JF Party On My Mind

JF Party On My Mind

Nimekua nikiwaza sana kwanini wana JF hatukutani hata mara moja kwa mwaka? Wengi mnaogopa kujulikana identity zenu lakini kwani ukija sehemu yenye watu 100 na ukajitambulisha wewe Gladys na huku unatumia Mzigua nani atakaekujua?
Tuacheni woga bwana tupangeni tukutane hata tugonge glass tubadilishane story mbili tatu atakaejitambulisha kwa Id yake itakua ni mapenzi yake.
Mkiunga mkono hoja wale waloandaa mwaka ulee tutawaomba waandae na mwaka huu tukutane maana ya mwaka ule inaniuma kweli kuikosa mpenda bata mimi.
Walevi utawajua tu
 
Enzi nikiwa anonymous niliona JF party ishatokea watu 'waligongana' balaa nanii zilikutana vya kutosha

Watoto walipatikana wa kutosha,michepuko ya kudumu na ya muda mfupi hewalaa

wenye akili walidaka madili ya maana

etc etc etc
 
Naunga mkono hoja
Mimi km tajiri mkuvwa hapa Dar nitagharamia vinywaji na chakula kwa wanaJf wote watakaojitokeza

Bila kusahau couples tatu zitakazopendeza zitapata nafasi ya kupiga lunch na dinner kwenye apartment yangu iliyopo Masaki kisha watalala hapo hadi majogoo
 
Back
Top Bottom