JF is my homeland

JF is my homeland

Ngamakisi

Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
93
Reaction score
45
habari zenu wana jamvi hili la ujasiriamali. kwa muda mrefu sana nimekuwa nikipita JF kama visitor tuu na sio user..ila ikafika kipindi nikaamua kabisa kuwa member.
My regret ni kwamba why didn't i know this site earlier? JF is so useful, has been so to me in one particular way.

tangu siku nyingi sana huwa najiona kwamba hii mambo ya kuajiriwa is not for me at all..nakuwa kwenye ajira kwa kujilazimisha sana ili kusudi angalau baadhi ya mambo yaende sawa..lakini siko comfortable. msahahara haukidhi, mazingira ya ajira somehow negative, room ya growth huioni(ni mpaka labda upate bahati ya kuwa na immediate supervisor ambae ni brilliant) habari ya savings ndo kabisa, ie never achieved

nimesha attempt several projects lakini zimekufa njiani, lakini haikunikatisha tamaa kwani najua wazi source ni nini--lack of close supervision. mimi nionavyo hakuna mjasiriamali mwajiriwa, hakuna..you cant be both(hapa naomba tuzingatie maana halisi ya ujasiriamali). so baada ya kuridhika na analysis yangu mwenyewe ofcourse na msukumo kutoka hapa jukwaani, nikafanya what everyone called me crazy, nuts, a fool,whatever! yes even my family. I simply said it was enough and quit my job. that was April 10 mwaka huu huu.

napenda sana kufuga kuku, mama yangu alikuwa mfugaji mwenye bidii, kweli kabisa pasipo my mom kufuga sijui kama mlango wa shule ningeuona. so nikaamza na kuku wa nyama, broiler. nili battle sana na swala la idadi, kuna wanaokuambia anza na wachache kama mia 2, wengine mia tano..ila mimi nikastick na imani yangu ya kijasiriamali---hakuna kuogopa wala hakuna kujaribu...nikanunua vifaranga elfu moja(by that time nimejenga chumba na sebule....still unfinished. nalala chumbani, nafugia sebuleni.niliwalea wale vifaranga kwa kuzingatia sana ushauri wa kitaalam, nina rafiki mama mmoja mtuzima kuliko mimi naye mkongwe wa kufuga alinisaidia sana. Katika vifaranga elfu moja walikufa watatu tu. ila inataka umakini. nilikua sitokitoki nyumbani ovyo, usiku ndo kabisa namonitor joto bandani. nilikuja kuuza jumla ya kuku 997. nilipata faida nzuri, nilifurahi lakini nilisikitika pia. nilijilaumu nilikuwa wapi siku zote..nimepoteza muda wangu mwingi in mylife kutumikia waajiri kwa stress nyingi, mambo za deadlines, targets, eeeh.

Kwahiyo mpaka sasa bado nafuga hao hao 1000, sijaongeza idadi, nakusanya mtaji vizuri, na pia nikwasababu banda langu ni dogo. naendelea kujifunza pia na mbinu nyingine za kupunguza gharama za uendeshaji. na pia ni commitment, sio kitu kidogo inabidi kujitoa hasaa. huwa nasoma comments za wakongwe wa ufugaji na kilimo huku jamvini naona kama they are speaking my mind! ujasiriamali is tough work but its profitable...kikubwa zaidi ambacho mimi najivunia, ni the fact kwamba im actually producing, selling my produce and making that money...i couldn't be prouder guys! kitu kingine imenifundisha sana kuwa mwangalifu wa matumizi, im so eye opened in this nowadays..

Lengo la kuandika post hii ni kukupa moyo wewe ambae unajijua ni mjasiriamali na unatamani sana kupractise, wacha kusita,risks zipo lakini kumbuka hata kwenye kuajiriwa risks pia zipo, tunazioverlook ili kujidanganya. Nisikuboe sana mpendwa, chamsingi fanya maamuzi. Napendaga kale ka slogan ka "kuchoma meli moto''.

LONG LIVE JAMII FORUM
 
posti yako nzuri sana mkuu. watu wengi huwa wanajidanganya eti. ''serikalini kuzuri, ukiajiriwa unaweza kuwa unafanya na mambo yako''. hili jambo huwa napingana nalo sana, kama ulivyosema hauwezi kuwa vyote. ujasiiriamal kweli ni vita na haitaji lelemama. big up sana mkuu.
 
Najaribu kupiga picha, kuamka ucku si kwa kwenda msalani bali kuangalia vifaranga. Ujasiliamali unaweza kukufanya uonekane punguani kupitia macho ya raia wa kawaida.
Hongera kwa mradi mzuri na wenye mafanikio. Nimeandika nikiwa nimesimama kwa heshima yako mkuu. Salaam
 
Mkuu story yako ni nzuri sana kwa kweli nimependa sana, Mkuu ni kweli kuhusu Ujasirimali hakuna Mfanyakazi Mjasiriamali mahali popote pale hapa Duniani,

Kuhusu Kuacha kazi, MKUU HIYO INAITWA KUCHOMA MELI MOTO, ni uamuzi mgumu kabisa na wenye kila aina ya uchungu, ni uamuzi uao weza kufikiwa na watu wachache sana,

That is why hata KUCHOMA MELI MOTO kulifanywa na Majeshi machache sana, Greeks, Spain, na Wachina enzi hizo

Na Kuhusu Ujasirimali, ni kweli, UJASIRIMLI SI KAZI YA KITOTO HATASIKU MOJA, ina hitaji uumilivu wa hali ya juu especially kama una tageti mbali, kuna changamoto za kufa mtu na wengi ndo hicho kinacho washinda.
 
Ngamakisi,

Ahsante sana kwa kututia moyo, tutavunja madaraja na sisi lakini wacha kwanza tumtumie muajiri kukusanya mtaji wa kutosha.
 
Mkuu Stoudemire changamoto zipo ila kwakweli za masoko sio sana...wafugaji wote tuliopo na bado hatujaweza kutosheleza demand iliyoko sokoni. sema tu inataka kuhangaika kuyatafuta hayo masoko. na si kwamba nauza kuku elfu moja in a day, it takes like 4 to 5 days. so kweli kuna changamoto. changamoto kubwa ni kuwafikisha umri huo mkuu.
 
Thanks mkuuRed Giant . mkuu mimi pia nilishajidanganya sana. kuna wakati kabisa nilitaka kuchoma meli moto mara likatokea tatizo la kiafya la mwanafamilia aliekuwa anabenefit health insurance through me nikaahirisha. challenges za huko zilivyonizidi ndo nikaamua. maana mshahara hautoshi kamwe(commuting expenses za dar tunazijua), mara nikaomba kabank loan(kakazidisha ugumu), ili kupunguza makali ya maisha nikaanza na vimikopo vya mtaani! aisee nilikaribia kupata kichaa. it's a vicious cycle na kujitoa hapo ni kufanya maamuzi magumu kwakweli. ila i have no regrets, non soever.
 
Najaribu kupiga picha, kuamka ucku si kwa kwenda msalani bali kuangalia vifaranga. Ujasiliamali unaweza kukufanya uonekane punguani kupitia macho ya raia wa kawaida.
Hongera kwa mradi mzuri na wenye mafanikio. Nimeandika nikiwa nimesimama kwa heshima yako mkuu. Salaam

Salute kwako pia mkuu pleo, najua tuko pamoja
 
Mkuu story yako ni nzuri sana kwa kweli nimependa sana, Mkuu ni kweli kuhusu Ujasirimali hakuna Mfanyakazi Mjasiriamali mahali popote pale hapa Duniani,

Kuhusu Kuacha kazi, MKUU HIYO INAITWA KUCHOMA MELI MOTO, ni uamuzi mgumu kabisa na wenye kila aina ya uchungu, ni uamuzi uao weza kufikiwa na watu wachache sana,
That is why hata KUCHOMA MELI MOTO kulifanywa na Majeshi machache sana, Greeks, Spain, na Wachina enzi hizo

Na Kuhusu Ujasirimali, ni kweli, UJASIRIMLI SI KAZI YA KITOTO HATASIKU MOJA, ina hitaji uumilivu wa hali ya juu especially kama una tageti mbali, kuna changamoto za kufa mtu na wengi ndo hicho kinacho washinda.

Mkuu Chasha asante sana, yani mimi hili jambo lilikuwa linanisumbua sana baadae ndio nikaja kugundua kwamba you can't be both. it's either you are A or B. and biliv me watu wengi sana wanafungua biashara zao, nzuri tu ila kwakuwa wanamkabidhi mtu mwingine na wenyewe kwenda walikoajiriwa, wanapigwa vibaya aisee. mwisho wa siku wanafunga biashara zao wakidhani kwamba hazina faida. nionavyo mimi biashara zote zina faida, ni commitment tu inatakiwa. haiwezekani mkaka anachoma mahindi mpaka anatoboa, we unafungua duka la vipodozi la mil 10 unachemsha, ni kujitoa tu. kumbuka kwamba huko ulikoajiriwa ni kwenye ujasiriamali wa mtu mwingine. you are there to accomplish his dream not yours. sorry kama naandika sana but this is the spirit i have.
 
Mkuu Ukweli ni Kwamba Huwezi fanikiwa kwenye biashara/project yako kama huta partcpate 100% katika hiyo Project, wengi tunafanya biashara kwa Limot controll, umewaachia, Wake zetu/waume/shemeji/binam/sijui Baba/Mama/Dada/Kaka/wachumba no waendeleze project zetu, sisi tunabakia kupiga simu jioni kuuliza mapato yameendaje na wala si kuuliza wateja wanasemaje au kuna changamoto gani bali ni kuuliza mapato.

Wakuu huwezi fanikiwa kwa stail hii katika Dunia hii ya ushindani, sema tu ni kwa sababu tunafanya substance business, Business for survive,

Wewe kama initiator wa Idea ni lazima uwepo full time katika eneo ambalo aidea yako inafanyika, that is why Mjasirimali mwanzoni yeye ndo kila kitu,Yeye ndo Meneja, ndo, surperviser, ndo mkurugenzi, ndo seller, ndo afisa masoko, ndo afisa ugavi na kazalika.

Mara nyingi tunashidwa kuendelea kwa sababu project zetu tumwaweka shemeji, sijui Dada, pale hao watu hawajui objective ya wazo, hawajui chochote zaidi ya kuuza tu,

so mkuu ni kweli huwezi kuwa mfanya kazi na mjasirimali, hii ni huku Bongo ndo tunaitana hivyo siku zinaenda ila kwa wenzetuni kitu hakiwezekani kabisa
 
Mkuu Ngumakasi hata mimi nilikuwa mchunguliaji wa JF toka 2009 nikajiunga mwaka jana tu. Ukishaionja JF huwezi kuiacha! Heshima kubwa iende kwa waasisi na wachangiaji, hasa jukwaa hili ambalo limenibadili mtazamo na mwelekeo wangu! Mkuu Ngumakasi mimi bado nimenasa kwenye utando wa buibui ya ajira ya serikali. Huwezi kufanya ujasilia mali ukiwa kazini. Ni mara nyingi sana kila ninapojipanga na kuanzisha dili kubwa sana linalohitaji usimamizi wa karibu, ninapewa safari kikazi nakuwa nje wiki nzima au zaidi, nabaki naagizia kwa simu, nikirudi nakuta mkorogo tu kila kitu kimetibuka. Wakati mwingine maboss wakigundua unamiradi watakupa safari kila mara mwisho wa siku miradi inakushinda. Kinachotushinda tuliomakazini kufanikisha miradi kwa kasi yenye tija ni kutoweza kusimamia, na kwa hakika kwa jinsi nilivyoshuhudia watu wengi niliowahi kuwaomba wasaidie kusimamia walivyo wezi na waongo ninajiuliza hawa matajiri ambao wamesambaza miradi yao ambako wao hawako wanadhibiti vipi wizi, aisee wizi upo hadi ngazi ya familia ??!! Inatisha jamani lol, inatisha jamani usipokuwepo hesabu unapigwa bao tu tena bila huruma wala aibu!! Hongera mkuu tangulia ngoja nikusanye kamtaji uzuri utaalamu na uzoefu wa nitakachoenda kukifanya ninao, acha niandae kiberiti na petrol ya kuchomea meli.
 
Mkuu Ukweli ni Kwamba Huwezi fanikiwa kwenye biashara/project yako kama huta partcpate 100% katika hiyo Project, wengi tunafanya biashara kwa Limot controll, umewaachia, Wake zetu/waume/shemeji/binam/sijui Baba/Mama/Dada/Kaka/wachumba no waendeleze project zetu, sisi tunabakia kupiga simu jioni kuuliza mapato yameendaje na wala si kuuliza wateja wanasemaje au kuna changamoto gani bali ni kuuliza mapato.

Wakuu huwezi fanikiwa kwa stail hii katika Dunia hii ya ushindani, sema tu ni kwa sababu tunafanya substance business, Business for survive,

Wewe kama initiator wa Idea ni lazima uwepo full time katika eneo ambalo aidea yako inafanyika, that is why Mjasirimali mwanzoni yeye ndo kila kitu,Yeye ndo Meneja, ndo, surperviser, ndo mkurugenzi, ndo seller, ndo afisa masoko, ndo afisa ugavi na kazalika.

Mara nyingi tunashidwa kuendelea kwa sababu project zetu tumwaweka shemeji, sijui Dada, pale hao watu hawajui objective ya wazo, hawajui chochote zaidi ya kuuza tu,

so mkuu ni kweli huwezi kuwa mfanya kazi na mjasirimali, hii ni huku Bongo ndo tunaitana hivyo siku zinaenda ila kwa wenzetuni kitu hakiwezekani kabisa

mimi hii nimei proove kabisa. nishawahi kuwa na restaurant, nilipigwa vibaya na wafanyakazi na mtu niliemuajiri kama meneja alinipiga vilevile..yani wahudumu wanamlia meneja timing na mteja pia anapunjwa vilevile. nilishafuga kuku pia awali(nyumba ya kupanga na banda la kupanga) kijana ana wa underfeed na aniba na kuuza pia. nilipokuja kusoma article fulani hivi iliyonitofautishia kati ya TRYING and DOING ndio nikaanza kujitambua: that ive never done a thing, was busy trying. utafunga biashara yako bure ukidhani hailipi kumbe ni nzuri sana na imeshamfaidisha uliemwajiri.

ila kama una passion huwezi kukata tamaa, it drives you to a point utataka sasa kufanya unachotaka na si kujaribu tena. jambo la ajabu sana its possible, ngumu yes lakini inawezekana. napenda nachokifanya. alafu surprisingly unashangaa pia unapata muda wa kufanya mambo mengine tena vizuri tu. waajiri wangu wote nawashukuru wamechangia kunichochea.
 
Kuna jambo lingine huwa linanitatiza sana pia. Utakuta mtu ana pesa cash lets say 2m, 5m or even 10m anaomba kushauriwa afanye biashara gani. Sipingi kwamba sio sahihi kuomba ushauri, ila napta wasiwasi kwamba hata huo ushauri hautamsaidia. Nafikiri ni rahisi sana kuanzisha, kumanage na kukuza venture yoyote ile provided uwe umeipenda. nimeshasoma sehemu nyingi sana kwamba''turn your interests and hobbies into business'' wadau hii imekaaje?
 
mimi hii nimei proove kabisa. nishawahi kuwa na restaurant, nilipigwa vibaya na wafanyakazi na mtu niliemuajiri kama meneja alinipiga vilevile..yani wahudumu wanamlia meneja timing na mteja pia anapunjwa vilevile. nilishafuga kuku pia awali(nyumba ya kupanga na banda la kupanga) kijana ana wa underfeed na aniba na kuuza pia. nilipokuja kusoma article fulani hivi iliyonitofautishia kati ya TRYING and DOING ndio nikaanza kujitambua: that ive never done a thing, was busy trying. utafunga biashara yako bure ukidhani hailipi kumbe ni nzuri sana na imeshamfaidisha uliemwajiri.

ila kama una passion huwezi kukata tamaa, it drives you to a point utataka sasa kufanya unachotaka na si kujaribu tena. jambo la ajabu sana its possible, ngumu yes lakini inawezekana. napenda nachokifanya. alafu surprisingly unashangaa pia unapata muda wa kufanya mambo mengine tena vizuri tu. waajiri wangu wote nawashukuru wamechangia kunichochea.
 
Hapo kwenye bold umenichoma mkuki moyoni lol!! Ilifikia hadi nilijiona kama natoa ajira tu kwa watu wengine ambapo mimi sikuwa nanufaika. Lakini wadau pamoja na kwamba tunaanza kidogo tukitarajia kupanuka ni muafaka kujiuliza na hili nimeliandika hapo juu lakini nauliza tena hawa wenye mabasi mengi, mtandao wamahoteli na maduka wanasimamiaje, wanatumia mbinu gani, maana nimeshuhudia kuna wizi wa kutisha Tanzania. Kuna culture ya wizi, watu wengi popote walipoajiriwa wanachowaza ni kujinufaisha kwa kuiba tu. Wajasilia mali mnadhibiti vipi wizi wa wasaidizi na wahudumu wenu? Tutaendelea bila kuhitaji usimamizi wa wasaidizi wetu?
 
Kubota kwa wenye mahoteli sina idea kwani kuanzia mchonga viazi mpaka mhudumu na cashier wapo kidili zaidi yanimpaka chakula kimfike mteja mezani ni shuhuli. ila kwa wenye mabasi(haya ya mikoani, mfano dar moro.by the way nipo moro) huwa nahisi wenyewe wanataka hesabu ya level seat times the number of routes travelled. vichwav ya njiani nafikiri ni halali ya dereva na konda.
 
Dah umenigusa kweli,mimi pia nimekulia kwenye ufugaji..nakumbuka nimehamshwa sana usiku kunyonyoa kuku.lakini ndio wamenifanya nifike hapa nilipo all the best..ukiwa na malengo na ukajipanga uwezi kuanguka.
 
Hapo kwenye bold umenichoma mkuki moyoni lol!! Ilifikia hadi nilijiona kama natoa ajira tu kwa watu wengine ambapo mimi sikuwa nanufaika. Lakini wadau pamoja na kwamba tunaanza kidogo tukitarajia kupanuka ni muafaka kujiuliza na hili nimeliandika hapo juu lakini nauliza tena hawa wenye mabasi mengi, mtandao wamahoteli na maduka wanasimamiaje, wanatumia mbinu gani, maana nimeshuhudia kuna wizi wa kutisha Tanzania. Kuna culture ya wizi, watu wengi popote walipoajiriwa wanachowaza ni kujinufaisha kwa kuiba tu. Wajasilia mali mnadhibiti vipi wizi wa wasaidizi na wahudumu wenu? Tutaendelea bila kuhitaji usimamizi wa wasaidizi wetu?

pengine hizo biashara huwa na faida sana kiasi hata wakiibiwa kinachobaki kiakuwa si haba. ila kitu kingine nimejifunza ni kuwekeana malengo na mtu uliye muajiri na ajue kabisa kitakachompata asipofikisha malengo. hili liahitaji uwe umekaa kidogo kwenye biashara yako ili ujue jinsi ya kupangiana malengo na uliyemuajiri. kitu kingine ni documentations hiki muhimu sana. kitakupa mwanga jinsi mambo yanavyoenda. hata hivyo mkuu biashara nyingi tu kati ya hizo ulizotaja zinakufa kila leo hasa ya mabasi na nahisi sababu kubwa ni huu usimamizi wa remote control.
 
Back
Top Bottom