Huyu anaitwa LETTA MBULU, yeye ndiye alieingiza yale maneno ya kiswahili "NAKUPENDA PIA NAKUTAKA PIA, MPENZI WEE" katika wimbo wa MICHAEL JACKSON uitwao LIBERIAN GIRL wa mwaka 1987 , kutoka kwenye album yake iliyoitwa BAD . LETTA MBULU na mume wake aitwae CAIPHUS SEMENYA ambao pia wote ni wanamuziki, walikuwa ni raia wa Afrika ya kusini waliokuwa wakiishi kama wakimbizi nchini Marekani wakati huo.
LETTA MBULU na CAIPHUS SEMENYA bado wapo na wanaishi jijini JOHANNESBURG nchi Afrika Kusini
.
Wahenga wengine hawakuwahi kujua.