Elections 2010 JF's Maxence LIVE on EATV "Uchaguzi Express Live"

Shukrani mkuu, tutaongea kupitia Radio, tulianza na Morning Star radio na leo itakuwa ni kupitia East Africa Radio.

Aidha, tutahitaji members kadhaa walio tayari kushiriki mijadala kwenye television na radio tuwasiliane nao ili tushiriki vipindi ambavyo wametuomba baadhi ya vyombo vya habari. Watakaokuwa tayari tuwasiliane ili tuweze kufahamishana ajenda kuu ni nini.
 
Sasa kutuweka sote ktk kapu la CHADEMA ni kuonesha huna upeo kuhusu JF na unayo tabia ya kutoa majumuisho marahisi bila ya kuwa na facts.
Hili itabidi niligusie kwenye radio, najua wataruhusu maswali; kuna uwezekano mkubwa likaulizwa. Shukrani kwa kutoa ufafanuzi mkuu
 
kwa umbumbumbu wake maxence ameshindwa kuwaambia watanzania kuwa hii jamii ni ya wachadema....! na kipindi kimeshaisha...!

Mimi sio Chadema ila nataka mabadiliko - Rais mpya. Chama kingine kuunda serikali!
 
kiongozi ukitoka tu hapo east-africa nitakuwa nakusubiri maryland nikupe kesto laiti zako tano tu
 
kiongozi ukitoka tu hapo east-africa nitakuwa nakusubiri maryland nikupe kesto laiti zako tano tu

Hahahahaaaaaa.......Then akishazimaliza akaitwa Clouds ataongea nini??? au Jamaa sio kichwa maji kama sie wengine Castle Mbili tu HOI?????
 

Sio Zaidi ya watanzania 500,000 ndio wana access ya internet. Na wengi wao wanatumia internet za maofisini hivyo hawako huru kwenye suala la Muda.

Wale wenye nazo majumbani au kwenye simu gharama yake ni Kubwa sana hivyo wanatumia kwa vitu vya ulazima.

Pia watanzania wengi hawajui internet ni burudani, na wanapenda muda wao free kuutumia kwenye Mabaa.

Ila JF ni makini kama waandishi wa habari watajiunga, na viongozi mbalimbali, kwani watapata nafasi ya kujua masuala mengi na kero nyingi.
 
Wale wenye nazo majumbani au kwenye simu gharama yake ni Kubwa sana hivyo wanatumia kwa vitu vya ulazima.
Mkuu, huo utafiti wako umeufanyia wapi? Sasa hivi Bongo kupata Access ya Internet ni pesa yako tu, Kwa mtu wa kipato cha kati hatashindwa kulipia Tsh 40,000/= kwa mwezi? na anapata unlimited up/dwn.... mimi nina net home/office na kwenye simu niko JF kwa masaa 5/8 kwa siku kutegemeana na muda nitakaoupata.

Mtaani kwangu 30% wana huduma ya mtandao.
 

Hongera sana Mkuu. NImeona clip ya mjadala mliokuwa nao EATV (shukran Mwanakijiji). Ni mwanzo mzuri.

Kutokana na mialiko kama hii, ni dhahiri kuwa JF inajulikana kwa walio wengi, hasa vijana. Nina ombi moja kuu. Nalo ni kutumia vizuri nafasi hizi vizuri kwa kuitangaza zaidi JF. Kwa mfano, katika kila usemacho, zungumzia JF (Kule JF tuna...., Kuna maoni yaliwahi kutolewa JF kuhusu ... n.k).

JF inatakiwa ikue kiasi ambacho itaweza kuwafikia watu wengi zaidi. Habari nyingi za nchi yetu zinapatikana mara moja JF. I call it a Web University.

Pamoja na kila kinachosemwa, JF ina bahati ya kutovumilia unafiki wa kisiasa au kimaadili. Kuna wengi hapa wa vyama mbalimbali ambao wanatoa maoni yao kwa heshima, bila kuvunja kanuni za JF na pia kwa kuheshimu maoni ya wengine.

Mkuu, nakutakia kila la kheri katika mijadala unaofuata katika media mbalimbali.
 
Max, ndio anajitambulisha kwenye radio, anasema anatoka JF.Mussa anasema kwa wale wanaopenda kuperuzi FB,TwT lazima watakuwa wanaujua huu mtandao wa JF. wamekwenda mapumziko kabla ya kuanza mjadala. Mjomba yuko hewani na kibao chake cha Adella
 
Max, ndio anajitambulisha kwenye radio, anasema anatoka JF.Mussa anasema kwa wale wanaopenda kuperuzi FB,TwT lazima watakuwa wanaujua huu mtandao wa JF. wamekwenda mapumziko kabla ya kuanza mjadala. Mjomba yuko hewani na kibao chake cha Adella

Ameanza kuhojiwa James, Niko Nairobi nawapata vizuri sana EA Radio!
 
Guys kwa wale ambao mna access na radio hivi sasa u may tune to East Africa Radio, JamiiForums ikiwakilishwa na Maxence Melo wapo live.

Ni review ya yale ambayo waliongelea jana kuhusiana na suala zima la uchaguzi, so kwa wale ambao hamkupata nafasi ya kuona live jana basi mna nafasi ya kusikia leo.

-wamegusia suala la usawa katika vyombo vya habari kuwahabarisha wananchi.
 
ni jamaa wa JF aliyeongea mwishoni ndo katoa point za ukweli wengine hasa huyo dada wa YTVA ni longo longo za face book., bravoo max.
 
Kwa Max anavishukuru vyombo vya habari na mitandao mingine. Anaviponda vyombo vya habari vinavyopendelea vyama fulani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…