JF Hard Talk "Zitto junior"

Figurative maana yake ni maana ya kiroho ya neno mfano Biblia inaposema moto inamaanisha NENO LA MUNGU na kwa wenye dhambi ina maana nk NENO LA HUKUMU ukisoma Yeremia 23:29 utaona hilo ila kuna watu wakisoma huu mstari wanadhani ni moto wa kimwili

Ufunuo 8:7
7 Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyotangamana na damu, vikatupwa juu ya nchi; theluthi ya nchi ikateketea, na theluthi ya miti ikateketea, na majani mabichi yote yakateketea.

Ssa figurative language ndio litakusaidia kuelewa biblia maana kila neno linalotumika lina maana yake kiroho sio kimwili..... Nafkiri tumeelewana hapa
 
Nmetoa moja hapo kuhusu MOTO.... MTI .... HEKALU.. Na nmekupa homework ya Ezekiel 31

Kama hapa tunakubaliana kuhusu mafumbo then well and good

2. Kuhusu kutoa baadhi ya mafumbo nje ya Bible unakataa ambayo uko sahihi kabisa lakini sasa nikuulize Biblia inasema Yesu alilisha WANAUME 5000 je ina maana kwenye huo mkutano kulikuwa hakuna wanawake na watoto???

Naomba unipe jibu kutokea ndani ya Biblia ukikosa basi naomba utamke rasmi kuniunga mkono kwa KUNIELEWA KABISAAAAAAAAAAAAA
 
Zito acha siasa,

Hayo maandiko unayo yasema hakuna anae yapinga,
Ila unavotuambia kuna mengine unatafuta ufafanuzi nje ya bible,

HUKO KAPOTEE PEKE YAKO, SISI WENGINE TUMEGOMA.

Yani unakazana tu kuniambia kuwa bible ina mafumbo ndio SIKATAI, lakin tafsir haipo nje, ukisema ipo nje ya bible NAKATAAAAA.

maana hata mm nikija kudanganya watu na kuwaambia hile amri ya kwamba USIZINI, Maana yake ni usilale na binti ambae kaolewa, lakin ukilala na mabinti wowote ambao hawajaolewa hata kama kumi, hata kama ndugu yako basi watu wataamini ufafanuzi wangu wa nje ya bible kuwa niwa kweli?????
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kwanza unipe ni kifungu gani kilichosema hayo,

Kuwa alilisha wanaume 5000.

Alafu ndio nikwambie kwann walitumia kauli hyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto acha siasa, kama unakataa nilichokisema tupe basi majibu au maana ya maneno hayo.
Acha kuzunguka zunguka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kula mwili na damu yake alimaanisha mafundisho yake yaani NENO LA MUNGU twenda pamoja

Yohana 6
35 Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.

Hapa Yesu anasema yeye ni CHAKULA hivyo atakayemla hatosikia njaa wala kiu..... Je njaa na kiu ya kimwili??

Amos 8:11
11 Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya BWANA.

Kumbe alikuwa anatimiza huu unabii hapa.... Sasa hapa kama hujui figurative language utakalia kusema meza ya bwana ni divai na mkate unashangaa Yesu anarudi anakuacha maana wakati ww unafakamia mikate kumbe Yesu alimaanisha ufakamie MAANDIKO YAKE

Wakristo tuamke biblia is FIGURATIVE LANGUAGE mwenye masikio na asikie
 
Nimejifunza kitu kwa . zitto junior. Ni mchambuzi mzuri ila ana athiriwa na tatizo la mapokeo amejifunza ana uelewa mzuri lakini anafungwa na mapokeo ni ngumu kubadirika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ni kweli hapa unachokisema Kristo alimaanisha kuishika kweli yake kiimani.
Lakini Kuna koment yako ktk huu Uzi ilinihuzunisha sikuamini Kama ni wewe kuhusu madhehebu na nilikuuliza hukujibu!!!

Je kanisa la nabii Tito wa dodoma waumini wake wanajihesabu haki uonavyo kulinganisha na maandiko ya Biblia?
Naomba unijibu je tukiishi katika madhebu yenye mafundisho yasiyoendana na Biblia huku tukijua tumeipoteza kweli ya Kristo inatufaa kujiona tu wenye haki wakati kweli tunaijua tumeiacha??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkate na divai...... ---Means kula na kunywa Neno la Mungu.


Hahahaaaaa mkuu kadanganye machoko,

Ukipinga kushirik meza ya bwana wew utakua umewapinga waluther na wacatholic piaa

Sasa hiyo dini yako ya uwongo sijui inamaana gani hasa.

But akili yako imekituma huko basi sawa yaishe.
Mimi sina la ziada nimenyoosha mikono.

Na sijajua elimu hyo unaisoma kwa madhuni gani??? Elimu ya uwongo mwanzo mwisho.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida yako hunielewi kabisa nimeshaweka msingi kwamba maneno yote ya Biblia yana maana ndani ya Biblia hili umekubali maana na ww naamini umepotoka

Nilichosema kuhusu nje ya Biblia sio mpaka yawe mafumbo bali ili kuelewa kitu kwa muktadha wake kwa undani zaidi hasa kama biblia hakijaieleza vizuri na ndio maana hata Yuda na timotheo wamemcite Book of enoch!! Sasa ina maana ww unajua maandiko kuliko Yuda na paulo??

Kingine nje ya Bible sio upotoshaji bali kuna vitabu vimetambuliwa na Bible na kuna makanisa yanavitumia mfano book of enoch na Book of jasher so ikiwa kanisani kwako ni NJE YA BIBLIA basi tambua makanisa mengine na NDANI YA BIBLIA.

Narudia tena Hakuna kitabu ambacho nimewahi jengea humu hoja JF ambacho hakuna kanisa ambalo linakitumia.... Vitabu vyote navyotumiaga ambavyo kwako unasema Ni nje ya biblia huwa ni ndani ya biblia kwa makanisa mengine so usilazimishe Canon ya Biblia yako ndio iwe sahihi hauwi objective.

Namalizia kwa kumnukuu martin luther aliyesema Apocrypha ingawa sio part ya bible ila ni VIZURI KWA MAFUNDISHO

So ina maana martin luther hajui Biblia!!
 
Hahaaaaaaa

Wew hayo makanisa yanayo tumia hvo vitabu ni wao mimi siwatambui hata kidogo.


Lakini swala la wew kunimbia kuwa Yesu aliposema tule mwili wake na kuinywa damu yake kamaanisha kuwa ni NENO LA MUNGU.

Nakataaaaaaaaa

Kama vip tengeneza uzi ukitoa maana ya andiko hilo utajiome kuwa ni ww peke yako ndio unatambua uwongo huo.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu alichouliza ni dhehebu gani liko sahihi mimi ndio nmejibu yote yako halali maana dhehebu halimpeleki mtu mbinguni ila niliweka msisitizo na nafkiri wengi mmeupuuza.

Kwamba.... Muhimu kujua maandiko sasa basi kama utajua maandiko ni obvious utafahamu kama kuwa Mwakasege au Nabii tito kapotoka so hata ww ukiwa dhehebu lolote ukijua maandiko utakuwa DHEHEBU SAHIHI kabisa huo ndio ulikuwa ufafanuzi wangu mkuu
 
Chief hapa kuna kitu unatakiwa kujiifunza kabla ya kumwita . zitto junior. Muongo waweza chukua Bible yako ukajipa mda kusoma mwombe roho mtakatifu akuongoze na fahamu kuwa kushiriki Meza ya Bwana hakufai kitu Kama haujamkaribisha Kristo maishani mwako
Zitto Junior kwa hili yupo sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mjadala ulianza vizuri tu kulikuwa hakuna haja ya matusi try to control your temper ndio maana mmeiita HARDTALK sasa mkianza kukashifiana kisa kutofautiana misimamo sidhani kama mjadala unakua na maana tena

Tukirudi kwenye hoja..... Mimi nimekuuliza hata kabla Yesu hajawapa agizo wanafunzi wake mezani aliwahi kuhubiri mlimani na mstari nimekuwekea akasema

Yohana 6:54
Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

Sasa kama unakataa hii maana yangu naomba unisaidie je Yesu alimaanisha kuwaambia watu wale NYAMA YAKE.

Nakusubiri
 
Kushiriki meza ya bwana hakufai kitu!!!!!!
Wew wasema.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asee,sasa mbn km unapanic ,tunawafuatilia sie wengine tujifunze kitu hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu maana itabaki pale pale, kwamba alitaka tufanye hivo kwa kula na kunywa mkate na divai na sio kwa

Na sio kwa kumkata Yesu kwa ajili ya nyama na damu..
Ndio maana ukaitwa ishirika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…