JF Scheduled Maintenance: June 13, 2020

JF Scheduled Maintenance: June 13, 2020

Hujaelewa swali lake mkuu. Anataka kujua ni kwann kila ikifika au kukaribia kipindi cha uchaguzi JF inazimwa?
Hakuuliza hivyo, lakini nimhakikishie kuwa hakuna kitu kama hicho. 2015 tuliposhambuliwa tulitoa taarifa na maandalizi ya sasa ni katika kuhakikisha hali hiyo haijirudii
 
Melo nina uzoefu na chaguzi mara nyingi unasema tutaweka miundo mbinu kadha wa kadha sasa najiuliza melo alisema anaweka ulinzi wa mtandao lakini ifikifika wakati wa uchaguzi utashangaa taarifa ,jamani kutokana na kadhia hii na hii mtandao haukuwa hewani rejea uchaguzi wa 2015
2015 kabla ya Uchaguzi hukuona maintenance notice kama hii. Hata hivyo, after the incident tulitoa taarifa ya kilichotokea na tulichofanya kukabiliana na mashambulizi yale.
 
Natamani mabadiliko haya yangewezekana kutokea.
1. Kuwe na dislike button
2. Member aweze kubadilisha jina (ID),
Vyote hivyo vimeishatolewa maelezo. Hata hivyo, namba moja(dislike button) ipo. Ila mimi nilikuwa mmoja wa waliokuwa wanapinga kitufe hiki. Mpaka sasa bado nina msimamo huo.
==
Mkuu, Melo, na jopo zima la ukarabati nawatakia kila la heri kwenye ukarabati huu mnaoenda kuufanya masaa kadha yajayo.
 
Vyote hivyo vimeishatolewa maelezo. Hata hivyo, namba moja ipo. Ila mimi nilikuwa mmoja wa waliokuwa wanapinga kitufe hiki. Mpaka sasa bado nina msimamo huo.
==
Mkuu, Melo, na jopo zima la ukarabati nawatakia kila la heri kwenye ukarabati huu mnaoenda kuufanya masaa kadha yajayo.
🤣 🤣 🤣 leo ndo najua, good
 
Safi
Wakuu,

Leo usiku wa manane, kati ya saa 8 na saa 10, tutakuwa na marekebisho kadha wa kadha katika miundombinu yetu yanayoweza kupelekea kusimama kwa baadhi ya huduma (na wakati flani huduma zote kusimama).

Hii ni katika kuimarisha zaidi miundombinu yetu na kuongeza uwezo wa kuhimili mikikimikiki yoyote inayoweza kutokea. Zoezi hili liliwahi kufanywa miaka 2 iliyopita lakini safari hii linatarajiwa kuchukua takribani dakika 30 hadi saa 1.

Tunapenda kutoa taarifa hii mapema ili mtu akiona kuna vitu haviko sawa muda huo asishtuke; ajue tupo kazini.

Endapo kutatokea lolote linalohitaji kushirikishana, tunaomba fuatilia kurasa zetu za Telegram - JamiiForums na Twitter - https://twitter.com/JamiiForums

Tunawashukuru kwa ushirikiano wenu katika kufanikisha zoezi hili.

/ Jamii Forums
 
Back
Top Bottom