JF story time: Huu ndio wimbo uliomkutanisha Juma Nature na Majani and the rest was history

JF story time: Huu ndio wimbo uliomkutanisha Juma Nature na Majani and the rest was history

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
11,191
Reaction score
35,870
The legend mwenyewe Bony love alikuwa anafahamiana na Mabaga fresh, kundi la hip hop lilioshirikisha vijana wawili walemavu waliokuwa wanachana sana.

Plan ilikuwa bony love ndio awe muuandaji wa wimbo wa mabaga fresh lakini kwa bahati mbaya bony love akaibiwa vyombo ya utayarishaji wa muziki.

Ila kwa bahati nzuri bony love na p.funk majani walikuwa wanafahamiana na wanaishi karibu.

So, bony akamuomba p atayarishe wimbo wa mabaga, wakaekeana miadi na vijana walikuja kwa p kurekodi wimbo lakini hawakuja wenyewe walikuja na kijana mwingine alionekana mkimya bila mbwe mbwe zozote.

Kumbe alikuja ili kutia verse katika goma la mabaga fresh, ilifika zamu ya nature kuchana verse, aisee bony mwenyewe akashangazwa sana na uwezo wa nature na akamuambia "NILISIKIA UNATAFUTA WASANII WA KUSAINISHA BONGO FLAVA BASI MCHUKUE HUYO JAMAA"

Utabiri na ushauri wa bony love ulikuwa sahihi maana baada ya hapo majani alimtengeneza juma nature kuwa legend wa muziki wa bongo flava.

THAT'S IT


View: https://youtu.be/6cWOlHsiaPw?si=UVGe0TOmTVg9raBH
 
"kukataa ugali ujinga sio uboss,
Sana sana ukila utakua unapunguza mikosi"

By
Juma nature.
 
Back
Top Bottom