Sanctus Mtsimbe
R I P
- Jul 14, 2008
- 1,820
- 1,032
- Thread starter
-
- #321
Brother Mtsimbe,
Thank you very much brother , I will be there live!
However, you have not mentioned the venue.
See you that day!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Njimba
kwa nini umeamua kuitambulisha TPN huku JF badala ya kutumia vyombo vya habari
Naomba nimsaidie Rais Mtsimbe kujibu swali lako kwa kukujulisha kuwa JF pia ni chombo cha habari.
Sanctus Mtsimbe, tembelea hii website hapa chini:
The Federation of Small Businesses, in UK
About the FSB
The Federation of Small Businesses is the UK's largest campaigning pressure group promoting and protecting the interests of the self-employed and owners of small firms. Formed in 1974, it now has 215,000 members across 33 regions and 230 branches.
Tanzania tuna network kama hii?
Hili ndilo bandiko la kwanza la Santus akiwa verified.Naitwa Sanctus Mtsimbe na naomba niungane na wana JF wengine waliojitambulisha kwa majina yao halisi na kuomba tuweze kuungana na kufanya mambo ya kimsingi katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.
Nimekuwa msomaji mkubwa wa JF toka mwaka 2007 na leo nimeona ni vema nami nijitokeze kuandika machache. Napenda kuishukuru na kuipongeza JF na uongozi na wanachama wake kwa kazi kubwa na nzuri manayoifanya katika kuleta changamoto mbalimbali.
Napenda kutoa mualiko rasmi kwa kuwakaribisha wana JF wenye mtazamo na mwelekeo wa kupenda maendeleo ya kweli kujiunga katika Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (Tanzania Professionals Network, TPN). TPN ni mtandao unaowaunganiasha wanataaluma wa fani mbalimbali bila kujali nafasi au vyeo vyao ikiwa na madhumuni ya kuwezeshana Wanataaluma na Wananchi kwa ujumla kiuchumi na kifedha.
Kwa kuwa michango mingi ya Wana-JF ni kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Watanzania na Nchi kwa ujumla (Kitu ambacho TPN pia inafanya), karibuni sana tuweze kuungana na kuonana katika mikutano ya mara kwa mara ambayo ina lengo la kuboresha maisha yetu.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea tovuti ya www.tpn.co.tz (Bado tovuti inaboreshwa . . . ). Tunakaribisha pia maoni yenu yenye mwelekeo wa kujenga na kuimarisha TPN.
Na kama kuna ufafanuzi wowote unahitajika, tafadhali tuwasiliane kupitia barua pepe president@tpn.co.tz au +255-754-833-985.