Jf ilinikutanisha na tapeli wa mapenzi

Ninachokiona ni kuwa hawa walikuwa wapenzi wa kweli,hakuna aliemdanganya mwenzie LAKINI inawezekana jamaa alishamchoka bibie............akafikiria atamtokaje wakati mamaaaa kafa kaoza,ikabidi jamaa afanye alivyofanya. POLE SANA.
Dunia ndio ilivyo cha msingi ni kujua kuwa si wanaume wote wapo hivyo.

Wakati unasikitika kukutana na mzimu hapa JF wenzio wanashukuru wamelamba dume. Bahati mbaya umelamba galasa. Siku nyingine CHANGA VIZURI KARATA NA SIKU ZOTE WEWE NDIE UWE MCHANGAJI........Sijui kama unanielewa.
 
Dah!umeamua kumchana Rejao hadi kwa hapa?usimuwaze ni snitch tu#
 
pole matapeli kila mahali sio kwa mtandao ni wewe tu kufanya utafiti wa kina kama unataka kuwa serious na mtu vinginevyo usanii mwendo mmoja afu ngoma inakuwa droo
 
pole shosti
mungu atakupatia haja ya moyo wako
kiukweli humu humu kuna watu na viatu
kuwa makini
wanaume si watu ni viumbe
 
Pole dada! ni kwel mimi nilishawai kurusha tangazo maksudi kuwa natafuta mwanaume aliyekuwa serious wa kuanzishanae familia kwa makusudi ili nijue kama jamaa wangu ataaply du nilishikwa na butwaa pale nilipoona jamaa wangu na yeye anrequest1 jamani tujiathari na matapeli wa mapenzi
 

Duh!, nimecheka sana. Hii kali, lakini nae inawezekana alikujua akataka kuona respond yako.
 
Let me be an opportunistic, as you know kufa kufaana bana sasa natangaza nia kupitia thread hiii hii...sifa zote ninazo...
1. An athletic body
2. Broad Shoulder
3. Tembo Card ipo Vizuri
4. GX 100 ipo.
5. A Mansion
6. Age mule mule fall in your category
7. A very honest Man
8. I have wife and Daughter

Kwa sifa hizi bila shaka...nategemea kupokea maombi ya kutosha ya usajili.....dirisha la usajili litafungwa baada ya mwaka mmoja!!!! Am serious about this who ever interested or in need she is welcome, with warm welcome
 
pole sana ila sijui lini mtajifunza kuwa uhusiano wa kufaa huwezi kuupata kwenye mitandao
inategemea,mbona kuna wengi tu mpaka wamefanikiwa kuoana?
cha msingi ni namna tu ya kuanzisha huo uhusiano
 
Nimepitia maoni yenu wote, kwa mlionipa pole ninawashukuru sana. Ninaomba pia niweke wazi mambo yafuatayo

1. kuhusu kuonana live tulishaonana na alionekana ni innocent na mcha Mungu kwa maneno yake, pia kwa muonekano sio mtu mbaya au anayeonesha kuwa na tabia mbaya
2. Kwa waliokazia kuhusu ulaji wa tunda, sina haja ya kumdanganya mtu nisiye mjua na asiyenijua ukweli ni huo kwamba kamwe hakuwahi kuuona utupu wangu na kwa hilo siko na sikuwa mrahisi kwa yoyote yule. Kwahiyo kama wewe unalazimisha kuamini hivyo wewe amini tu upendavyo ila tunda ni langu na halikuliwa.
3. Watu hukutana popote na kufanikiwa kuwa na mahusiano yenye manufaa tu, hivyo kukutana na mtu online, street, kanisani au kwingineko hakucount ila ni aina ya mtu uliyekutana naye ndio inacount.
4. Hata kama ingekuwaje, bado ingekuwa vigumu kwa mimi kujua mambo ya mahusiano yake kwani mpenzi wake yuko mkoani kama nilivyokwisha elezea kwenye post yeye ndiye anayejua wanawasiliana lini na kwa namna gani.
5. Hii post iko hapa ili kuwapa somo wengine ambao kwa njia moja au nyingine wana mpango wa kuanzisha mahusiano ili wawe makini na kutojirahisisha kabla ya kujuana kwa undani iwe online, street n.k.

Otherwise michango yenu wote kwa upande mmoja au mwingine inajenga kutegemeana na nini unaamini as far as relationship is concerned.
 
Ole wako uje uniumbue na ule mtongozo nlokupiga juzi.....😛hoto:

hahahah babu bana......we hata ukinirushia tongozo mi nitajua ni upendo tu wa sweetie babu lol!! Sasa babu ODM ebu nenda chamber basi unipe kataarifa!
 
Mhh makubwa tena haya! sasa wanaume nyie mkoje lakini? msipokuwa na vidumu hamjisikii kabisa?kwani mna matatizo gani nyie wwanaume?lazima tu mchovye weeeeeeeeeeeee ndo mpate raha, haya sio maisha badilikeni muwe wakweli
 


Baelezeye baelewe ati
 
Njoo kwangu mama hutajuta hata kidogo.
 
Chunga sana, kuna kisa kililetwa juzijuzi na mwana JF wa zamani kuhusu haya mapenzi ya kwenye mtandao kumbe mtu alikuwa unausambaza UKIMWI makusudi kabisa. Pole.

FaizaFox bora umeropoka ingawa ukweli ni kwamba umetoa onyo kuwa na uangalifu sana. Nisingependa JF itokee kama mtandao fulani wa bongo... ulivyokuwa na mazoea ya kusema mikutano ya kujuana, matokeo ni kweli waliokuwa wanakutana kwa ajili ya kujuana walijuana kiukweli na kikamilifu, leo yanayowasibu wanayajua wenyewe kwa kutokwenda huko na akili mbili. Na baadhi yao labda imebaki historia ya kusimuliana wakati walikuwa vijana wachanga vijana wachanga wenye ndoto nyingi na kubwa katika maisha na taifa.

Ulimwengu wa leo njia bora na rahisi ni kukutana online, lakini hapana budi kuwa na tahadhari kubwa sana, maana tunadili na kufahamiana na watu tusiowajua wala kuwaona, na kabisa tabia vigumu kuifahamu kama hujapata muda wa kuwa karibu naye na kusoma maisha yake yalivyo. Dunia hadaa, ......shujaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…