JF is my homeland

Mkuu ngumbuke nakuunga mkono, mara nyingi ukweli kwa maana ya fact huwa mgumu kweli.Kwakweli kama kuna uwezekano wa kukusanya mtaji hapo ulipo please do it. mimi pia nawashukuru hawahawa waajiri. ugumu nilioupata umekuwa somo tosha kwangu, ila pia kiukweli sehem ya mtaji imetoka hapohapo. whether nilisave mshahara ama nilitumia mkataba wa ajira kama dhamana ya mkopo, fine tu. ila hili la kuchoma meli moto liko independent kidogo. zamani nilikuwa nikiona wafanyabiashara waliofanikiwa nadhani ni miujiza ila sasa najua ukweli, ni commitment inatakiwa because kiukweli ukilegea unaanguka mbona?[/QUOTE]
Kaka Ngamakisi, ninamshukuru Mungu kwamba hapa nilipo uwezo wa kukusanya mtaji mdogo wa kuanzia upo. Hata sasa ninapochangia mada hii, nimeshawasiliana na rafiki zangu wawili, mmoja alikuwa na wazo la kuendelea kuajiriwa kama nilivyo mimi ( sasa nimebadilika ), alipata kazi ya uhadhiri huko Makumira mwishoni mwaka jana, kwa mshahara wa 1.8 monthly,jamaa yake mmoja akampa shule ya kilimo cha mpunga na vitunguu( huko lumuma Kilosa). Huyu ndugu yangu sasa najihisi aibu kuongea naye.
Kwa sasa ninajipanga kwenda Lumuma kwa mwongozo wa huyu ndugu au Bagamoyo, bonde la mto Ruvu kuna jamaa mwingine ameanzisha kilimo cha vitunguu septemba hii.
Nina hakika sitokosa 3m ya kuanzia by feb 2014 nikishalipa ada za wanangu wawili. Mungu atutie nguvu na tuendelee kuelimishana na kutiana moyo.
Hakika kila kitu ni kuthubutu na kuwa tayari kwa matokeo kwani ni kweli hao matajiri tuwaonao na kuwashangilia kila siku walithubutu na kuwa tayari kwa matokeo yoyote yale. Sisi bado tumejawana woga na kibaya zaidi tunafikiri kuajiriwa ndio MAUJANJA!! Kumbe hakuna kitu.
 



nakupa moyo sana ngumbuke, ukiamua kwa dhati hakika utaweza. hii nchi imejaa fursa we usipime. huoni wageni wanavyoikodolea macho,ona hata viongozi wetu walivyochanganyikiwa mpaka wamebaki kununua ma ekari ya ardhi kila uchao? kila kiti kiko hapa nyumbani. utavuka amini.
 


Kaka Ngamakisi, nashukuru mno kwa kunitia moyo. Yaani sasa najiona kama kijana mmojawapo mwenye mafanikio hasa nisomapo topic hii na ile ya Eberhard.
Pia ongezea michango ya wataalam kama akina Chasa, Malila, Mama Joe na wengineo.
Kwa mijadala hii na mawazo ya kimaendeleo kama haya miongoni mwetu vijana hasa tunaoteseka katika ajira za sekta binafsi, mimi sasa ninauona mwisho ulivyo mzuri na watoto wangu watakavyokuwa na furaha na raha kwani baba yao nitakuwa nimewaandalia kilichochema!

Asanteni sana wana JF!
 
Hongera Mkuu kwa ujasiri wa kuthubutu kuacha kazi na kujikita kwenye ujasiriamali.Wengi wetu tuna hofu ya uthubutu ,tumeng'an'gania mishahara ya mwisho wa mwezi..Nashukuru umenipa moyo kupitia post yako.
 
one day yes!
bado nina changamoto 2 kubwa (sina umeme na sina uzio) but with time nitapata solution tu.

I just cant wait!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…