JF Karibuni Tanzania Professionals Network

Mimi ni mtaalamu wa kupindua Nchi vipi nije?
 

Unataka kujiunga na TPN kutokana na kufahamiana na Mtsimbe toka Mnazi Mmoja ama kutokana na kuelewa Sera kamili za TPN?

Yaani umefuatilia TPN toka bado Kamati ya Uanzishwaji mpaka leo hii hukupata Hamasa ya kujiunga nayo? Mpaka moto huu ambao umewashwa hapa JF ndo umekufumbua macho? Hukuwahi wish kwamba ungekuwa among wanaotajwa kama Founding Members wa TPN?

Kuna namna hapa!!!
 

Kipanga Mweupe karibu sana. Kwa wale wenzetu wanaopanga kurudi nyumbani, tungependa kuifanya TPN iwe kama Labour Exchange Centre ya Professionals na pia Business and Projects Exchange Centre. We do hope this will assist our brothers and sisters who would like to come back home, to be sure of what they will do when they are back.

Nashukuru kwa kuweza kunikumbuka. Hakika ni miaka mingi sana. Karibu tuungane, wakati ni huu sasa. AGM itakuwa mwezi wa nane.
 


F2S nimekupata . . . TPN inachofanya kwa sasa ni kumobilize na kuhamasisha members wake wafanye miradi mbalimbali kwa kadiri wanavyoweza kuibuni na kui-present. Sasa hivi kuna walioungana kuendesha miradi fulani fulani. Nadhani ni mwanzo mzuri. With time miradi itakuwa mingi.

TPN kama Network haifanyi biashara lakini mipango yake ni kuwawezesha wadau wake wafanye mambo makubwa ya kuleta mabadiliko ya kweli katika nyanja mbalimbali.
 
F2S

Na wewe unahitajika leta mchango wake,

Remember, Mjenga nchi ni mwananchi. Njoo tuungane na TPN tujenge nchi, mawazo yako ni bomba sana!

Njimba

Thank you Wazalendo for supporting the intiatives. You are all welcome friends.
 
Ndugu Mtsimbe,

Katika kuboresha muundo wa jumuia yako, ni vizuri muweke sections zinazotenganisha taaluma mbali mbali ndani ya TPN. Kwa mfano mimi ni mwanachama wa IEEE (Institute of Electrical and Electronics Engineers) ingawa mimi siyo mhandisi wa umeme kama ambavyo ungetegemea, bali ni mhandisi wa mitambo (Mechanical Engineer). Ila kwenye IEEE kuna Automatic Control Society (ACS) ambayo ndiyo imenifanya niwe mwanachama wa IEEE. Vivyo hivyo huko kwenye TPN, ni vizuri muweke vijumuia vidogo vidogo kama hivyo ambavyo vinawakutanisha watu wa fani moja. Hiyo itakuwa na kivutio cha kuleta professionals mbali mbali wakitegemea kukutana na wenzao wenye backgrounds zinazofanana.
 
Ndugu S. Mtsimbe,

Mimi kama mmoja watanzania ambao wangeweza kujiunga na TPN nina machache ambayo ningependa kushauri na kupata ufafanuzi kabla ya kujiunga.

1. Nimepitia tovuti yenu, nimekutana na makosa kadhaa ya wazi ya lugha. Nadhani ni vizuri tovuti hii kwa sababu inawakilisha Tanzanian Professionals basi iwe na utaalamu wa hali ya juu. Napendekeza TPN itafute wahariri wazuri (tunao wengi) ili kuipitia. Mfano mdogo tu (na ipo mingi) mtu akisoma vision ya TPN kwenye ukurasa wa mbele haieleweki mpaka akifungua ukurasa wa objectives, ndio anaelewa. Wageni wenu wakitaka kuijua TPN watataka kusoma Vision. Wakishindwa kuielewa vision, wameshindwa kuielewa TPN.

2. Nashauri pia muwe makini sana na matumizi ya takwimu na taarifa mnazoweka kwenye tovuti. Ikiwezekana muonyeshe vizuri wapi mmepata (vyanzo) takwimu hizo. Kwa mfano, mkisema tanzania ni nchi maskini sana yenye watu zaidi ya "50% below poverty line...", basi mueleze chanzo. Kwa sababu hatuna hakika kama hiyo ndio takwimu sahihi. Na nadhani ni muhimu pia kuzipa takwimu nguvu - zimzungumze zenyewe bila kuweka maneno yoyote yanayoweza kuleta hisia za kuongezea "chumvi".

3. Jingine ambalo yawezekana ni swala la muonjo tu (na hili linaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu) na labda sio muhimu sana ni muonekano mzima wa tovuti hiyo. Kwa mawazo yangu tovuti hii inaonekana kama ya jumuiya kibiashara au klabu zaidi kuliko kitaaluma. Ingependeza kama mngekuwa na vitu vichache sana kwenye ukurasa wa mbele na rangi chache zaidi, kwa maana nyingine kusiwe na makeke mengi sana.

4. Mwisho, ningependa pia kujua umuhimu wa lugha ya taifa katika taasisi hii. Kwa sababu hii imekuwa ni conflict kubwa kwenye taaluma zetu hapa nyumbani na kumezuka mjadala mkali sana kwa miaka mingi wa athari ya lugha ya taifa na ya taaluma mashuleni kwenye maendeleo ya taifa. Na kwa sababu TPN itawajumuisha watu mbali mbali hata wasioweza kuelewa lugha ya kiingereza (kutokana na mission ya TPN). Je, mmefikiria swala hili na je kwa sababu hii ni taasisi ya wataalamu wa kitanzania na kwa sababu moja ya matatizo ya msingi ya watanzania ni wataalamu wetu kutumia mbinu za mataifa mengine kutatua matatizo yetu "local", je si vizuri chombo hiki kikalifanya hilo kuwa moja ya maswala muhimu kwa sababu kwa mataifa mengi yaliyoendelea huko ulaya na Asia ya kusini lugha imekuwa ni sehemu muhimu ya maendeleo ya kiuchumi.
 
F2S,

Tuwape mda tu hawa TPN labda hapo mbeleni watatuonyesha mambo makubwa nafikiri changamoto zako wataziona.

Thanks GM, something is already happening . . . . hoping that in August AGM we will have a new TPN more stronger and effective.

Our Treasurer is heading to Dodoma this week to open up a chapter. We have been informed by interested parties and members of TPN in Dodoma that more than 30 people has confirmed for a meeting.
 

Mzalendo Njimba, karibu sana katika Mtandao wa kweli . . . . Our next meeting is scheduled to take place on 31st August 2008. I forsee there might be some constitution changes. Also, we need to expand the leadership base as we have grown and there are so many challenges which needs collective leadership, so we may be requesting members to join the leadership team.
 
GM,

I can see tunafikiria kitu kimoja na kwa wakati mmoja!

what a coincidence!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Njimba

Wazalendo . . . mkishaanza kuona mitazamo yenu inafanana, ina maana muelekeo ni mzuri. Collective positive minds and attitudes is what will bring changes in this country.
 

Mzalendo Wakunyuti, nashukuru sana kwa mawazo yako mazuri. Nikitumia lugha ya kigeni . . "You have hit the bulls eyes". Nitafikisha maoni yako TPN na tutayafanyia kazi yote. Kama utakuwa DSM tarehe 31 August 2008 karibu katika AGM .
 

Mzalendo FairPlayer, hakika umenena, na hoja ya kutumia majina halisi hapa JF tumeshakubaliana kuwa haifai labda tu kwa sababu maalumu sana.

Tafuta muda ndugu yangu uanze kujishughulisha rasmi TPN. Njooni wote tushauriane na kusaidiana nini cha kufanya. Nadhani uwezo tunao mkubwa sana kama wote kwa pamoja tukiamua. AGM itakuwepo tarehe 31 August 2008.
 
Mimi ni mtaalamu wa kupindua Nchi vipi nije?

Du Mwanawani hii ni kali sana . . . LOL. Nadhani tunaweza kukutumia ndani ya TPN, si kwa kuipindua serikali iliyopo madarakani bali kwa kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii ili kuuondoa umasikini na kubadilisha hali za maisha ya Watanzania kuwa bora. Njoo tujadiliane . . .
 

Mzozo, katika kipindi kifupi ambacho nimekuwa katika uongozi nimejifunza mengi sana kuhusu wanataaluma wetu. Ukiacha wachache sana wengi wanapenda ku-observe kwanza wajue muelekeo . . . Watch and See . . . With time mambo yatabadilika.
 

Ndugu yangu Kichunguu, kuna mambo moja au mawili ningependa kuyagusia . . . Kwanza kuundwa kwa TPN hakukuwa na maana ya kuchukua majukumu ya vyama vingine vya kitaaluma ambavyo tayari vinafanya kazi yake vizuri. TPN inashirikiana vizuri sana na vyama hivi na ndiyo maana baadhi ya vyama hivi viongozi wake ni members wa TPN na wengine pia ni viongozi wa TPN.

Madhumuni makubwa ya TPN ni kushughulikia mambo ambayo taaluma moja peke yake haiwezi kuyamudu hasa ya kiuchumi nk. Hata hivyo mawazo yako ni mazuri sana ina nawezekana kabisa ndani ya TPN tukawa na vikundi vya wanataaluma zinazofanana. Nitayawakilisha TPN.
 
Mzalendo Wakunyuti, nashukuru sana kwa mawazo yako mazuri. Nikitumia lugha ya kigeni . . "You have hit the bulls eyes". Nitafikisha maoni yako TPN na tutayafanyia kazi yote. Kama utakuwa DSM tarehe 31 August 2008 karibu katika AGM .

Ahsante Kwa ukaribisho wako Bw. Mtsimbe. Tuombe Mungu yote yatawezekana.
 
Ndugu yangu HOFSTEDE sikubaliani na wewe suala moja kwamba kila tatizo ni CCM hapana. Bwana Sanctus alichoeleza yeye ni kitu tofauti kabisa na suala la taaluma sasa hiyo CCM huko kwenye taaluma inatoka wapi labda kuhusu hili suala la ajira nakubaliana na wewe kama utakuwa umeajiliwa ikulu na ikafika mahala wana taaluma mnakutana uso kwa uso hapo kuna utata, Lakini na imani mtandao wa TNP unajitegemea utakapojiunga huko siyo lazima ujitangaze kuwa wewe ni JF member
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…