JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

asanteni sana kwa historia hii thabiti na jadidi. kwa mara ya kwanza nimejua kuwa ndugu Putini ameishi hapa kwa miaka minne. natoa rai kwa Serikali kupitia mada kama hizi na kuzihifadhi na kuzitangaza. TBC kwanini hamna vipindi vyenye maana kama hivi??? punguzeni siasa mapambio mfundishe vijana historia kama hizi.
 


Josina Machel. mwanaharakati, Mwanamapinduzi, Mpigania uhuru wa Msumbiji, Mke wa kwanza wa Samora Machel Rais wa Msumbiji. binafsi namlinganisha na TAMARA BUNKE mwanamke jasiri msaidizi wa Major Ernesto CHE Guevara ama Salia Sanches Mwanamke shupavu Msaidizi wa Fidel Castro
Licha ya harakati zake Josina hakuonja matunda ya uhuru. alifariki na kuzikwa Dar es Salaam kabla ya uhuru wa Msumbiji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…