Episode 03
Na mende msafi
Previously in jf talk garden
@deogaratius kisandu: acheni upumbavu nyinyi..mbona mna wivu sana nyinyi. Kwanza tokeni hapa kama hamuwezi kuongea vya maana ntamwaga meno yenu wote chini hapa kwa teke moja tu.
Mod Two: (huku akimyooshea kirungu cheusi deo kisandu) we kisandu, kuwa mstaarabu tutakutoa nje sasa hivi.
Sasa endelea…..
Mende msafi anamwangalia mod two huku akiwa anacheka. mara watu wanaanza kusogea pembeni kwenda kumzunguka msichana Fulani aliyevalia kitop cheusi na kofia nyeusi. Mende msafi nae pia anaungana nao. Anapiga hatua huku mikono akiwa ameiweka mfukoni.
Anafika katika lile kundi lakini anakuta watu wengi wameshafika kabla yake hivyo anashindwa kumuaona mtu aliyekaa katikati. Mende msafi anasimamia vidole ili angalau amuone huyo mtu lakini hamwoni. Mende msafi anamshika mabega Principle girl ili apate balance ya kunyanyuka juu zaidi. Principle girl anageuka huku akiwa amekunja sura.
Principle girl: mkuu vipi, mbona tunashikana mabega tena aisee
mende msafi: samahani mkuu, nilikuwa nataka kupata balance ili nimuone huyo aliyekaa katikati.
Principle girl: kwa hiyo unanifanya tripod stand sio.
mende msafi: samahani mkuu.
Principle girl: usipende kitonga( kisha anasonya msonyo wa hamorapa)
Mende msafi anangalia pembeni kwa aibu. Anaangalia kama kuna watu walikuwa wanafuatilia yale mazungumzo, anamuona Kichwa Kichafu akiwa anamwangalia huku akicheka. Mende msafi anameza mate kisha anapiga hatua chache kulizunguka lile kundi la watu kisha anaangalia katikati, anamuaona mtu akiyekaa. Mtu huyo ni Demiss. Ameshika makaratasi na pen.
Demiss: (anasimama) jamani eeh, tulieni basi. mimi hapa nipo nachora katuni za memba wa humu. Kwa hiyo unataja jina la memba unayetaka nimchore. Ila kuna baadhi nilikuwa tayari nimeshazichora (anachomoa karatasi moja analiangalia kwa muda kisha anawaonyesha watu waliomzunguka. Karatasi hiyo imechorwa katuni ambayo kichwani kuna nywele zilizo nyolewa kwa staili ya kiduku huku miguu yake yute imeelekea upande wa kulia na pembeni yake kukiwa na redio ) huyo DJ Sepetu (watu wanacheka kwa sauti kubwa. The Tweet anaikwapua ile picha kutoka kwa Demiss na kikimbia nayo. Watu kadhaa wanatoka kwenda kwa The Tweet kuingalia ile picha. Demiss anachukua picha nyingine anawaonyesha watu. Karatasi hii imechorwa mtu anayekimbia huku miguu yake ikiwa imepinda kama upinde wa mvua. Halafu pembeni imeandikwa joseverest. Watu wanacheka kwa sauti.)
Watu wanaanza kupiga kelele kila mmoja akimtaja Yule ambaye anataka demiss amchore katuni yake. Demiss anachanganywa na kelele za wale watu anashindwa kuendelea kuchora. Demiss anasimama
Demiss: (kwa sauti ya pozi la kike)jamani si mtulie basi nachora ya mmoja mmoja jamani
Kichwa Kichafu: demiss naomba katuni ya mod, natumaini hautaniangusha.(watu wanacheka)
Mwifwa: kweli mkuu kichwa kichafu. Tena hiyo ndo iwe ya kwanza.
Demiss: mmh. My dears, mnataka nitimuliwe humu? (demiss anapiga hatua akitaka kutoka katikati ya kundi linalimzunguka)
Watu waliomzunguka demss wanamzuia na kumsukuma katikati alipokuwa huku wakimshinikiza aendelee kuchora. Wengine wanampigapiga kichwani na mabegani huku wakimlazimisha achore katuni za wengine haraka
Demiss: sasa basi tulieni jamani
Alosto anajipenyeza katikati ya kundi la watu na kunyakua kofia aliyovaa demiss na kukimbia nayo.
Demiss: jamaaaani. (ananyanyuka lakini watu wanamzuia, demiss anakaa chini na kuanza kulia)
goodfool: hahahahaha….wewe si ulijisifia hapa kuwa kuwa ulikuwa unaiba gest? Sasa wajanja wamekuotea na wewe.
Mara anakuja Nyani Ngabu anajipenyeza katikati na kwenda kumshika demiss na kumnyanyua.
Nyani Ngabu: (akiwa anawaangalia watu waliowazunguka) jamani eeh basi mwacheni mchuchu huyu aende akachore hizo katuni anawaleteeni kesho. Au vipi majita?
Watu wanapiga kelele kumpinga Nyani Ngabu. Wengine wanamsogolea kutaka kumpiga.
Nyani Ngabu: (kwa sauri ya kibabe na hasira) any one that will athropolize my crodert body and this cutefulized lady, I will trumptize him.
mende nsafi: (huku akimsukuma nyani ngabu) aaah kwenda zako na wewe na kiingereza chako cha kolomije.
Nyani Ngabu: (huku akimgeukia mende msafi) hey you dude, hivi unajua bei ya shati uliloligusa. Bei ya hiyo shati ni sawasawa na kontena 9 za makinikia, nauli ya bombadia kutoka dar hadi kwenu mara 14 na inabaki chenchi inayotosha kuwalisha ukoo wenu wote kwa siku 29. Don’t mess with me you basidiyomycota. (kisha anamshika demiss na kuanza kutoka pale katikati ya kundi la watu, watu wanawapisha.)
Nyani ngabu anatoka katikati ya watu kisha anageuka na uliangalia lile kundi
Nyani Ngabu: USA baby…(kisha anatoka nje ya jengo la chit chat akiwa na demiss)
Watu waliobaki wanabaki wanatizamana.
Je mende msafi ataikabili vipi hali ya kudharauliwa hadharani? Je demiss ataendelea kuchora katuni au ataacha? Tukutane katika episode ijayo.