JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Hii picha ya kumbukumbu ya wanamuziki mahiri kutoka mkoa tanga ilipigwa mwaka 1972
Hii ni bendi ya NEW STAR JAZZ BAND YA TANGA ILIKUWA NA WANAMUZIKI MAHIRI WAKIWEMO HAWA JAMAA
Tanga imejaliwa kutoa mwanamuziki wenye vipaji
Kutoka kushoto marehemu SULEIMAN MWANYILO (COMPUTE)
Kulia aliyesimama anaitwa HASSANI NGOMA huyu pia aliwahi kupigia Atomic kabla ya ujio wa john kijiko ndiye aliyepiga solo kwenye nyimbo ya "tanzania yetu nchi ya furaha na nyingine wewe afidha wangu
Mwingine anaitwa MOHAMEDI MODDY MRISHO huyu kwa sasa anapigia bendi ya kilimanjaro wana njenje anapiga vyombo mbalimbali likiwemo gitaa la solo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wangapi wanakumbuka shindano la ' Tusker project fame,lililovuma Sana kati kati mwa miaka ya 2000 chini ya udhamini wa Kampuni ya East African Breweries Limited?Wangapi wanamkumbuka mshiriki Mmoja maarufu Sana Kwa jina Hemed kutoka Dar Tanzania?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chakula cha h ubongo hapa ni "titanic"; ilizama mnamo 1912, Nan ikapatikana mnamo 1985 katika futi 12,500 za maji ya bahari yenye chumvi, miaka 111 baadaye na bado inaonekana nzuri na shinikizo la pauni 6000 kwa inchi ya mraba, lakini Chevy haiwezi kutengeneza gari ambalo linaweza kuishi ufukweni kwa miaka 11 bilamashimo ya kutu ndani yake



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duwa saidi wa simba akiruka juu kufunga goli maridadi akiunganisha mpira wa kona ilichongwa na Abdul mashine na kumuacha golikiba wa yanga steven nemes akigalagala chini na mabeki wa yanga wakibaki golini awana na kufanya
Mechi ilichezwa tarehe 26-9-1993
Mzunguko wa kwanza ligi ya muungano
Simba ilishinda goli moja kwa bila goli la duwa saidi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
MJUE MALIKIA MWAMI THERESA NTARE

Alipata nafasi ya kwenda kusoma Ulaya enzi ukoloni nafasi maalum za watoto wa machifu.Alihitimu mafunzo ya ya sheria.Alikuwa msaada mkubwa sana wa kisheria wakati wa kudai Uhuru,hasa kwenye mikataba ya kimataifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Britannic ndiye iliyokuwa mdogo zaidi kati ya meli tatu za stima za darasa la 'Olimpiki' za White Star Lines, kufuatia Titanic na Olimpiki. Hapo awali iliundwa kama mjengo wa Atlantiki, ilibadilishwa haraka kuwa meli ya hospitali kwa ajili ya huduma katika Mediterania wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia.

Kwa jukumu lake jipya, Britannic ilipakwa rangi nyeupe tena na misalaba nyekundu maarufu na mstari wa kijani mlalo, na ikapewa jina la HMHS (His Majesty's Hospital Ship) Britannic.

Mnamo Novemba 21, 1916, saa 8:12 asubuhi, ilipokuwa akisafiri kwa meli katika Bahari ya Aegean, Britannic aligonga mwamba rasi ya Ujerumani na kuzama ndani ya muda mfupi sana wa dakika 55. Ingawa watu 30 walipoteza maisha yao, tofauti na Titanic, wengi wa watu waliokuwemo (watu 1,035) walinusurika kuzama.

Kuzama kwa Britannic kunawakilisha upotezaji mkubwa zaidi wa meli wakati wa Vita vya Kwanza vya Kidunia. Kwa sababu ya ukubwa mkubwa wa meli hiyo na maji yenye kina kirefu ambayo ilizama (futi 400/122), ajali hiyo inasalia kuwa mojawapo ya ajali kubwa zaidi za meli za abiria ulimwenguni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…