Hivi kuna ushahidi kuwa hili ni matokeo ya kazi ya JF, au tunataka kudandia sifa za wengine?
Tusiwe tunajisifu kwa sifa tusizostahili...
Ahsante Tanzania 1 kwa uzalendo wako wa dhati na kwa kuinua gravitas ya mdahalo.
Bahati mbaya wanasema mambo mengine tuyaache kama yalivyo. Tupunguze jazba na malumbano. Tukitaka tuwasiliane nao pembeni pembeni watuambie ni kiongozi gani waliongea nae na ilikuwaje wanafunzi wakarudishwa.
Lakini viongozi wengi tunao wasulubu hapa nao wanaona ni jazba na malumbano, na kufuaitilia vitu vidogo vidogo. Kwa mfano, kutoka kwenye thread moja ya leo, Mtanzania wa kawaida anaweza asione ubaya wa kampuni ya Maji kutangaza jina la mkwepa bili. Lakini sisi tumekemea hili kama ni kuingilia mambo binafsi.
Hatuwezi kufuatilia vitu vidogo vidogo kwa wengine halafu sisi tukataka simile katika kutakana ukweli. Tutakosa uaminifu. Sio kwamba tunasaliti misheni yetu dhidi ya uozo wa Serikali na Mafisadi, isipokuwa tunataka baraza liwe na gravitas. Tunaposema, ngoja kidogo, hiyo sifa sio yetu, tunaonyesha objectivity. Objectivity itakayotusaidia siku tukisema 'Lodi Lofa jiuzulu,' kwamba haitaonekana kama ni 'jazba na malumbano ya kufuatilia vitu vidogo.'
Uwajibikaji unaanzia kwetu wenyewe, na kidogo kuliko vyote tunacho weza kufanya sisi 'arm-chair critics' ni pamoja na kuwa wakweli. Vinginevyo tutaonekana tunakaa nyuma ya vioo vya Komputa kubwabwaja tu, kama alivyo tuasa Mama Mwanaidi Maajar, ubalozi wa London. Sio kwamba ni malumbano na jazba na kufuatilia vitu vidogo, ila ni kutaka kujipima wenyewe katika viwango vile vile tunavyo wapima wengine.
Tanzania 1 ahsante tena kwa uzalendo wako.