ndani ya Bible.... Hata mti wa mema na mabaya haukuwa mti kama mti bali ni fumbo ila mkiambiwa mnadai tunapotosha

Embu nikupe homework kasome Ezekiel 31 leo usiku alafu uje unielezee umeelewa nini
 
Noooooo,

Mimi sio hao wakaataaji

Kwan kuna watu hawali apple kisa jambo hilo??????
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani unamaanamisha unataka mm nikutafutie uthibitisho wa kile kilichoandikwa kwenye bible???????

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maana nikasema wwe una hatari ya kuwa kama wale wayahudi walioambiwa hekalu wakadhani ni JENGO

Ndio maana leo hii kuna watu wanapotoshwa sijui Israel watajenga hekalu sijui mpinga kristo ataishi humo hawajui kumbe hekalu atakuwa MTU

Kasome Wakorintho 3:9 na 16 Biblia inasema hekalu ni MTU!!

Nilicheka sana wakristo humu JF walikuwa wanatoka mapovu kusherekea kuzaliwa ndama mwekundu eti ndio sign ya siku za mwisho sababu hekalu linakaribiwa kujengwa

Mkuu taratibu tutaongea lugha moja wakati ukifika
 
Hahahaaaa ninmafumbo yapi hayo mkuuu, mbona toka mwanzo hujanipa maana ya fumbo hata moja???????

Mafumbo ambayo yametolewa maana humo humo kwenye bible mm siyakatai.


Lakin unaponiambia fumbo umelifumbulia nje ya bible
HAPO NDIO SIKUELEW KABISA.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mimi silipingi hilo lililotolewa maana ndani ya bible kabisa.


Swali langu la kuhusu fumbo la uumbaji wa Mungu hujanijibu kabisa.

Na fumbo la mti wa katikati, hujanijibu kabisa

Najua ni kwasababu unayo majibu kutoka nje ya bible.

Lakin majibu kama yatakua ndani ya bible wew niambie tu nitajua.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto hebu tuwekane sawa kwanza mala moja,

Naona unazidi kuniambia yale ambayo mm sijayapinga.
Na kuniambia yasio nihusu
Hayo ya ndama mwekundu mm siyatambui.

Naomba unipe majibu kwa yale ninayo kuuliza.

Naomba unipe maana ya kula mwili na damu yake yesu alimaanisha nn?????

Naona wew totally unayo majibu nje ya bible
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto acha siasa, kama unakataa nilichokisema tupe basi majibu au maana ya maneno hayo.
Acha kuzunguka zunguka.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…