JF special thread kwaajili ya Facts

JF special thread kwaajili ya Facts

Je wajua kitendo cha kupiga chafya moyo husimamisha mapigo kwa mda huo
Ni kweli..

Na unapozuia chafya kuna uwezekano:

1. Macho yakatoka nje.

2. Mishipa ya damu ya puani kupasuka hivyo kupelekea damu kuvuja puani.

3. Presha inaweza kuongezeka kwenye ubongo (intra-cranial pressure) jambo linaloweza kupelekea kuvilia damu ndani ya ubongo (intra-cerebral haemorrhage)

4. Msuli unaotenganisha kifua na tumbo unaofahamika kitaalamu kama diaphragm kuchanika.
 
Haswa Hilo hilo, Kuna viungo huwa havifanani aisee, Mimi hata miguu nikivaa kiatu lazima nibanwe kimoja kipwaye
Pumbu, mkono, na vidole vya mikono havilingani (kwangu)
 
Iko hivyo yani.

Kiujumla viungo vyote vya mwili ambavyo vipo bilateral (yaani viwili viwili) huwa vinatofautiana kwenye ukubwa na nafasi.

1. Figo ya kulia ipo chini kuliko figo ya kushoto kutokana na uwepo wa Ini.

2. Sikio lako moja ni dogo na jengine kubwa.

3. Mkono na mguu wako mmoja ni mrefu kuliko mwengine.

4. Katika mapafu yako, pafu la kushoto ni dogo kuliko la kulia.


Kila kitu kina sababu yake, ila kiimani tunasema "Binadamu hajakamilika"
Namba 3 Hapo siiamini Sana ila kwenye sikio nakubali.
Hata sura yenyewe imekaa upande kidogo Yani Kuna upande mmojawapo umeingia ndani kuliko upande mwingine.
Kuna wengine ukiwaangalia straight kutoka mbele unaona Kama jicho moja liko juu jingine liko kwa chini kumbe Ni sura ndo imekaa upande.
 
:-|
FB_IMG_16060361141909158.jpg
 
Back
Top Bottom