JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Pale UDSM Libary kuna sehemu inaitwa SPECIAL RESERVE. Ukienda pale wanazo kopi za magazeti hata ya miaka ya kuanzia 1920, yaani miaka 40 nyuma ya uhuru wetu. Kuna siku walikuwa wameyaleta kwenye maonyesho nilishangaa sana. Magazeti ya kipindi cha ukoloni wanayo na huwa wanatunza nakala kila siku hadi leo hii. Wasomi nao mambo yao ni ya ajabu sana, wanaweza kukusisimua katika kiwango cha ajabu sana
 
Kuna siku nitatafuta muda nikajisomee magazeti ya kabla ya uhuru nione walichokua wanajadiliana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…