Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,120
Kama uliwahi kuambiwa duniani watu hufanana kwa sura tu basi huenda uliambiwa ukweli nusu, watu huweza kufafanua hata tabia, akili au fikra.
Kwa miaka mingi hapo kabla hapa JF alikuwa mwamba aliyejulikana kwa jina la Deo Kisandu, mwamba alitisha sana, alitingisha kwa mada nzito nzito za majigambo, mikwara, kujiamini, kuchanganya zikihusu siasa, sanaa, imani, elimu, afya na jamii. Mwamba alipitia madhila kibao ya kimaisha ikiwemo kupoteza kazi yake alioajiriwa na serikali na kufungwa jela. Wapo tuliombeza, wengine kumdhihaki na wengine kucheka tu. Lakini kwa uhakika, mwamba alikuwa na kitu na pia alikuwa na matatizo. Tulishindwa kutumia kitu alichokuwa nacho na pia tulishindwa kumsaidia. Huenda ni miaka 2 au zaidi sasa imepita bila Deo Kisandu kuonekana humu JF. Hakika tumemkosa sana!
Sasa sahau kuhusu Deo Kisandu, kuna mwamba mpya kabisa ameibuka humu JF anaitwa Dennis Roberts, yuko imara mnoo. Mwamba anajua vitu, anamwaga vitu hapa JF na anajiamini vilivyo. Yaani huyu kijana ni copy&paste ya Deo Kisandu. Mwamba anapita mule mule.
Afya ya akili ni muhimu.