Stoudemire
JF-Expert Member
- Mar 24, 2012
- 839
- 207
, aisee wizi upo hadi ngazi ya familia ??!! Inatisha jamani lol, inatisha jamani usipokuwepo hesabu unapigwa bao tu tena bila huruma wala aibu!! Hongera mkuu tangulia ngoja nikusanye kamtaji uzuri utaalamu na uzoefu wa nitakachoenda kukifanya ninao, acha niandae kiberiti na petrol ya kuchomea meli.
pengine hizo biashara huwa na faida sana kiasi hata wakiibiwa kinachobaki kiakuwa si haba. ila kitu kingine nimejifunza ni kuwekeana malengo na mtu uliye muajiri na ajue kabisa kitakachompata asipofikisha malengo. hili liahitaji uwe umekaa kidogo kwenye biashara yako ili ujue jinsi ya kupangiana malengo na uliyemuajiri. kitu kingine ni documentations hiki muhimu sana. kitakupa mwanga jinsi mambo yanavyoenda. hata hivyo mkuu biashara nyingi tu kati ya hizo ulizotaja zinakufa kila leo hasa ya mabasi na nahisi sababu kubwa ni huu usimamizi wa remote control.
Mkuu Ngumakasi hata mimi nilikuwa mchunguliaji wa JF toka 2009 nikajiunga mwaka jana tu. Ukishaionja JF huwezi kuiacha! Heshima kubwa iende kwa waasisi na wachangiaji, hasa jukwaa hili ambalo limenibadili mtazamo na mwelekeo wangu! Mkuu Ngumakasi mimi bado nimenasa kwenye utando wa buibui ya ajira ya serikali. Huwezi kufanya ujasilia mali ukiwa kazini. Ni mara nyingi sana kila ninapojipanga na kuanzisha dili kubwa sana linalohitaji usimamizi wa karibu, ninapewa safari kikazi nakuwa nje wiki nzima au zaidi, nabaki naagizia kwa simu, nikirudi nakuta mkorogo tu kila kitu kimetibuka. Wakati mwingine maboss wakigundua unamiradi watakupa safari kila mara mwisho wa siku miradi inakushinda. Kinachotushinda tuliomakazini kufanikisha miradi kwa kasi yenye tija ni kutoweza kusimamia, na kwa hakika kwa jinsi nilivyoshuhudia watu wengi niliowahi kuwaomba wasaidie kusimamia walivyo wezi na waongo ninajiuliza hawa matajiri ambao wamesambaza miradi yao ambako wao hawako wanadhibiti vipi wizi, aisee wizi upo hadi ngazi ya familia ??!! Inatisha jamani lol, inatisha jamani usipokuwepo hesabu unapigwa bao tu tena bila huruma wala aibu!! Hongera mkuu tangulia ngoja nikusanye kamtaji uzuri utaalamu na uzoefu wa nitakachoenda kukifanya ninao, acha niandae kiberiti na petrol ya kuchomea meli.
Hongera sana mkuu.Ujasiriamali ni mgumu hasa unapoanza kwanza unakutana na changamoto ya jamii inayokuzunguka kukuona umechanganyikiwa kwanini uache kazi ambayo ilikuwa na uhakika wa kipato kila mwisho wa mwezi.Na hili ndio linalopelekea kushusha hari ya vijana kupata udhubutu wa kufanyamambo makubwa mana kwa tafsiri finyu ya kitanzania ukiwashukuwa na degree wewe hurusiwi kufuga kuku kama shughuli yako rasmi, ni lazima uwe kwenye taasisi ndo utapata heshima.Lakini mi naamini hizi shughuli zauzalishaji zikifanywa kwa nguvu zote na vijana amabo wameenda shule kuna mwanga mkubwa sana huko mbeleni.Hongera sana
Mkuu Ngamakisi nashukuru sana kwa wazo lako. Hapo kuna elimu kubwa sana nimeiona. Nitaliboresha zaidi maana hakuna jinsi. Kuhusu hayo uliyoyasema serikalini ni kweli hali iko hivyo. Hiyo hali ya security ndiyo adui wa maendeleo. Wataalamu wanasema mtu aliyeko kwenye CONFORT zone huwa hataki misukosuko. Kwa wenye damu ya ujasilia mali, piga ua kuajiriwa ni suala linapaswa kuwa la mpito tu na siyo kuchukulia kuwa nimefika. Nikilima eka 20 za mpunga ambazo ninazitunza kwa miezi 4 tu ambapo wala siyo full time toiling kama ofisini, mwisho wa siku naingiza kipato ambacho ni mara mbili ya mshahara wangu kwa mwaka mzima! (Just in 4 months tu), sasa hii miezi nane inayobaki ......., nikilima vitunguu tena? Sasa haya mavitu ninafanya kwa kujibanabana lakini nafanikisha hakuna shaka kwamba nikiyatokea mzima mzima sitajutia, labda mito yote ikauke na watu wasile chakula tena, Kaka tangulia nitakukuta, acha nimalizie kukamilisha maandalizi maana hata kuchoma meli kwenyewe ni nahitaji niandae kiberiti na petrol.Mkuu Kubota, binafsi hata mimi natoa heshima kubwa sana kwa waasisi wa na wachangiaji wa Jami FORUM. it's a forum of it's own kinn, yani madarasa kibao. na kweli ukiingia huku hutoki...lol big up sana. kweli kabisa ni tabu kweli kufanya yote mawili, ila perhaps ningekuwa nimeajiriwa na serikali yetu hii tukufu ninge manage. nasikia huko work load ni ndogo! sijui ni kweli? na ni kama vile hamjabanwa sana!! sijui pia kama ni kweli, na job security ipo ya kutosha as opposed to the private sector that i ve been working for ever since time memorial.
ninamfano mzuri wa jirani yangu mmoja amabe yeye nilifikiri amefanikiwa kwenye hili...yeye alikuwa vendor wa m-pesa, tigo pesa, dstv, luku,.you name them. wafanyakazi kila siku wanampigaje? ni shoti tu deile. baadae akaja akampata mtoto wa ndugu yake ambaye waliwekeana makubaliano tofauti kidogo. kwamba yule kijana atafanya kazi pale kwa uaminifu kwa miaka mitatu, atakuwa analipwa nusu tu ya mshahara wake wa mwezi. then baada ya miaka mitatu anamaliziwa the other 36 halves plus kumpeleka shule(yule kijana hakufanya vizuri form four finals). hivi tunavyoongea three years have lapsed na duka la jirani yangu lipo pazuri, na mtaji umekua, kijana hajawahi kuiba hata senti, hajawahi kupata the so called shoti not even once..na yupo shuleni amerudia form three. ila jirani yangu amerudi kwenye same challenge he was facing before, ya kupata mfanayakazi mwaminifu. labda hii inaweza kukusaidia mkuu.
Kila la heri.
Sana tu Kubota, yataka maandalizi sikatai. Mimi mwenyewe nime battle sana na akili yangu over this wala siwezi kuelezea. Ila kama upo kwenye comfort zone itumie mkuu, ni fursa kwako pia kufanya maandalizi yako vizuri pia kutunisha kale kamfuko ketu pendwa kale( naamini unanipata).
Hili swala la kuwa na wasaidizi waaminifu nalo ni changamoto kweli jamani. Nadhani ndio maana hawa wenzetu waasia n familia nzima inahusika na biashara. yani alomst all their businesses are home businesses ila bado kuna siri hatujaijua. mbona sisi ndugu zetu wanatupiga za uso? tena ngumi sio makofi yani mpaka mtu mzima unatamani kulia. hii inanisumbua sana kwasababu kufikia hatua ya kuweza kuajiri mtu na yeye akabenefit from your entrepreneurship ni sifa nzuri, it is a credit. kwahiyo mkuu siku ukipata the right mode for this tafadhali weka jamvini kwa faida ya wote.
Kila la heri
Najaribu kupiga picha, kuamka ucku si kwa kwenda msalani bali kuangalia vifaranga. Ujasiliamali unaweza kukufanya uonekane punguani kupitia macho ya raia wa kawaida.
Hongera kwa mradi mzuri na wenye mafanikio. Nimeandika nikiwa nimesimama kwa heshima yako mkuu. Salaam
Sema tu vile sie wafanyakazi, academics hatusemi yanayofanyika usiku vyumbani mwetu: nani ambaye hakukesha ili tu apate cheti, degree ili aende kutembeza bahasha aajiriwe? hata huku makazini bado kuna stress hadi kukosa usingizi: deadlines, evaluation, performance appraisals, training, presentations yote haya unavuna vi hela na vi praise ambavyo ni vya muda mfupi na sana vinazidi kukubana uendelee kuwa muajiriwa daima. Yaani mimi nakupongeza sana kwakweli na umekuwa wazi kuonyesha changamoto za ujasiriamali sio kutajirika haraka na bila kuwa committed kama wengi wanavyofikiria: ITS A MATTER OF DEATH AND LIFE, UKIISHACHOMA MOTO MELI THERE IS NO RETREAT NO SURRENDER!
Mkuu Kwenye Red hapo, Tatizo kubwa ni kuto kutoa elimu kwa huyo Ndugu yako watu wengi huishia tu kukabidhi majukumu bila kumpa elimu Ni lazima elimu ya kutosha itolewe,
- Ni lazima ndugu zako wapate elimu ya biashara, Umuhimu wa biashara yako kwako, Na faida gani watipata wao mbele a safari, watu huishia kuoneana aibu kisa umemeweka Shemeji yako so hata akfanya nini haulizwi,
Na mwisho ili kweli kufanya the real business basi huna budi ku opt moja, kuendelea na kazi ya kuajriwa au kuchoma meli moto na kuendelea na shughuri zako, Why? Wewe ndo mwanzilishi wa Idea, wewe ndo unapaswa kupigania wazo laoko na si mwingine yoyote yule, si mke wako wala shemeji wala mdogo wako wala kaka wala Dada it is you,
Biashara yako haiwezi kusonga mbele bila wewe na biashar sio kuanzisha na kuweka watu na wewe kubakia kupiga simu kuulizia, Mwazno wa biashara ni lazima upartcipate vilivyo na baadae ikisha kuwa kubwa ndo unawza kaiimisha majukumu, sasa tunacho kifanya ni kinyume, tunakaimisha majukumu mwanzo wa biashara,
Mama I could not agree with you more.
Hizi kazi za watu targets, mara andaa presentation, mara Appraisal mara sijui Internal Audit , mara compliance mara mtu wa Risk kapita, mara Extyernal Auditor yaani ni full stress. Nilipoanza kazi fresh from chuo macho yalikuwa yanaona vizuri, mwili ulikuwa mzuri sina hata dalili ya kitambi, mgongo hauumi, tumbo lipo safi. Sasa hivi hapa nilipo tumbo wanasema kuna vidonda, macho yameshaanza kufa kukodolea kompyuta, mgongo sometimes unauma bila sababu ya msingi, Kichwa nayo sometimes inagonga, kitambi nacho napigana nacho kufa kupona nikijisahau kinachomoza. Yaaani haya maisha ya kuajiriwa ni upunda na utumwa sijui kama sukari na BP zitanikosa within these 10 years nikiendelea.
Yes me too..!Oneday!
Mama I could not agree with you more.
Hizi kazi za watu targets, mara andaa presentation, mara Appraisal mara sijui Internal Audit , mara compliance mara mtu wa Risk kapita, mara Extyernal Auditor yaani ni full stress. Nilipoanza kazi fresh from chuo macho yalikuwa yanaona vizuri, mwili ulikuwa mzuri sina hata dalili ya kitambi, mgongo hauumi, tumbo lipo safi. Sasa hivi hapa nilipo tumbo wanasema kuna vidonda, macho yameshaanza kufa kukodolea kompyuta, mgongo sometimes unauma bila sababu ya msingi, Kichwa nayo sometimes inagonga, kitambi nacho napigana nacho kufa kupona nikijisahau kinachomoza. Yaaani haya maisha ya kuajiriwa ni upunda na utumwa sijui kama sukari na BP zitanikosa within these 10 years nikiendelea.
Binafsi namshukuru muanzisha uzi mkuu Ngamakisi, umetoa elimu tosha kwa vijana ambao wengi wetu mawazo yanakuwa yamegota kwenye kuajiriwa shukran mkuu na nakutakia kila kheri, pia michango ya wanajamvi wengine kama Mkuu chasha mzee wa KUCHOMA MELI, mkuu kubota, mama joe na wengine wengi siyo siri michango yenu inasaidia na inaelimisha katika kuondokana na janga zima la kuajiriwa. Shukran sana wakuu binafsi naendelea kuufuatilia mnakasha huu kwa umakin zaidi.
Ukweli utabaki kuwa ukweli, ila mkuu inauma hii kauli inauma. Huu ni mwaka wa kumi sasa kumbe nina accomplish someone's dream. Acha tukusanye mitaji kwao katika mazingira hayo hayo ya kufull fill their dreams. 2014 ni mwaka wa KUCHOMA MOTO MELI.you are there to accomplish his dream not yours. sorry kama naandika sana but this is the spirit i have.