Wakuu kumradhi, ilikuwa kipindi hicho wawepo Synovate, nilichotarajia tujadili sicho kilichojadilika hivyo ikabidi twende kadiri inavyowezekana na kuongea na vijana kupitia TV ya vijana EATV.
Hii leo saa 4 asubuhi nitakuwa East Africa Radio; hapa natambua naongea na watu wazima wengi na si wa Tanzania pekee bali na wale wa Kenya na Uganda wamo.
Kuna vitu nimeona kuwa itabidi tuvifanyie ufafanuzi:
- JF inatembelewa na watu si pungufu ya 12,000 kwa siku; watu hawa wanaoitembelea si watu wa kupenda siasa tu, si watanzania tu n.k. Aidha kila mmoja anakaa ndani ya JF kwa wastani wa dakika 15 akiiperuzi (huu si muda mdogo). Kwa mwezi (August stats) JF inapata hits milioni 60+
- Asilimia 67.2 ya watembeleaji wa JF ni kutoka Tanzania
- Watumiaji wa JF mpaka sasa walio wengi ni umri wa miaka 25 na kuendelea mpaka miaka 44, wengi ni wahitimu wa vyuo walau.
- JF ipo ranked kuwa ndani ya tovuti 35,000 (nafasi ya 34,544 hadi naandika) kutembelewa sana ulimwenguni (tembelea Alexa - Jamiiforums.com Site Info ) na ni ya kwanza Tanzania kuwa na wasomaji wengi (japo Alexa huwa hawaandiki hilo, unaweza kujaribu mwenyewe kulinganisha na tovuti nyingine)
- JF ni user generated content website. Kila anayejisajili anaweza kuanzisha hoja na ikajadiliwa (kama inajadilika) na registration ipo huru kwa kila mmoja
- JF si mali ya CHAMA wala MTU flani, hoja zilizoandikwa na watu zinamilikiwa na watu hao zikisimamiwa na waendeshaji wa JF. Kila mwana JF ni mmiliki wa alichokiandika, anapata uwezo wa kuki-edit au kukiondosha anapoamua. Ukiwa mwanachama na ukashiriki mjadala wowote unakuwa umejiweka katika familia ya wana JF.
Sidhani kama nilikosea kuwataja baadhi ya wanachama wenye kutumia majina yao halisi bila kujali wapo chama gani; nakumbuka nilimtaja Nape, nadhani nilimsahau Bashe pia, hawa tunao ni jambo la heri kuwa wapo tayari kwa debate.
Kila mtu ana haki ya kutoa mawazo yake, kila mmoja anavyoona inastahili, tunayazingatia. Tunachofanya ni kuiangalia mijadala isiharibiwe kwa kuzingatia sheria tulizojiwekea.
Kwa wale wanaoi-access JF via mobiles endapo kutakuwa na matatizo (test period) tunaomba tufahamishwe ili turekebishe kabla hatujaja na kitu kipya Oktoba hii.
Shukrani wakuu