Marehemu Georges Kiamuangana Mateta na bendi yake Veve, miaka ile ya 70 mwanzoni. Kuna kibao kimoja marehemu mzee wangu na marafiki zake walikuwa wanapenda sana kusikiliza, "NAKOMITUNAKA", ikimaanisha kwa Kiswahili "NINAJIULIZA". Kibao hicho kilipotoka miaka ile ya 70 kiliibua mitafaruku kwenye jamii nchini mule (Congo-Zaïre) mpaka Kanisa Katoliki nayo ilikuja juu kwa kutopenda maudhui ya wimbo huo uliosadikika kukufuru, Verkys na bendi ya Veve kupitia kibao hicho "NAKOMITUNAKA" walijiuliza, ngozi nyeusi ilitoka wapi? Kwa nini watakatifu, manabii ni wazungu? Na shetani inasadikika kuwa ni mtu mweusi kama anavyochorwa, kwa nini? Ninajiuliza Mungu wa watu weusi ni yupi? Mbona watakatifu weusi hawakubaliki?, N.K.
Inasadikika kuwa marehemu Georges Kiamuangana Mateta aliwekwa ndani kwa sababu ya kutunga na kutoa huo wimbo kwa kuwa ingeweza kuchagia machafuko.
Ninausikiliza huu wimbo sasa hivi, ninatafakari na kujiuliza maswali kama huyo marehemu...
[emoji848][emoji848][emoji848]
Ustaarabu haukuletwa na Waarabu au wazungu barani Afrika. Tulishastaarabika huko nyuma.
Sent using
Jamii Forums mobile app