Mheshimiwa mwenyekiti wa JEC.
Zimetimia siku tatu tangu nitoe malalamiko yangu kuhusu mmoja wa wagombea Bwana. NYANI NGABU... Kwa kuheshimu maamuzi na mapendekezo ya JEC kuwa inabidi huyu Bwana naye apewe nafasi ya kujitetea kabla JEC haijatoa hukumu na kwa kuzingatia na kuheshimu usawa, ilinibidi kuvumilia na kusubiri huku nikiwa na matumaini kuwa angalau huyu Bwana hata angekuja na kutoa tamko la kuwaomba radhi wana-JF aliowahi kuwaathiri kwa namna moja au nyingine. Mpaka dakika hii naona ameamua kukaa kimya hali inayonishawishi kuamini kuwa ameamua kupuuza agizo halali la JEC na kudhihirisha mojawapo ya sifa zake kuu: Dharau.
Hivyo basi, ninaomba kusikia tamko rasmi kutoka JEC juu ya malalamiko yangu pamoja na kitendo cha huyu Bwana kulipuuza agizo halali la JEC.
Vinginevyo nipate kuwasiliana na Wanasheria wenzangu ili tuamue nini kifanyike baada ya kusikia tamko halali la JEC.