Jiajiri kwa mtaji chini ya Shilingi 50,000 na utengeneze faida mpaka 20,000 au zaidi kwa siku

Jiajiri kwa mtaji chini ya Shilingi 50,000 na utengeneze faida mpaka 20,000 au zaidi kwa siku

Digital base

Senior Member
Joined
Jul 19, 2020
Posts
131
Reaction score
199
Habari ya leo wakuu, poleni na mihangaiko ya kila siku,leo nna vitu 7 natamani kuwashirikisha vijana wenzangu wanao hitaji kujikwamua katika hari ya maisha duni tuliyo nayo.

katika mambo haya muhimu ni bidii na kujitoa ndo njia pekee itakayo kuinua toka chini mpaka viwango vya juu kulingana na mahitaji yako ama malengo yako husika. Karibu.

1. KUSAFISHA SOFA ZA VITAMBAA
Vifaa:

Una nunua dawa ya kusafishia sofa dukani lita 1 inayo tosha kusafisha sofa set 1 ya watu 5 kwa 13,000 ikiwa zaidi unaongeza dawa maana hata faida ni kubwa,una nunua vitambaa vikubwa viwili kwa 500.

Then una tafuta mtu wa masoko wa kukusaidia kutafuta wateja wako majumbani na maeneo mbalimbali huku mkishirikiana na wewe ila kila mmoja anaenda eneo lake yeye una mlipa kwa kamisheni ikiwa ata pata mteja.

Na gharama za kusafisha sofa kwa set 1 ni kuanzia 50,000 mpaka 80,000 kulingana na ukubwa wa set ama makubaliano na mteja wako.

2. KUNG'ARISHA MASINK
Vifaa:

Una nunua dawa ya kung'arisha masink dukani 5000 kwa lita 1, brash ngumu 1 ndogo ya 2500, gloves ngumu za 5000 ambazo ni za kusafisha tu baada ya kazi,Mask ya 1000.

Then una tafuta mtu wa masoko wa kusaidia kutafuta tenda za aina hiyo huku nawewe ukiendelea kutafuta wateja yeye uta mlipa kwa kamisheni kila mteja anaye kuletea.

Dawa hiyo ina ng'arisha sink lililo na uchafu sugu ama kufubaa na kurudisha kuwa jipya kabisa.

Gharama za kung'arisha sink 1 la kawaida ni 7000 na la kukaa ni 10,000 maelekezo ya kutumia dawa una mwagia sink lote then una usubiri kwa dk.20 kabla ya kusugua.

Lita 1 ina tosha masink 4 maana una mwagia kidogo tu,kazi hii utaiweza ikiwa tu hauna kinyaa.

3. KUNG'ARISHA TILES ZA CHINI NA UKUTANI
Vifaa:

Una nunua dawa (Tiles cleaner) kwa bei ya 4200 kwa lita 1 hapo una chuku kuanzia lita 2,Brash ngumu kubwa 1 kwa 3500, Gloves kwa 5000, Mask kwa 1000 na miwani kujikinga macho.

Kisha una tafuta wateja wako kwa njia unayo ona inaku faa.

Matumizi ya dawa una mwagia sehemu zilizo na uchafu sugu then una tandaza na brash kila eneo kwa tiles zote Kisha una iacha kwa dk.15 kabla ya kusugua.

Gharama za kung'arisha Tiles za chini na zajuu kwa choo/bafu 1 ni kuanzia 20,000 kulingana na makubaliano yenu na mteja wako.Matumizi ya dawa ni lita 1 kwa bafu 1.

4. KUNG'ARISHA VIOO VYA ALMINIUM MAJUMBANI NA MAOFISINI
Vifaa:

Una nunua dawa ya kung'arisha vioo achana na ya kusafishia tu ipo ya kung'arisha ina uzwa 5000 kwa Lita 1,una nunua magazeti ya 1000,vitambaa viwili kwa gharama ya Tsh.2000 kila kimoja kina tumika tofauti,una mwagia dawa kidogo sana then una sugua muda huo huo kwa kitambaa kisha una chovya kitambaa cha pili kwenye maji safi una sugua kioo kisha una kausha kwa magazeti.
Ghama za kusafisha kwa dirisha 1 ni kuanzia 2000 mpaka 3500 kulingana na ukubwa wa dirisha na matumizi ya hiyo dawa ina tosha madirisha 10 makubwa.

5. MOBILE CAR WASH
Vifaa:

Una nunua dawa ya kusafishia magari isiyo hitaji maji mengi wakati wa kusuuza,una nunua dawa ya kusafishia sofa ikiwa kuna uhitjai wa kusafisha seats za gari,una nunua vitambaa vya kufutia wakati wa kuondoa maji maji,maji Lita 10 magazeti ya kufutia maji kwenye vioo.

Gharama mna kubaliana na mteja wako ila ni kuanzia 5000 kwa gari 1 kama ni pamoja na kung'arisha seats gharama inaongezeka.

6. KUJI FUNZA KUTENGENEZA SABUNI ZA MAJI,MICHE & ZA UNGA NA KUZI UZA
Vifaa:

Una nunua malighafi kulingana na unacho taka kutengeneza gharama za mali ghafi zinatofautiana kulingana na maeneo uliyopo.Ikiwa hujui unaweza kutafuta mwalimu wa ujasiriamali akupe mafunzo kwa wiki 1 tu utakuwa una jua kila kitu.Hiyo ni biashara ya uhakika maana una zalisha sabuni nyingi kwa gharama ndogo ila wewe una pata faida nzuri.

7. KUTENGENEZA DAWA ZA USAFI AINA ZOTE
Vifaa:
Una nunua malighafi zako kulingana na nini una taka kutengeneza,mfano kuna dawa ya kung'arisha Tiles zilizo fubaa ama kuwa na uchafu sugu, dawa ya kung'arisha Masink yaliyo fubaa ama kuwa na uchafu sugu aina zote za masink.

Hizo ni dawa zenye soko kubwa sana katika Hotel, Shule, vyuo na watu wanao jihusisha na usafi pia we mwenyewe utakuwa mteja wa bidhaa zako ikiwa uta pata tenda ya usafi sehemu yoyote ile. Kutengeneza dawa za kusafishia sofa,dawa za kuondoa madoa kwenye nguo nyeupe pia dawa ya kuondoa madoa kwenye nguo za rangi, dawa za kuua wadudu kama mende na kunguni pia ni dawa zenye soko kubwa katika Hotel, Hospital, Viwandan, Lodges na maeneo yote ya public services na gharama za mali ghafi hazi zidi 30,000 kutoa Lita 20 za dawa na gharama zake ni 5000 kwa dawa za kusafishia Tiles na masink,13,000 dawa za kusafishia sofa,15,000 kwa Lita dawa ya kuua wadudu n.k.

Hivyo ikiwa ume hangaika kutafuta fursa ya kuku ingizia kipato jaribu na hizo pia huenda uka pata kitu kipya.
Mfano wa kazi nnazo ongelea nilizo fanya mimi picha za kabla na baada ya kusafisha Tiles za chini
IMG_20210429_145944_264.jpg

IMG_20210430_113422_375.jpg

IMG_20210430_113431_172.jpg
 
Habari ya leo wakuu, poleni na mihangaiko ya kila siku,leo nna vitu 7 natamani kuwashirikisha vijana wenzangu wanao hitaji kujikwamua katika hari ya maisha duni tuliyo nayo.

katika mambo haya muhimu ni bidii na kujitoa ndo njia pekee itakayo kuinua toka chini mpaka viwango vya juu kulingana na mahitaji yako ama malengo yako husika. Karibu.
Unafanya ipi kati ya hizo?!
 
Habari ya leo wakuu, poleni na mihangaiko ya kila siku,leo nna vitu 7 natamani kuwashirikisha vijana wenzangu wanao hitaji kujikwamua katika hari ya maisha duni tuliyo nayo.

katika mambo haya muhimu ni bidii na kujitoa ndo njia pekee itakayo kuinua toka chini mpaka viwango vya juu kulingana na mahitaji yako ama malengo yako husika. Karibu.
Big up sana mkuu, uko vizuri na shukrani kwa kushare nasi
 
Tupe recommendation ya hizo dawa za kusafisha tiles na masink za uhakika. Kanjanja nyingi madukani
Nzuri zaidi za kutengeneza mwenyewe mkuu ikiwa uta hitaji nitafute kwa mafunzo ya siku 1 tu kwa upande wa dawa za kung'arishia Tiles na masink au zote unazo taka wewe
 
Dawa ya kusafishia masofa inaitwaje na zinapatikana wapi
Mimi mara nyingi huwa natumia bidhaa nnazo tengeneza mwenyewe ila ukienda maduka ya bidhaa za urembo na usafi uta pata wewe waambie nna shida na dawa ya kusafishia sofa
 
Somo zuri sana. Naamini umelitoa kwa hiari ya kusaidia tu na si vinginevyo. Sasaaaa tuambie ni bidhaa gani tununue au tufundishe jinsi ya kutengeneza hizo dawa/sabuni kama jinsi wewe unavyotengeneza! Umeamua kutusaidia usisite! kama pia lilikuwa tangazo la biashara tuambie
 
Back
Top Bottom