JF ilivyoua huba langu

JF ilivyoua huba langu

Kwani nyie si ndio tuko nanyi mitaani huku 🤣

Uzuri wa jf inaonyesha tabia halisi za watu mitazamo, akili, mawazo ya jamii yetu kwa sababu uwepo wa id fake umefanya watu wawe huru kufunguka
Yaani angenikiuta na hii ID ya sa hivi ilivyohuru ndio angezimia😁😁
 
Samaleko,

Basi bwana, miaka kadhaa nyuma nilikuwa na Id yangu xxxx, haikuwa Maarufu hata kidogo, nilikuwa napenda kumchangia kidogo kwenye Jukwaa la siasa, intelligence na international news na History.Sasa Maulid moja akaja ex shemeji yenu kunitembelea,Kwa kawaida nikiwa nyumbani napenda sana kumsikiliza Country music,basi nikawa nimewasha laptop zile miziki zinaimba,halafu tab nyingine nilifungua JF,Sasa yule bwana alivyofika Mimi napikapika akasema bwana mi natoa Hawa wababu wako,Nia abadilishe aweke miziki anayopenda yeye,Mimi Niko zangu napikapika,basi Ile anaendelea kushikashika laptop nikasikia naulizwa,
Baby una account Jamii forum?
Mi kiroho safi nikamjibu eeh mbona siku nyingi[emoji16][emoji16]
Eeeeeh bwana nilisimangwaaa,nilisomewa risala,niliambiwa sifai kabisa,Mimi sio wife material,maana mke wa mtu hawezi kuwa member wa JF.
Basi kila mkitofautiana utakisia wewe umeshaharibika sababu ya JF[emoji849],ikawa JF,JF,JF sipumui,mpaka safari ikaishia njiani...

Sasa nikawa nashangaa Ina maana wadada tulio JF tuna tabia mbaya kiasi hiki[emoji1787]??eti kina kaka mkigundua wapenzi zenu ni member wa JF mtakasirika?

NB:nilihisi lazima na yeye ni member humu ila sijui ID yake,nikabadili zangu ID chaaaa..

Happy Maulid to all
Na yeye hafai sababu ana account jf
 
Huyo alikuchoka alikuwa anakutafutia sababu hana lolote, sema ulikosea usingeachana naye kwanza mpk ungejua ID yake ili wazaramo tuwe tunampitia na kijembe 😂😂😂
Mzaramooo
 
Kwa kweli alitafuta sababu sio siri🤣🤣🤣
Si ndio hivi mzaramo Leo nimekumbuka nimemleta kilingeni wazaramo wenzangu mshughulike nae🤣🤣🤣
Mshenzi huyu alikuwa na yake
Akakutafutia sababu
 
Ile ya bunju ni story ndefu, tukiacha madhaifu ya kibinadamu na vikwazo vya kua na ID jf vp bado hujamiss zle moments nzuri tulivokua pamoja
🤣🤣🤣🤣Kwa like gubu lako nishasahau hata hizo good moments zenyewe
 
Back
Top Bottom